M4C: Lema aelekea Ujerumani

Nashukuru kwa ushauri in fact sio ushauri mmbaya ila nijibu Swali moja tuu. Je Unajua operation sangra na M4C vinavoendelea Moro na kwingineko? Chadema nzima iko vijijini ni Lema peke Yake Ndio anapiga jaramba ughaibuni sasa sioni kinacho haribika kwa Lema pekee kutokuweko vijijini ilihali uongozi wote uko vijijini kwa sasa. Ingekuwa Hakuna mtu aliyeenda kujenga chama vijijini na badala Yake wawe na Lema uko wote apo ningekugongea like mpaka za ziada ila kwa hili ndugu nisamehe sijashawishika nasisitiza Asante kwa ushauri



Ubishi ni kipaji kama vilivyo vipaji vingine vyote ambavyo mwanadamu kajaaliwa na Mungu, narudia tena hiki cdm wanachofanya si sahihi, lazima tuwashauri kuwa raslimali chache walizonazo wahakikishe wanazitumia vizuri, na nguvu zao waelekeze vijijini maana huko ndio kuna wajinga wengi wa elimu ya urai na ccm wanautumia ujinga wa hao wa vijijini kama mtaji wao wa kisiasa. sasa kama huu ushauri unuona hauna mashiko au unakuhalalishia kuwa mimi ni ccm.sina cha kufanya kwani hayo yatakuwa matatizo yako.
 
JIULIZE KWANZA, unajua busara ni raslimali adimu sana, nikikundekeza wewe utanifanya nitumie ya kwangu ndivyo sivyo kama unavyo pendekeza cdm watumie raslimali chache walizo nazo.
 
Mnatumia kodi zetu vibaya, badala mfungue matawi vijijini mnakimbilia nchi za nje, hivi kuna manufaa gani huko? Naipenda chadema ila kwa mwendo napata wasiwasi nanyi. Hizo garama anazotumia ni za kwake binafsi au za chama? Si ruzuku hio? Kodi zetu? Upuuzi mtupu makamanda wangu mnaoufanya. Huku serengeti hatuna matawi ya chama, sasa hapo mnajitanua nje huku ndani pamejaa? Watz hebu tuache hizi siasa uchwara!
umechoka hamia ccm
 
wakati mwingine nashindwa kuwaelewa hawa cdm, nilitegemea nisikie aelekea kijiji fulani, hawa wa majuu siunaweza kutana nao huku mtandaoni, hebu tumieni akili imarisheni chama vijijini acheni ulimbukeni kama hawa wengine.
uzuri wake umesema wakati mwingine unashindwa kuwaelewa CHADEMA kama kipindi hi ambapo wanasambaza itikadi nje na ndani yaani UK sasa Ujerumani huku wanaanzisha rasmi operation Sangara leo Huko kirombero itakayo zagaa nchi nzima

kimsingi uko sawa kutowaelewa maana hii kasi haikutegewa hata kidogo. ila ungekuwa na akili japo kidogo tu ungejilazimisha kubaini umuhimu wa matawi nje ya nchi ila kwa sasa endelea kutowaelewa hawa jamaa hadi 2014 jibu utalipata tu
 
Duble Chris, umenifurahisha kuwa ningekuwa na akili hata kdg, inawezekana naandika haya tokea mirembe hospital kwa mtazamo wako. ila wewe mwenye akili umeshindwa kuona maneno "acheni ulimbukene kama hawa wengine" katika hayo uliyo ninukuu, unajua kwa mtu asiye na akili hata kidogo kama mimi namuona lema na cdm, kwa hili la kwenda majuu, wanafanya siasa za mipasho kuwa nape kaenda usa ngoja na sisi twende uk, sasa hiyo ndio priorty yenu. wasio na akili kama mimi always watawaona mnachemsha hasa pale watakapo kua wanawapa ushauri wa bure nyie mkaendelea kubisha just for the sake of it.
 
HIVI TUNAENDA WAPI NA HAYA MATAWI YA CDM? KWANINI TUSIFUNGUE HATA OFISI ZA CHAMA VIJIJINI? SASA UJERUMANI HAO WAJERUMANI WATAPIGA KURA? Tufungue matawi hata ya nyumba moja hapa kwetu TANZANIA.USHAURI TU.

Ushauri: Elewa kuwa anaenda kukutana na Watanzania wanaoishi huko Ujerumani. Wanaoruhusiwa kupiga kura hapa nchini ni watanzania tu
 
Najua siku hizi dunia imekuwa kama kijiji ila nachelea kukubali kuwa Lema yuko Germany maana nimemuona pale mahakamani akiwa na Marando wakimpongeza Balozi Mahalu. Someone has to prove me wrong with concrete answers
 
Yaani wewe kwenye CDM viongozi woooote hawafai ila isipokuwa Zitto....kweli CDM inawasababishia watu msongo wa mawazo
Kumbe hili unalitambua...
Huo ndio ukweli, wengine waliobaki wote ni wapayukaji tu. Bado wapo low sanaa kwenye dhana nzima ya uongozi
 
Acha kutuzuga, mbona yupo nchini leo alikuwa anamlaki Costa Mahalu pale mahakama ya Kisutu? Jamaa yupo bongo tu
Magamba bwana,umeambiwa Ujerumani ni sawa na Tegeta -Posta?watu wameendelea wakati liserikali lenu dhaifu la magamba hakiwezi hata kupeleka wanamichezo olimpiki...ukichukua flight from Germany to dar unawahi kufika kuliko ukiwa na daladala kutoka tegeta to posta!!!Shame on you na magamba yenu!!
 
Jamani wadau hapa jamvini mimi ni kada wa chadema na mfuasi wa siasa anazofanya lema lakini tusimamie kwenye ukweli na tuache uzushi,jana nimemuona lema pale mahakama ya kisutu wakati wa hukumu ya kesi ya mahalu uko ujerumani kaenda lini ?
 
Back
Top Bottom