M4C Kimanga (Picha moja)

MAGAMBA a.k.a WADHAIFU jana waliandika humu JF kuwa raia walio hudhuria walikuwa chini ya arobaini (40)

Achana nao tujenge chama letu CHADEMA, lengo letu kwa kijana ajitahidi angalau kupata wanachama 10.Pia hao ni wageni wa mabadiliko hivi vyama wakati vinaanza vilikuwa haina idadi kama hiyo,kutoka kwenye sifuri hadi 40 hapo chama kinakua.Hata kama hawakuzidi 40 walokuwepo wanatosha, aluta continua mapambano bado yanaelendelea.
 
Weye kweli giza, lini CHADEMa ilifanya mkutano sehemu hiyo ikapata idadi kama hiyo?

Hivi wewe hunapajua Tabata Kimanga? Kwanza hakuna uwanja mkutano umefanyika barabarani na barabara za Kimanga ni nyembamba sana na watu wamejibana hapo lazima uone watu wengi.
 
Unaweza ukazungungumza na watu 40 nakila mmoja akapeleka habari kwa watu 25 tu tayari ni wengi mno. Idadi si hoja hasa kama wamekuja wenyewe.
 
attachment.php
 
Pipozi Pawa Mungu yuko nanyi amini haya nisemayo .It is about time watu wako mbolewe View attachment 57322 wadau. habar zenu binafsi. hii ni picha niliyofanikiwa kuipiga kwa kutumia kisimu changu cha laini mbili. hawa ni sehemu ya wakazi wa Kimanga waliohudhuria 'somo' la mabadiliko lililokuwa likitolewa kwa ufasaha na makamanda wetu, Mh. Godbless Lema, na mtu mzima, miaka 80, Mh. Mzee Philemon Ndesamburo. kwa umati umati huu Mungu ashukuriwe mwelekeo ni mzuri viva piposss pawaaaaaaaaaaaaaaaaa naweza tu kuwahakikishia kuwa hakukuwa na msafara wa aina yoyote kwenda kwenye mkutano ule, mimi huwa nashinda Mawenzi (ambapo msafara wowote wa magari ukiwa unaelekea Kimanga lazima upitie hapo). sikuona mbwembwe za aina hiyo. kila mtu alienda kivyake bila kusukumwa wala kutishwa. Dondoo: 1. Kamanda Lema alizungumzia sana ishu ya udini na namna inavyotumiwa vibaya na watu wa ccm, kwa lengo la kuwagawa na kuwatawala Watanzania. Somo lilieleweka vema, kwa kila muislam na mkristo aliyehudhuria, na kwa wale ambao hamkuhudhuria eleweni hivyo. Lema pia akadai ccm wamekuwa wakieneza propaganda kuwa chadema ni chama cha wachaga, akaeleze kuwa huo ni uwongo uliopindukia, lakini pia akahoji, hivi kipi cha maana basi? kwamba tumkatae mtu kwa uchaga wake, lakini akija mvutabange, mwizi, mbadhirifu wa mali za umma tumchague kutuongoza ati kwa vile siyo mchaga? Alihoji. 2. Ndesamburo aliwalaumu wananchi wa Dar Es Salaam kwa uwoga na kukosa uthubutu. Akarejea jimbo lake la moshi kwa namna ambavyo limekuwa mahala salama kwa watanzania waishio huko, tangu mwaka 2000 lipo chini ya chadema likiwa na huduma zote muhimu za kijamii, na pia ndiyo jiji linaloongoza kwa usafi kulinganisha na majiji mengine. Akaendelea kusema mwaka 2000, mkapa, akiwa Rais alijaribu kutumia vibaya madaraka yake ya urais kwa kumtisha msimamizi wa uchaguzi kuwa wamtangaze mgombea wa ccm kuwa mshindi, lakini vijana wa pipoz pawa walikuwa macho, tayari kwa lolote, askari wakanywea na mzee ndesapesa akaukwaa ubunge. 3. Diwani wa Kipawa ni jembe. Mama anachana kama 2-Pac Shakur. yeye aliwashauri kina mama waamke. wanadanganywa kwa kanga na vilemba vya kuteleza wanaisaliti nchi. Yalikuwa mengi. na ama hakika kufikia mwaka 2015, wengi watakuwa wameamka kutoka usingizini na mabadiliko ya kweli yatafikiwa. Pipozi Pawa Mungu yuko nanyi amini haya nisemayo .It is about time watu wako mbolewe
kwa umati umati huu Mungu ashukuriwe mwelekeo ni mzuri viva piposss pawaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
jana kuna wadhaifu walikua wanatoa updates utadhani walikua eneo la tukio, m4c inawanyoa kotekote.....
T2015CDM HIYOOOOOOOO MAGOGONI!
 
Nimeipenda hii habari ya kunenepesha mifupa. Ndo maana naipenda JF. Jamani Dr. SLaa yuko wapi hatumsikii au amepewa likizo kidogo.
 
Hivi wewe hunapajua Tabata Kimanga? Kwanza hakuna uwanja mkutano umefanyika barabarani na barabara za Kimanga ni nyembamba sana na watu wamejibana hapo lazima uone watu wengi.

Nakujua Tabata Kimanga na naishi,mkutano umefanyika kituo cha mabasi na barabara ilifungwa kutokana na uwingi wa watu.Huo ulikuwa mkutano wa kata,mikutano ilofanyika maeneo yale huo ni wa tatu.Zito,Mpendazoe na Lema ila huu wa Lema ulikuwa na watu wengi sana na ambao umevunja rekodi ya mikutano yote ya CHADEMA.Kama bado unakaubishi,nitakugharimia nauli ya kwenda eneo hilo kwa siku yeyote unayoona inafaa.Idadi ya walojiunga ni wengi sana,pole sana indelea na kaubishi ka kimagamba magamba.
 
mheshima mnyika ameyasema yote bungeni bila uwoga kwani hakuna asye jua kuwa serikali ni dhaifu na udhaifu wake umetokana na mheshimiwa rais kulea watu wanaofanya ubadhilifu wa fedha za uma
Kwa udhaifu umeanzia kwake rais ndo maana mnyika alitoa kauli hiyo kwa kujiamini bila kuogopa
 
Wale wazee walokuwa wakilia kutoka na hutuba ya Ndg Lema, nao kama una picha zao ziweke.Na pia Lema alipoacha gari yake kuwahi majukumu ya chama nayo iweke kama ipo, tuacha ubinafsi Lema anakubarika kwani jana gari yake vijana walitakaa kuisukuma ila alikataa, alipopanda bodaboda alishangiliwa sana na watu.Lengo letu jimbo la Segerea 2015 liwe chini ya CHaDEMA.

usihofu nitaziweka mkuu. Hawa magamba nyeupe wao wanaona nyeusi, wala msitumie nguvu nyingi kuwaelewesha. Uwezo wao wa kufikiri umezibwa na gamba.
 
usihofu nitaziweka mkuu. Hawa magamba nyeupe wao wanaona nyeusi, wala msitumie nguvu nyingi kuwaelewesha. Uwezo wao wa kufikiri umezibwa na gamba.

Ipo sawa ila kuwapa dawa kwa kaugonjwa sio mbaya, unajua mwenyeenzi Rabi hamfichi mnafiki na hao gambaz aka nyinyiemu jana kutwa walikuwa wanahangaika na habari za kinafiki.Lakini baadae wameumbuka hata leo ukiwaambia jana Lema kashangiliwa sana na wapenda mabadiliko watagoma.Ila wasiachwe lazima tuendelee kuwapiga makonzi kichwa,kwa staili za mbwa mwitu yaani wakigeuka huku kwenzi kule kwenzi na bado mbaka magamba yote yapukutike.
 
View attachment 57322


wadau. habar zenu binafsi.

hii ni picha niliyofanikiwa kuipiga kwa kutumia kisimu changu cha laini mbili. hawa ni sehemu ya wakazi wa Kimanga waliohudhuria 'somo' la mabadiliko lililokuwa likitolewa kwa ufasaha na makamanda wetu, Mh. Godbless Lema, na mtu mzima, miaka 80, Mh. Mzee Philemon Ndesamburo.

naweza tu kuwahakikishia kuwa hakukuwa na msafara wa aina yoyote kwenda kwenye mkutano ule, mimi huwa nashinda Mawenzi (ambapo msafara wowote wa magari ukiwa unaelekea Kimanga lazima upitie hapo). sikuona mbwembwe za aina hiyo. kila mtu alienda kivyake bila kusukumwa wala kutishwa.

Dondoo:
1. Kamanda Lema alizungumzia sana ishu ya udini na namna inavyotumiwa vibaya na watu wa ccm, kwa lengo la kuwagawa na kuwatawala Watanzania. Somo lilieleweka vema, kwa kila muislam na mkristo aliyehudhuria, na kwa wale ambao hamkuhudhuria eleweni hivyo.

Lema pia akadai ccm wamekuwa wakieneza propaganda kuwa chadema ni chama cha wachaga, akaeleze kuwa huo ni uwongo uliopindukia, lakini pia akahoji, hivi kipi cha maana basi? kwamba tumkatae mtu kwa uchaga wake, lakini akija mvutabange, mwizi, mbadhirifu wa mali za umma tumchague kutuongoza ati kwa vile siyo mchaga? Alihoji.

2. Ndesamburo aliwalaumu wananchi wa Dar Es Salaam kwa uwoga na kukosa uthubutu. Akarejea jimbo lake la moshi kwa namna ambavyo limekuwa mahala salama kwa watanzania waishio huko, tangu mwaka 2000 lipo chini ya chadema likiwa na huduma zote muhimu za kijamii, na pia ndiyo jiji linaloongoza kwa usafi kulinganisha na majiji mengine. Akaendelea kusema mwaka 2000, mkapa, akiwa Rais alijaribu kutumia vibaya madaraka yake ya urais kwa kumtisha msimamizi wa uchaguzi kuwa wamtangaze mgombea wa ccm kuwa mshindi, lakini vijana wa pipoz pawa walikuwa macho, tayari kwa lolote, askari wakanywea na mzee ndesapesa akaukwaa ubunge.

3. Diwani wa Kipawa ni jembe. Mama anachana kama 2-Pac Shakur. yeye aliwashauri kina mama waamke. wanadanganywa kwa kanga na vilemba vya kuteleza wanaisaliti nchi.

Yalikuwa mengi. na ama hakika kufikia mwaka 2015, wengi watakuwa wameamka kutoka usingizini na mabadiliko ya kweli yatafikiwa.

Pipooooooooooooz!
Sahihisho mkuu,huyo diwani niwa kata ya Kimanga mkuu....nashikuru kwa habari tuliwakilisha vyema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom