M4C Kimanga (Picha moja)

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Kimanga-mwisho.jpg

wadau. habar zenu binafsi.

hii ni picha niliyofanikiwa kuipiga kwa kutumia kisimu changu cha laini mbili. hawa ni sehemu ya wakazi wa Kimanga waliohudhuria 'somo' la mabadiliko lililokuwa likitolewa kwa ufasaha na makamanda wetu, Mh. Godbless Lema, na mtu mzima, miaka 80, Mh. Mzee Philemon Ndesamburo.

naweza tu kuwahakikishia kuwa hakukuwa na msafara wa aina yoyote kwenda kwenye mkutano ule, mimi huwa nashinda Mawenzi (ambapo msafara wowote wa magari ukiwa unaelekea Kimanga lazima upitie hapo). sikuona mbwembwe za aina hiyo. kila mtu alienda kivyake bila kusukumwa wala kutishwa.

Dondoo:
1. Kamanda Lema alizungumzia sana ishu ya udini na namna inavyotumiwa vibaya na watu wa ccm, kwa lengo la kuwagawa na kuwatawala Watanzania. Somo lilieleweka vema, kwa kila muislam na mkristo aliyehudhuria, na kwa wale ambao hamkuhudhuria eleweni hivyo.

Lema pia akadai ccm wamekuwa wakieneza propaganda kuwa chadema ni chama cha wachaga, akaeleze kuwa huo ni uwongo uliopindukia, lakini pia akahoji, hivi kipi cha maana basi? kwamba tumkatae mtu kwa uchaga wake, lakini akija mvutabange, mwizi, mbadhirifu wa mali za umma tumchague kutuongoza ati kwa vile siyo mchaga? Alihoji.

2. Ndesamburo aliwalaumu wananchi wa Dar Es Salaam kwa uwoga na kukosa uthubutu. Akarejea jimbo lake la moshi kwa namna ambavyo limekuwa mahala salama kwa watanzania waishio huko, tangu mwaka 2000 lipo chini ya chadema likiwa na huduma zote muhimu za kijamii, na pia ndiyo jiji linaloongoza kwa usafi kulinganisha na majiji mengine. Akaendelea kusema mwaka 2000, mkapa, akiwa Rais alijaribu kutumia vibaya madaraka yake ya urais kwa kumtisha msimamizi wa uchaguzi kuwa wamtangaze mgombea wa ccm kuwa mshindi, lakini vijana wa pipoz pawa walikuwa macho, tayari kwa lolote, askari wakanywea na mzee ndesapesa akaukwaa ubunge.

3. Diwani wa Kipawa ni jembe. Mama anachana kama 2-Pac Shakur. yeye aliwashauri kina mama waamke. wanadanganywa kwa kanga na vilemba vya kuteleza wanaisaliti nchi.

Yalikuwa mengi. na ama hakika kufikia mwaka 2015, wengi watakuwa wameamka kutoka usingizini na mabadiliko ya kweli yatafikiwa.

Pipooooooooooooz!
 
Pipozi Pawa Mungu yuko nanyi amini haya nisemayo .It is about time watu wako
mbolewe View attachment 57322

mbolewe
 
Pamoja na propaganda zao za udini na ukanda,
M4C haitawabakiza magamba 2015 CDM itakuwa Magogoni.
 
M4c! Haimbakizi mtu hakika!
2015 ndiyo msema kweli!

Watanzania watakuwa wameamka toka usingizini tayari!

Tunashukuru kwa news Kamanda!
 
Presha inawapanda na kuwashuka magamba, ila wao ndo waliichezea bahati wakajipange upya kama hawatokufa
 
NDesa pesa hujakosea mzee wangu,watu wa dar ni waoga sana wamezidiwa na wakerewe,na watakuwa ni watu wa mwisho kubadilika licha ya kuwa mjini.nape baada ya jangwani sijamsikia tena
 
Naamini wale wenye Mapenzi mema na nchi yetu wanaelewa CDM si chama cha wachaga na si cha wakristo, Ni muhimu waislam na wengine mkawa sehemu ya Mabadiliko ya kweli na mkajiunga na CDM tuondoe ufukara nchi mwetu. Tanzania bila ccm Inawezekana kabisa
 
nitaongeza picha nyingine baadae. Kisimu changu cha mchina kinasumbua kuupload.

Wale wazee walokuwa wakilia kutoka na hutuba ya Ndg Lema, nao kama una picha zao ziweke.Na pia Lema alipoacha gari yake kuwahi majukumu ya chama nayo iweke kama ipo, tuacha ubinafsi Lema anakubarika kwani jana gari yake vijana walitakaa kuisukuma ila alikataa, alipopanda bodaboda alishangiliwa sana na watu.Lengo letu jimbo la Segerea 2015 liwe chini ya CHaDEMA.
 
MAGAMBA a.k.a WADHAIFU jana waliandika humu JF kuwa raia walio hudhuria walikuwa chini ya arobaini (40)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom