M4C Bukoba Mjini Inaanza Kuleta Matokeo!

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,429
1,045
Leo niko napitapita kwenye vijiwe mbalimbali hapa BK mjini. Nimejulishwa kuwa katika Mkutano wa Mbunge uliofanyika hivi karibuni, wananchi wamempa ishara ya taa nyekundu Kagasheki.

Simulizi liko hivi:

Hivi karibuni Lwakatare, Anthony Komu, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala-CDM
na kijana mmoja toka Singida ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu-CDM walikuja Kagera kwa programme ya kichama ya kuwanoa madiwani wa CDM. Baada ya Programme, Chama-Mkoa kikawaandalia mkutano wa hadhara.
44.jpg


Wakati wa kuhutubia, Kijana toka Singida akamwaga sumu kwa kuwaambia watu waliohudhuria mkutanoni kuwa; msitegemee lolote jipya toka kwa Kagasheki eti kwa kuwa amekuwa Waziri Kamili. Akawaambia labda niwape swali akija mmuulize hivi “Twiga wetu wanarudi lini?” Akashindilia zaidi kwa kuwaambia, ukiwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Usalama wa Taifa, Polisi, na Magereza vyote vinakuwa chini ya Wizara yako. Na hakuna mtu anaweza kuja na ndege akachukua wanyama wakubwa na akaondoka bila kubugudhiwa kama Usalama wa Taifa hawahusiki. Kwa hiyo Kagasheki asiwazuge, akija mmulize Twiga wetu wanarudishwa lini?

Siku chache Kagasheki akatua BK na akafanya mkutano wa hadhara. Wakati mkutano ukiendelea, Vijana wakaanza kiutani kumnyooshea vidole viwili.
1.jpg


Taratibu miguno ikaanza kusikika huku ikisindikizwa na maneno “Tunataka Twiga wetu” Ghafla Kagasheki akahamaki na kukosa uvumilivu, akaanza kurusha maneno hovyo. Ikawa ndo kama kawapa watu ruhusa kupiga chorus kwa sauti za “Tunataka Twiga wetu” na “Twiga wetu wanarudi lini” Mzee wa watu akaendelea kurusha meneno hovyo “Najua hao ni CHADEMA” mara “hao CDM watachukua majimbo mengine huko kote lakini nawahakikishia hili hawatalipata” Kutokana na mvulugano huu, kwa wale wanaomfahamu Kagasheki akiisha panic hawezi kulejea haraka katika control. Ikabidi mkutano uishe

Baada ya kurejea Jijini, haraka sana Kagasheki akatangaza hatua zinazochukuliwa kuwarejesha Wanyama wetu walioibiwa

Haya ndo nimewakusanyia kwa leo toka vijiwe nilivyotembelea hapa BK Mjini.
 
Bottom line ni kwamba Hamis Kagasheki anastahili kuwajibishwa kutokana na kashfa ya Twiga wetu kwa sababu wakati wa tukio hilo alikuwa naibu waziri wizara ya mabo ya ndani, Hii wizara ya utalii itamtesa sana kwani tayari faru wa kikwete George ameuawa siku cha che baada ya kagasheki kuingia wizarani pale, majuzi majambazi wamevamia kambi ya watalii na kuua watu wawili akiwemo mtalii mmoja, Kagasheki pull up your socks vinginevyo wizara ya utalii ndio ya mwisho kwako
 
Kama kuna watu wanatulet down basi ni watu wa mkoa wa Kagera ukiondoa kule home Biharamulo tu!!!!!!!
 
Hizo picha mbili zimenisikitisha sana. Inaonekana huko kwetu BK bado watu wanaabudu CCM. Ebu chunguza hizo picha uone mkusanyiko mkubwa uko wapi. Wahaya sijui wamekuwaje. Ujasiri wao uliotokana na usomi wao umekwenda wapi? Nani kawaloga? CCM nka yatwita si Mulangira.
 
si mshangai Kagasheki viongozi wengi ccm wanafikiria vyeo vyao ni vya kudumu maisha, wana mawazo ya kikamuzu Banda, Niwashauri wakati unawakataa Hamtakiwi tena ccm
 
Back
Top Bottom