M-PESA.TIGO PESA na MAHUSIANO...

Hivi wakuu hakuna line isiyo na huu ujinga ujinga wa dash dash PESA ili niwe nasema line yangu haitumagi hela??????????????
 
Yaani acha tu, hapa nilipo sasa hivi kuna mtu kanishtukiza eti nimtumie hela kapungukiwa na elfu 30 ya kusuka, namtafutia jibu la kimjibu hapa, wadada wanafikiri pesa hazina mipango mda wote, enzi hizo hakuna huu ujinga ilikuwa raha kweli, ngoja nimjibu mtandao haupatikani nazani wameblock my tigo pesa account
Nyie nanyi mnanishangaza. . .
Unafikiria jibu la kumjibu wakati tayari jibu liko wazi?Mwambie huna. . .ebooo!!! Wanaume wazima mnakua kama wavulana bana, au ni wavulana?
 
mmh mie maisha yangu yamekuwa marahisi haswa na izi huduma kwangu nying faida si hasara ,
wadhamini kibao yan duuh! ki ukweli wanajigonga wenyewe mie sikatai tuma baba!
 
Hivi wakuu hakuna line isiyo na huu ujinga ujinga wa dash dash PESA ili niwe nasema line yangu haitumagi hela??????????????
teh kwani anakulazimisha yan kujisumbua si unasema tu sitaki au sina!
tatizo mnapenda kujikweza ivyo tutumieni tu sie tunapokea.
kizuri ni kwamba ww mwenyewe unaenda kunitumia lolz, kwa mapenzi yako! coz nikiomba sio lazima unipe na wengi wenu mnajiongezaga wenyewe bana.
 
Ukikitumia kitu vibaya lazima upate athari zake....btw Boss naomba umwambie Lily Flower hapo chini namsalimia sana..muulize kama ana M PESA nimtumie hela ya kununua mchicha nasikia siku hizi umepanda bei fungu linauzwa buku...

Mkuu....choooonde... kibubu chetu usikivunjage...
 
mimi nilishakula vichwa vingi saaaana kwa njia hii
ujue inakuwaje
cheki hii
mpesa man: upo smile
smile :nipo my dear

mpesa man:ushakula baby wangu
smile fix: nimefulia dia leo sili

mpesa man:mmmh baby wangu usile na mimi nipo nikufate?
smile: hapana boss yupo siruhusiwi kutoka leo

mpesaman: basi nakutumia hela kidogo ya lunch.

smile:usjali dear usijitese nipo ok

mpesa man:nimekutumia laki moja dear laki si pesa mbonaa?
smile:mmmh thax anyway bye dia






idumu milele huduma ya mpesa na tigo pesa

Ha..ha..ha Kumbe ndio majina tunayopachikwa haya.M-pesa Man!! dah umeniacha hoi.Most women deserve an Oscar when it comes to this act.
 
lolz! hii mitandao ina umuhimu wake jaman, kama unaitumia vibaya sawa utajuta tu siku zote.
mie tangu haya makitu yaweintroduced dah maisha yangu yamekuwa marahisi mara 200 lolz.
tanx to founders wa haya mambo aisee, well done guyz.
 
Hahahaaa nicheke kwa afya yangu mie. . Ukizaliwa mwanaume tabu kwelikweli mie hata nilikuwa sijawaza eti kuna watu hii huduma imekuwa kero kwao lol. .ukiona mwanaume anasoma msg anakuna kichwa saivi si bure anatafuta jibu. .No network. .Lol lol. .
 
hii mitandao ya simu pesa imesaidia sana kwa wale ambao wana adabu au wanaiheshimu matumizi yake , kwani kwanza imerahisisha ukaribu wa kutuma na kupokea pesa hasa unapokuwa umekwama au umepata tatizo ni rahisi sana kuliko hata banks ...
ila waleeee wengine ndo imekuwa ni sehemu ya kusumbua au kuleta usumbufu maana kila mara ninaomba nauli nitumie kwenye tigo pesa etc sasa ukikaa ukajiuliza hata ukimtumia buku na gharama zake ni ngapi na nini mantiki ya hilo haiji kichwani
 
Ndoa hazivunjiki kwa sababu ya simu, zinavunjika kwa watu kutumia vibaya simu. Huwezi ukamkuta mtu anaetumia simu yake ipasavyo anajikuta matatani kwajili ya simu.

Acheni kusingizia simu na hizo sijui MPESA. . .Kwani mtu anakulazimisha untumie mtu pesa?Kama una akili yako mwenyewe unafanyaje kitu ambacho hupendi tena bila ya kulazimishwa?

tatizo lako wewe umeelewa angle moja tu
wenzio tunazungumzia angle zote
wala kutuma sio tatizo
wapo wanaofurahia pia kutuma na kuhonga kwa njia hii
na wanao hongwa ndo wanapata matatizo
tunazungumzia kwa ujumla wake
 
Ha..ha..ha Kumbe ndio majina tunayopachikwa haya.M-pesa Man!! dah umeniacha hoi.Most women deserve an Oscar when it comes to this act.

umeonaa ehh?
wewe umem save eti wife to be
yeye kaku save tigo pesa lol
 
huu ni ujumbe kwa wanaume
tugome kujiandikisha m pesa na tigo pesa
mimi siku zote hujibu 'bado sija register' niki register nitakutumia lol
mmmm, mtaweza? mnavyopenda kuonekana hamshindwi kitu! kumbe mnatuma huku mnaumia moyoni? ha haaaaa. kwa raha zenu!
 
tatizo lako wewe umeelewa angle moja tu
wenzio tunazungumzia angle zote
wala kutuma sio tatizo
wapo wanaofurahia pia kutuma na kuhonga kwa njia hii
na wanao hongwa ndo wanapata matatizo
tunazungumzia kwa ujumla wake

Ujumla gani??
Unless kuna watu wanatapeliwa/ibiwa bila wao kujua sioni lawama zinatokea wapi maana kwangu hayo mengine ni ya mtu kujitakia na kuendekeza.
 
Kama ilivyo matumizi ya simu yalivyo badili mahusiano

sasa kuna hili la matumizi ya kutumiana pesa kwa njia ya simu

m-pesa,tigo-pesa..airtel money,z pesa na kadhalika.......

je unafikiri mahusiano yame athirika kwa kiasi gani sasa?????

nini kimeongezeka zaidi?faida? au hasara??????

kwa uzoefu wangu wanaume wengi 'wanaona hii teknolojia' imewasaidia wanawake

zaidi since wanaume ndo 'main provider' kwa sehemu kubwa ya jamii....

imekuwa rahisi 'kuchunwa' kwa kupigiwa tu simu na kutakiwa utume pesa....

na wengine wanaona now ni rahisi hata 'kumzidi mtu' maarifa kwa njia hii

na wengine wanaona 'utapeli' wa mapenzi na 'wizi' umerahisishwa......

je wewe waonaje ?

uzoefu wako ukoje kwa hili????????

You have said it all, Mkuu!!!

No more from me!!!!!
 
Ujumla gani??
Unless kuna watu wanatapeliwa/ibiwa bila wao kujua sioni lawama zinatokea wapi maana kwangu hayo mengine ni ya mtu kujitakia na kuendekeza.

watu wakisema mitandao ya jamii imeongeza watu ku cheat
hawalalamiki na kulaumu mitandao ya jamii
wanazungumza mabadiliko ya jamii yalioletwa na mitandao ya jamii
now umenielewa?
 
Back
Top Bottom