Watu
JF-Expert Member
- May 12, 2008
- 3,231
- 1,470
Mojawapoa ya quality za mwanamapinduzi halisi, ni utashi wa kutovumilia mmoja wa wale wanaofikiriwa kama wana Mapinduzi anapoonewa ama Kunyanyaswa.
Binafsi, nimesikitishwa sana na Mpigania haki Bwana Mwigamba kukamatwa na Mapolisi kwa Makala yake. Uko wapi Uhuru wa Kutoa Maoni unaohubiriwa katika Katiba.
Kiukweli Polisi wamedhihirisha uwezo wao wa kutofikiri kwa kumkamata Mwigamba, na kwa Mtindo huu hata mimi najiona Rumande siku si Nyingi.
Polisi wamekuwa kama wazinzi ambao kila siku wanaenda kanisani na kuhubiria kutozini, lakini akiwa palepale kanisani anamtamani muumini mwenzake, au mwanakwaya mwenye pete ya ndoa ati kwa kuwa ana sauti nzuri..Mfano wangu ukiufikiria kwa juu juu hutauelewa lakini kimsingi nimekumbuka nilivyomuuliza ndugu yangu askari polisi aliyetumwa kuwadhibiti wafuasi wa Chadema pale Shinyanga baada ya Kura za ubunge kuchakachuliwa, nilimuulliza hivi;
'Unadhani Chadema ilishinda? Akajibu 'Ndiyo',
Nikamuuliza tena wewe ulikuwa unalinda kura pale ofisini ulishuhudia uchakachuaji? akasema 'Ndiyo' ,
Nikamuuliza tena ulitambua kuwa Haki ya Mtanzania unapindishwa? Akasema 'Ndiyo'.
Nikamuuliza ulipoamriwa kuwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wadai kuibiwa kura uliwatawanya? akajibu 'Ndiyo'
Nikamuuliza unadhani ulitumia akili yako sawasawa? akakosa Jibu
Hilo ndilo analoongelea Mwigamba. Mojawapo ya watu wanaochelewesha Mapinduzi ya kidiplomasia katika Nchi zetu za Afrika ni Maaskari polisi!
Nikakumbuka pia nilivyohadithiwa na Rafiki yangu mmoja kule Tarime miaka fulani ya nyuma sana wakati Maaskari wanatafuta siraha, walikuwa wanawalazimisha wanaume kuwalala mama zao kama option ya kutaja Silaha ziko wapi..........'Uvunjifu Mkubwa wa Haki za Kibinadamu!
Okay Tuache porojo sasa
Suala la Msingi hapa ni kuwa je tuko tayari uona wana harakati wanakamatwa na kushitakiwa wakati tukiwa Kimya? Maana kama wewe ni mwanaharakati kweli ujue ni zamu yako......
Na kwa kuwa tunafumba macho na Kusikitika Kimoyomoyo kwa Mwigamba..basi Sheria ya katiba ikianza kutumika, sisi tunaojiita wanaharakati tutaozea jela .....na watu watasikitika kimoyomoyo tu na Maisha yao yataendelea
Hapo ndipo unapoona Akili zetu zilivyolala
Akili za Kusherekea Uhuru ambao watu wanaishi Maisha ya kiutumwa nchini mwao
Kuna Utumwa mkubwa zaidi ya umasikini?
Yaani nina Uchungu kwelikweli............................
Tuanzie kwako! Dhamana ilikuwa wazi, ww hukuwepo mahakamani? Huna hiyo mali ya mil 5 isiyohamishika?
Haya viongozi wa chadema wote hakukuwa hata na mmoja alikuwa tayari kuona huyo bwana halali selo?
Anza ww kuonyesha mfano wakumsaidia nasi tutakuja