M-Pesa, Tigopesa n.k. ni utapeli mwingine?

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Naomba tujaribu kuchangia hapa!

Nilitaka kujua tu M PESA inafanyaje kazi.

Kwanza nilitafuta sheria yetu inasemaje. Kwamba kila taasisi inayojishughulisha na fedha lazima iwe imepata leseni toka Benki kuu ya Tanzania. Kufanya kinyume na haya ni kuvunja sheria za nchi kwa mujibu wa THE BANKING AND FINANCIAL INSTITUTIONS ACT 2006. Nimepitia kote, FINANCIAL INSTITUTIONS, COMMERCIAL BANKS na hata REGIONAL UNIT BANKS hakuna pahala Vodacom, Tigo wala Airtel wamesajiliwa kufanya biashara ya fedha! Kwa hili linanituma kusema kuwa hawafanyi biashara kihalali na hii inaweza kuliingizia hasara kubwa Taifa hili.

Wataalamu wa VODACOM wanasema kuwa ukitumia huduma ya M PESA lazima transaction zako lazima ziende Uingereza then zirudi kwenye mitambo ya Vodacom Tanzania. Ina maana kuwa Benki Kuu ya Tanzania haihusiki ku- monitor chochote kwenye hizi huduma.

Kama ni kweli BOT hawana muingiliano na hizi taasisi je ikitokea siku moja Voda ama Airtel ama Tigo wakasema database yao imecrush itakuwaje?

Je ina maana kuwa BOT (T) hawajui hilo ama wanafumba macho kwa personal interest za watu wengine?

Kuna pia fununu nimeisikia kuwa VODACOM walifanya party pale Dodoma kwa ajili ya waheshimiwa na kila mtu akaondoka na kibahasha kinono ili kuwafumba macho ( sina uhakika sana ila kama kweli watatuambia humu).

Naomba kuwasilsha

EM
 
Kama vile umetoa maneno mdomoni mwangu. And I tell you kuna siku zikikusanywa billions of money in their data bases, surely the system will crush and that will be the end of the deal kama ilivyotokea kwenye DECI.

Wataalamu wa IT tuambieni, uwezekana huo haupo? Au na benki ni hivyo hivyo, lakini huko kuna hard copy nadhani???? back up system ikoje ya haya makampuni, anyway tuna haki ya ku-raise reasonable doubt!!!!
 
kama vile umetoa maneno mdomoni mwangu. And I tell you kuna siku zikikusanywa billions of money in their data bases, surely the system will crush and that will be the end of the deal kama ilivyotokea kwenye DECI. Wataalamu wa IT tuambieni, uwezekana huo haupo? Au na benki ni hivyo hivyo, lakini huko kuna hard copy nadhani???? back up system ikoje ya haya makampuni, anyway tuna haki ya ku-raise reasonable doubt!!!!

Angalao Benki Kuu watueleze njia hii ni salama? Na je wateja wengine huwa na kiasi kadhaa kwenye simu zao. Ikitokea mteja amepatwa na kifo (hatuombei hayo) fedha ya huyu mteja hurudishwaje?
 
Kimya ina maana kuna ukweli ndani yake. Mimi naamini hata humu watu wamechelea kujibu kwa sababu ama wanajua ukweli au wanalinda maslahi yao. Mimi natoa anagalizo WATANZANIA TUWE MACHO NA HIZI BENKI AMBAZO SIO RASMI ZITATUFIKISHA PABAYA.
 
Fanyeni utafit kuhusu hilo msiongee tu jambo ambalo hamjafanya utafiti kwa kina .. Umetaja sheria hapo juu je umewahi kuuliza mamlaka husika kuhusu hilo.. Je, umewahi kuthibitisha kwamba hizo kampuni hazina kibali cha kufanya hvyo au kuangalia kampuni hzo katika usajili wake hzo huduma za pesa hakuna.

Kama kumbukumbu zangu zko sahihi Vodacom ndo wakwanza kuanzisha hii na kwenye uzinduzi wake alikua amehudhuria Waziri wa fedha wakati alikua Zakia na gavana wa BOT. Sasa sijui kama na wao walikieendea kitu ambacho hawakijui au vp.

Ila sibishi kama haiwez kuwa utapeli ila kufanya utafit wa kina ni vizur zaid kabla ujasema chochote.
 
Acha kukurupuka mleta mada.

Hawa jamaa wana a/c bank iliyounganishwa na system zao.

Mfano mawakala wa Tigo pesa na M-pesa huwa wanaenda bank mara kwa mara kujaza" flot".

Fanya utafiti kabla yakuongea
 
Umesoma ila Elimu yako bado haijakusaidia ktk kufikiri mambo, kumbuka hawa watu wana akaunti benki Na zko connected Na system zao hvyo Wao wanasimama Kama mawakala wa banki kwa brand names zao. Na ndio mana mtu kuweka flot kwenye till zao hawaendi tigo wala zoda wanaenda benki.

Ushauri thread nzuri but heading uko wrong ungeliza badala yakutuhumu mdau..
 
Nimeshangaa juzi natoa 500,000 tsh kutoka Tigopesa makato ni 7,000 tsh. Yaani ni shida hii mitandao. Ni bora huduma za kibenki aiseee.

Sirudii tena kufanya miamala na hii mitandao ya simu..
 
Nimeshangaa juzi natoa 500,000 tsh kutoka tigopesa makato ni 7,000 tsh. Yaani ni shida hii mitandao. Ni bora huduma za kibenki aiseee. Sirudii tena kufanya miamala na hii mitandao ya simu


Mpango kurudi bank tuu, mtego,huu
 
Uko sawa mkuu kwa kiasi flan hivi ila hizi huduma zimerahisisha maisha kwa kiasi flani ila shida hapo kwenye makato kila mwaka wanapandisha hadi kero
 
Mimi nauliza je, kama mteja wa hizi Huduma either amepata ajari na kufa papo hapo na kwenye simu alikuwa na pesa hii pesa nani huwa ananufaika nayo?.
 
Back
Top Bottom