M4C kuibomoa CCM

Bitabo

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,900
687
Kwa jinsi upepo unavyokwenda, naanza kuiona Movement for Change ikiibomoa CCM mda si mrefu. Hawa wakuu hawako mbali sana kujiunga na M4C. nadhani Zitto atakuwa anaratibu mchakato huu.

Nape Nnauye
Janauary Makamba
Faustine Ndugulile
Deo Filikunjombe
Samuel Sitta
Edward Lowasa
Harisson Mwakyembe
....
...
....
ongezea wengine kama unakubaliana na M4C japo hao kwenye bold sioni wakikubaliwa kujiunga na M4C.
 
Hatutaki mamluki, chadema itaandaa makamanda wake pasipo kutegemea kina shibuda type!
 
WANAOITWA NI WENGI ILA WATEULE NI WACHACHE. CHADEMA NI MTEULE WA WAtZ
 
Hapo juu nimekupa asilimia 100, kwa Deo Filikujombe peke yake, wengne tupa kule hatuwahtaj...!
 
Hao wengine kama akina EL, DM na Six wakikaribishwa wataibomoa kabisa CDM asubuhi na mapema. Kwanza kwa kuiondolea mvuto kwa umma. Hii ni sawa na kuchukua uozo ulioifanya ccm ikose mvuto na kuukumbatia.
 
Ilipofikia, hatuhitaji masaza, bali vijana wenye nguvu na moyo na ambao wapo fiti kupambana na magamba na SIO hao ndumilakuwili, huku wataka na kule wataka kama naniiih. Si tunapigana kule yy analeta habari za urais sijui madudu gani then anakuwa wa kwanza kutueleza mpira unazunguka vp.. !!
 
James Lembeli
Ole Sendeka - Ingawa ni mnafiki sana
Charles Kitwanga (Mawe matatu)

Majimbo mengine yapo rehani 2015 tunachukua kikubwa ni M4C ihubiriwe kwa sana.
 
Kwa jinsi upepo unavyokwenda, naanza kuiona Movement for Change ikiibomoa CCM mda si mrefu. Hawa wakuu hawako mbali sana kujiunga na M4C. nadhani Zitto atakuwa anaratibu mchakato huu.

Nape Nnauye
Janauary Makamba
Faustine Ndugulile
Deo Filikunjombe
Samuel Sitta
Edward Lowasa
Harisson Mwakyembe
....
...
....
ongezea wengine kama unakubaliana na M4C japo hao kwenye bold sioni wakikubaliwa kujiunga na M4C.

Bora Nape
 
Nakubali kabisa M4C itaharakisha mabadiliko, ila jamani huku pwani namaanisha dsm,pwani,Lindi,Mtwara tutengeze streategy special ili ukombozi utimie. naona vikwaaza vya mabadiliko ktk sehemu hizo
 
Jamesi Lembeli ni wetu toka kitambo ata kuwa mbunge wa cdm kule kule jiomboni kwake. wengine ni Beatrec Shelukindo na ...................................
 
Ni kweli M4C ndio mkakati wa kuelekea kuizika ccm, lakini kwamba lengo ni kuvua samaki ccm na kuwahamishia cdm hapo sikubaliani na wewe, ccm inapaswa kubomolewa ili kifike mahali makada wengi wainue mikono juu kwenye siasa (wajiuzulu) halafu new era ianze kuchukua nafasi maana kuna wengi wanauwezo wakiwezeshwa hakuna sababu ya kutegemea mamluki..
 
Naomba nikukumbushe kauli ya Mbowe na Zitto, CHADEMA "tunalea vijana hili waweze kuwa viongozi wa wazalendo, wanaochukia rushwa na wako tayari kwaajili ya nchi yao". Tumeweza kufika hapa pasipo kutengemea wafuasi wa CCM kuhasi kambi zao na kuhamia CDM. Pamoja tunaweza leta mabdiliko, CDM inajivunia vijana masikini kutoka katika familia masikini.
 
Nakubali kabisa M4C itaharakisha mabadiliko, ila jamani huku pwani namaanisha dsm,pwani,Lindi,Mtwara tutengeze streategy special ili ukombozi utimie. naona vikwaaza vya mabadiliko ktk sehemu hizo
Ukombozi barani Afrika haukutokea mara moja ulienea pole pole.
 
Nasema hivi hayo majina yamekuwa common mno masikioni mwetu tumezaliwa tumeyakuta tunazeeka tukiwa tunayasikia. Nchi hii in vijana na mabinti wa kutosha kukomboa nchi yao hatuitaji hao makapi. Wakae huko huko CCM kwao ili ife wakiwemo ndani yake.
 
Back
Top Bottom