M4C imekosewa mahesabu haitafanikiwa

Logic ni kufundisha elimu ya uraiya na kutafuta mtaji mkubwa wa kura z 2015, hatuvizii bali tunajitokeza mapema coz tuna bonafide.

Elimu ya uraia ingeweza kutolewa kwa approach nyingine sio hii ya M4C..kwa kufanya hivyo utakua unatumia silaha kubwa kwa swala mdogo....utakubaliana na mm M4C ingetumika vzr ndio ingesaidia CDM kushika dola...so what next after M4C..kuna silaha kubwa zaidi ya hii ya kuchange mind za watu kwa maana ya wingi wao?

Khs kutafuta mtaji wa 2015 sikubaliani na wewe kbs...,mtaji wa CDM hautokani na kutafutwa na wao unatokana na udhaifu wa CCM kutoshughulikia kero za wananchi na kutotambua viongozi bora badala yake wanachukua bora kiongozi kwa faida ya mitandao yao ndani ya chama. matokeo yake hata wazuri wa CCM ndio wanakuja CDM ebu niambie ni nani wa CDM ambaye hakupitia CCM akabaniwa ndio akasepea CDM??/
 
Nayo tungechelewa mngesema kuwa mmepokea watu bila kuwapima, pia mngewalaumu watz tu kuwa oohh msikurupuke CDM hawana timu inayoelewana....

Watanzania tutapoteza muda kwa kuvutana na kuyumbishana kwa hoja hapa.....

Umuhimu wa kuwahi ni kwamba kuna changamoto zitatokea kwa kupokea watu wapya plus mapandikizi kama Shibuda, chama kitapimwa kwa uwezo wake kuzivuka changamoto hizo.......

Tusiyumbishane hapa jenga chama kwa nafasi yako
 
...labda alijitangaza yeye zaidi ya chama.

Na akumbuke muamko na uelewa wa Tanzania kipindi cha Mrema yuko kwenye peak ndio ulikua kama alio nao sasa hv huyo RIBOSOME,Watanzania wa leo wengi wamesha elimika sana,na ndio wanaoiumiza na kuizika c.c.m!!!Mzindakaya alishawaonya C.c.m Watanzania wa leo sio wakuwadanganya kwa amani na utulivu,kwani wame elimika na wanataka maendeleo
 
Alichokozea Mrema, kwanza alikuwa very weak academically. So far CCM wakatumia vyema udhaifu wake huo kumkolimba kisiasa. Na ndiyo maana mpaka leo anarufu ya CCM.
Unaweza tuwekea CV ya Mwenyekiti wa chadema tuilinganishe na ya Mrema? Nakuhakikishia huwezi, itakuumbua.
 
Siasa hutegemea sana upepo unavyovuma. Kwa sasa wengi wameanza kuingia CDM toka CCM tukianza na Milya kule Arusha na kufuatiwa na wana CCM kibao. Sasa mh unataka wasubiri nini? Wakisubiri watakuwa wamechelewa. Upepo wa kasi umeanza kuvuma wenyewe, na huu ndio wakati mwafaka wa msafiri kutia mashua yake ktk bahari na kuacha ipelekwe huko upepo unakokwenda.

Kumbuka, kizazi hiki si kizazi cha kucheza nacho. Hiki ni kizazi kinachotaka mabadiliko, maisha mazuri, na maendeleo ya kweli. Ni kizazi ambacho hakitadanganywa tena. Kizazi cha CCM kimeshaanza kupotea, wazee wetu hawana nguvu tena ya kutetea chama cha Nyerere. Watoto wao sasa wameamka. Ni nani atakayewazimisha?
 
Tundu Lissu, Kabwe, Halima, Mbilinyi etc hawakuwahi kua wanachama wa c.c.m! Na kutoka c.c.m kuhamia CDM hiyo ni hoja dhaifu sana, Watanzania wanataka mabadiliko inategemea hayo mabadiliko wanataka wayapate kupitia chama gani,unategemea Slaa wa C.c.m ndio huyu wa Cdm? Ndio maana Cdm ni chama pinzani,tena chenye nguvu!
 
Kuna mtu aliyekuwa anakusanya watu wengi kwenye mikutano zaidi ya Mrema?

Muulizeni alikosea wapi?
tumia ubongo kidogo wewee. mrema ni mtu cdm ni chama. tena chama makini ndio maana wana nyinyi m wanajileta wenyewe.
 
Ebu niambie kwann leo?mie nimekwambia impact amabayo ingekuwepo M4C ingeanza 2013...!we niambie logic na impact yake kwa kuanza shv.
Kaka nimekuelewa....tena sana. Lakini kumbuka kuwa chama hakijengwi siku moja.

Kuna maeneo mengi sana CDM haijafika. Kazi kubwa iko Dodoma, Singida, Tabora, Lindi, Mtwara, Sumbawanga, Iringa, Pwani, Dar, Tanga na Zanzibar. Huko kote watu wanahitaji ukombozi. Hii movement haitakuwa na maana kama CDM tutaacha na kurest. Lakin kwa sababu tumeamua kuchangia chama, tutahakikisha kuwa Operation hizi zinaendelea hadi 2015. Na hapo ndipo utaona faida yake.

Kaka kumbuka huu msemo wa kidhungu.....THE EARLIER THE BETTER.

Unataka tushtuke kumekucha!!!!!????
 
Tundu Lissu,Kabwe,Halima,Mbilinyi etc hawakuwahi kua wanachama wa c.c.m!na kutoka c.c.m kuhamia CDM hiyo ni hoja dhaifu sana,Watanzania wanataka mabadiliko inategemea hayo mabadiliko wanataka wayapate kupitia chama gani,unategemea Slaa wa C.c.m ndio huyu wa Cdm?ndio maana Cdm ni chama pinzani,tena chenye nguvu!
Una uhakika na hao uliowataja hawakuanzia CCM??? Fuatilia kadi zao za mwanzo kwenye safari zao za siasa... sio kila aliyehama alitoka akiwa na cheo kama Shibuda fikiri kabla haujajibu
 
Mleta thread, ana mawazo kama ya fisi. Fisi hufuata binadamu kwa nyuma, kwa matarajio kuwa anavyorusha mikono, mbele nyuma, itafika mahali itanyofoka, kumbe ni maumbile ya binadamu ndivyo alivyo. Magamba endeleeni kusema chadema inakufa kesho, kesho mpaka 2015 IKULU. Shauri yenu.
 
Kuna mtu aliyekuwa anakusanya watu wengi kwenye mikutano zaidi ya Mrema?

Muulizeni alikosea wapi?

Ribosome, wakati ule mikutano ya Mrema ilikuwa mikubwa lakini huewezi linganisha na ya CDM.
Mwisho, ile ilikuwa mikutano ya Mrema binasfsi lakini CDM hawana mikutano ya Slaa au Mbowe bali CDM.
 
Una uhakika na hao uliowataja hawakuanzia CCM??? Fuatilia kadi zao za mwanzo kwenye safari zao za siasa... sio kila aliyehama alitoka akiwa na cheo kama Shibuda fikiri kabla haujajibu

Mbilinyi nina uhakika kwa kua i knw well him back in a days,Lissu nae nina uhakika kwa kua nilisoma makala yake kwy gazeti moja last year na alisema katika maisha yake hata kabla ya mfumo wa vyama vingi hajawahi kua mwanachama wa c.c.m,na hakuna aliyewahi kumpinga!
 
..wanachotakiwa kufanya CCM ni kutekeleza ahadi zote walizotoa ktk uchaguzi.

..pia washughulike na matatizo kama kupanda kwa gharama za maisha, mfumo mbovu wa elimu, matatizo ya umeme, matatizo ya maji, huduma za afya, kumaliza kabisa tatizo la ufisadi, etc etc.

..CCM wanatakiwa kufanya kazi waliyotumwa na wapiga kura, badala ya kuhangaika kuwashambulia Chadema.

Hapa mkuu umenena kitu ambacho CCM hawakioni. Wanadhani kuimaliza CDM ni kuingiza migogoro kwa kuwatumia kina Shibuda et al. Ulichoongea hapo ni njia mujarab ya kuimaliza CDM nguvu. Kwanza kabisa wawashitaki wale wote waliokuwa implicated kwenye Richmond, Dowans na mpaka Epa na wahukumiwe kifungo cha maisha bila kujali status zao ndani ya CCM.

Kama CCM wanafikiria kusubiri mwaka wa uchaguzi ndiyo waanze kuwajaza watu mapesa watakuwa wamechelewa sana kwani watanzania wamekuwa kama 'KUNGURU WA ZENJI', Kunguru wale hapo mwanzo ilikuwa rahisi sana kuwauwa kwa jiwe au manati, lakini jinsi walivyokuwa wanakumbana na tragedy zile yaani mtu akiina tu na kuokota kitu na kuwarushia wanaona mwenzao anaanguka na kufa, mtu akishika kitu na kukivuta kisha kuachia wanaona mwenzao anaanguka na kufa. Wakajua kuwa 'Mwanadamu hana kibyongo akiinama anaokota dongo' basi hata ukiinama kujikuna wao wanaruka, wakiwa hewani ukinyoosha mikono juu wanajua manati wanaruka. Vivyo hivyo kwa watanzania wanajua kuwa 'CCM si wakweli wakikupa kula wanataka kura kisha kukuacha na njaa miaka mitano.

Anyesema timing ya CDM ni mbovu haoni mbali na hajui nini maana ya Politics. You have to capitalise at a time where most people can hear your msg. Nikikwambia mimi binafsi japo sina Chama wala sitarajii, kama mpiga kura itawagharimu sana CCM kunishawishi kuwa they are genuine on peoples concern ili niwapigie kura uchaguzi wa 2015 kama ntajaaliwa kufika. Ila kama watatekeleza hayo yaliyoorodheshwa na Jokakuu ninakuhakikisha kuwa sitakuwa na shida kuchagua wa kumpigia kura.

Kulindana na ufisadi ni adui mkubwa wa CCM na wasiposhughulikia hilo hasira ya wananchi itawaangukia labla wafanye mapinduzi ya kijeshi ama kipolisi baada ya kushindwa uchaguzi na kukatalia madaraka kwa kuchakachua.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom