M/kiti wa CHADEMA mkoa wa Arusha akamatwa na kuswekwa rumande - kisa makala ya uchochezi

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Mwandishi wa habari/makala na m/kiti wa Chadema mkoa wa Arusha, Samson mwigamba, amekamatwa na polisi kwa madai ya kuandika makala ya uchochezi ktk gazeti la Tanzania daima la jumatano wiki iliypita, Tanzania daima la leo limeripoti.

Jana ilipripotiwa na gazeti hilohilo, kuwa Samson Mwigamba, mmoja wa waandishi ambao ninapenda sana makala yake alihojiwa (jumanne) kwa saa tatu na baadaye akaachiwa. Lakini muda mfupi kabla gazeti halijaenda kuchapishwa( jumatano jioni) likapata habari kuwa mwigamba amekamatwa tena na kuwekwa mahabusu. Nanukuu gazeti gazeti hilo;

Ktk hatua nyingine m/kiti wa Chama hicho hicho mkoa wa Arusha Samson Mwigamba jana alikamatwa tena na jeshi la polisi kanda maalum ya Dsm, na atafikishwa ktk mahakama ya kisutu leo kwa tuhuma za uchochezi.

Mwigamba ambaye alidaiwa kuitwa na kuhojiwa na mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini, (DCI) Robert Manumba, alihojiwa juzi kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa.

Hata hivyo, habari zilizopatikana wakati tunakwenda mitamboni, m/kiti huyo alikamatwa tena na kuwekwa mahabusu kwa tuhuma za kuandika makala ndani ya gazeti hili, toleo la jumatano wiki iliyopita.

Mwigamba aliandika nini ktk gazeti la Tz daima jumatano wiki iliyopita?

Makala hiyo ni ndefu kidogo, lakini hata baada ya kusoma zaidi ya mara mmoja, sioni uchochezi unaosemwa na polisi. Bahati mbaya sina gazeti hapa lakini ninaweza kutoa muhtasari kwa faida ya wasomaji. Mwigamba aliipa kichwa makala yake; Waraka maalum kwa polisi wote nchini.

Ktk makala hiyo, mwigamba anasisitiza kwamba jeshi la polisi lisitumike kama robot. Yaani wasikubali kufanya kila kitu wanachoombiwa kwa kuwa tu kimesemwa na mabosi. Nao wafikirie na kuona kama kitu alichoagizwa ni haki au uonevu. Akaendelea kueleza kuwa, kama amri ya mabosi wao ni ya kwenda kuwapiga watu ambao wanatafuta haki zao na ambao ni shangazi zao, dada, kaka, wazazi, wajomba zao au watanzania wenzao - wasikubali. Hakusema wasifuate maagizo ya mabosi wao, ambayo ni ya haki.

Mwigamba akaelezea kuwa, chanzo cha kutii kila kitu bila kuhoji lina mizizi yake ktk aina ya mafunzo wanayopewa jeshi hilo ktk vyuo vyao.


Mwigamba akaeleza historia yake fupi, jinsi alivyojiunga na mafunzo ya jeshi hilo na kuacha ndani ya muda mfupi sana, ( nadhani mwezi mmoja?) kutokana na mateso ya yasiyo na sababu na uonevu. Falsafa kubwa inayojengwa ktk mafunzo ya jeshi la polisi lililomshinda, ni kutii amri au kuitekeleza bila kuhoji mantiki yake. Alitoa mifano mingi nami nitatoa mfano mmoja kati ya mifano yake.

Afande ( bosi ) akisema; wewe ni mjinga kama mama yako; kuruta( mwanafuzi) anapaswa kujibu; Ndiyo afande.


Jambo jingine lililomsumbua ni kutoruhusiwa kwenda kusali siku ya jumamosi - akahisi kuwa imani yake imeingiliwa.


Mwigamba ktk makala anataja majina ya marafiki zake wawili aliosoma nao sekondari ( Edwin na x nimemsahau), ambao leo ni wakubwa ktk jeshi hilo la polisi ( mmojawapo yuko wilaya Igunga) na kusisitiza marafiki zake hao watende haki kwa watanzania wote kwa kuwa sisi sote ni ndugu na jamaa. Awakumbushia ugumu wa maisha walioyapitia wakati wa masomo yeye na rafiki zake hao wawili.


Lakini muhimu ktk makala hiyo ni jambo lile lile kuwa, hao marafiki zake pamoja polisi wote nchini wasikubali kutii kila kinachoamriwa ambaocho si haki, hata kama kimetolewa na mabasi wao. Anasisitiza, lazima wahoji mantiki na uhalali wake kisheria. Hawaambii waasi jeshi au wasitii sheria halali za Tanzania. Anataka wafuate sheria halali tu, lakini siyo matakwa binafsi au ya kisiasa ya mabosi wao.

MAKALA YA MWIGAMBA:

Waraka maalumu kwa askari wote

MAKALA hii ilikuwa itoke Jumatano ya wiki iliyopita lakini kwa sababu za kiufundi ikashindikana. Imekuwa ni bahati nzuri kwamba inapotoka leo, ijibu swali la askari polisi dereva wa gari la maji ya kuwasha.

Askari huyo alimweleza Mwalimu Mkuu wa watu jinsi roho inavyomuuma pale anapowamwagia Watanzania wenzake maji hayo ya kuwasha wakati wakidai haki yao. Askari uliyeuliza na wenzako wote someni makala hii kwa utulivu. Huu ni waraka maalumu kwa askari wote wa majeshi yote vikosi vyote Tanzania Bara na Visiwani.

Kwa lugha ya wazi zaidi nazungumza na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania, Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa, askari wa Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM), askari wa Jeshi la Magereza na wale wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).

Kuwa mwanajeshi lolote kati ya hayo niliyoyataja si dhambi na si kweli kwamba kuwa mwanajeshi kunakuondolea uwezo wa kufikiri na badala yake ukawa unafikiriwa na watu wengine.

Wala haimaanishi kuwa askari kuwa kama robot ndio nidhamu bora kuliko zote duniani. La hasha! Mimi nilikataa utumwa huo!

Mwaka 1999 nilihitimu elimu ya cheti cha ufundi mchundo, yaani Full Technician Certificate (FTC) katika uhandisi wa Elektroniki na Mawasiliano ya Anga, yaani Electronics & Telecommunications Engineering kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).

Nikiwa bado sijapata kazi ya maana, mwezi Aprili mwaka 2000 niliona tangazo la kazi ya Radio Technician katika Jeshi la Magereza. Nikatuma maombi na kuitwa kwenye usaili uliofanyika Chuo cha Maofisa wa Jeshi la Magereza Ukonga, Dar es Salaam mwezi Juni 2000.

Wote tuliofaulu usaili tulipangiwa siku ya kuripoti Chuo cha Magereza Kiwira kule Tukuyu, Mbeya.

Kufika kule nilishuhudia mambo ya ajabu. Ingawa wao hufurahia na kusema eti wanakutoa uraiani na kuwa mwanajeshi lakini baadhi ya matendo yanayofanyika wakati wa mafunzo ya jeshi ni ya kuwapumbaza askari wetu ili baadaye wakiwa kazini, watawala wawatumie watakavyo.

Nilishindwa kuvumilia kaulimbiu ya wakufunzi wa jeshi pale walipoelekeza kwamba chochote kruta (askari mpya mafunzoni) unachoambiwa lazima uitikie "ndiyo afande". Nilishindwa kuitikia kwa mfano pale mkufunzi mmoja mwenye cheo cha koplo alipotutamkia mfululizo wa sentensi zifuatazo:

Mkufunzi: Nyinyi makruta mbona wote hamkuja na majembe?

Makruta: Ndiyo afande!

Mkufunzi: Hamkuambiwa makao makuu ya jeshi kwamba lazima mje na majembe?

Makruta: Ndiyo afande!


Mkufunzi: Kwa hiyo kwa kuwa hamkuambiwa na nyinyi hamkuyabeba?


Makruta: Ndiyo afande!

Mkufunzi: Wote ni wapumbavu pamoja na mama zenu waliowazaa.

Makruta: Ndiyo afande!

Ni hayo pamoja na mambo mengine ya kulazimishwa kwenda kwenye kile kinachoitwa disko, ambapo pamoja na uchovu wa kutwa nzima wa kazi ngumu na nyingi bado ni lazima ukae hapo mpaka saa 4 usiku tena ukinyooshewa kidole tu na mwenzako lazima usimame na kuimbisha wimbo tena kwa tabasamu, wimbo mmoja wapo ukisema "Magereza ninavyokupenda nitakunywa sumu juu yako", ndiyo yaliyonifanya nikakataa kazi ya jeshi baada ya wiki moja tu ya mafunzo.

Siku niliyokataa jeshi ilikuwa ni Jumatano asubuhi ambapo sikwenda mchakamchaka na wakati wenzako wanatawanyika kufanya usafi wa nje maeneo mbalimbali, mimi nilibeba begi langu na kuanza kuondoka chuoni majira ya saa moja na nusu hivi asubuhi.

Nilikamatwa na mkufunzi mmoja wa jeshi na kupelekwa pamoja na begi langu kwa Ofisa Mafunzo wa chuo. Aliponiuliza sababu nilimtajia mbili, kwanza kwamba sifurahii mambo ya jeshi na kubwa zaidi kwamba mimi ni Msabato na nimeambiwa na wenzangu kwamba hapa hakuna kwenda kusali, siku zote za juma ni kazi.

Kitu ambacho sitaweza maana Sabato takatifu lazima nipumzike! Bila kuuliza zaidi aliconclude kwa kuniambia kwamba, "Sijawahi kuona mtu anaacha kazi kwa ajili ya mambo ya dini.

"Ni dhahiri wewe ulikuja kutupeleleza na hivyo kazi yako imeisha sasa unataka kurudi. Tutakuweka rumande, tena ile ya polisi kwa wiki mbili wakati tunafanya upelelezi juu yako."

Askari aliyenileta alianza kunivuta ili kunipeleka rumande lakini nilikataa huku nikiendelea kujieleza kwa ofisa mafunzo ili ajue kwamba sikuwa na mpango huo aliousema.

Baada ya kuelemewa na hoja zangu alinipeleka kwa makamu mkuu wa chuo ambaye yeye alitumia zaidi Biblia kunihubiri kwamba nakaidi amri ya mamlaka wakati hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu.

Jibu langu lilikuwa fupi na lenye msimamo mzito kwamba ikiwa mamlaka ya wanadamu inafika mahali inanena tofauti na Mungu, Mtume Petro ametuandikia kwamba katika hali ya namna hiyo, "Imetupasa kumtii Mungu kuliko mwanadamu".

Na yeye alinishindwa akanipeleka kwa mkuu wa chuo na wao wote wakiwapo. Ushauri waliokuwa wakimpa mkuu wa chuo ni kwamba mimi niwekwe rumande kwanza ili wafanye upelelezi. Lakini sikuyumba katika msimamo wangu.

Nilimweleza mkuu wa chuo kwamba mimi ni raia na si mpelelezi. Nilizirudia rudia sababu zangu za kuacha jeshi tena kwa ujasiri mkubwa na kumhakikishia mkuu wa chuo kwamba akinipa hayo ninayoyataka niko tayari kubaki jeshini.

Hatimaye kauli ya mwisho ya mkuu wa chuo ilikuwa ni hii: "Jeshi ni wito. Tunaweza kumlazimisha huyu kijana kuwa mwanajeshi lakini baadaye ikatuletea madhara makubwa sana." Akamalizia kwa kusema, "chukueni maelezo yake kwa maandishi kisha arudishe vifaa vya jeshi."

Wakati naondoka nilimsikia ofisa mafunzo akitoa maelekezo kwa walio chini yake kwamba mwanafunzi mwingine wa jeshi akija kuripoti na kwenye daftari akajaza kwamba ni Msabato, msimsajili kwanza mpaka aje kwangu! Sijui kama Wasabato wameendelea kupokewa kwenye hicho chuo cha magereza lakini ninachotaka askari wote wa majeshi yetu yote na vikosi vyote, ni kwamba askari unaweza kusimama kwa miguu yako na kufikiri kwa akili yako mwenyewe!

Ndugu zangu askari, nchi imefika mahali ambapo Waingereza hupenda kupaita ‘critical point'. Ni mahali ambapo wananchi wako tayari kwa mabadiliko na watawala wako tayari kwa mapambano ili kubaki madarakani.

Katika point hii askari wetu wanakuwa na nafasi kubwa ya aidha kuwezesha mabadiliko hayo kutokea kwa wakati wanaoutaka wananchi, tena kwa amani ama kuyachelewesha (si kuyazuia) na kusababisha yatokee baadaye kidogo kuliko wananchi walivyotaka, tena baada ya kumwaga damu nyingi ya Watanzania wasio na hatia!

Napenda kurudia kwamba hakuna jeshi lolote duniani hata kama tungekusanya majeshi yote ya dunia hii na kuyaleta Tanzania hawataweza kuizuia nguvu ya umma pale inapokuwa imeamua kufanya mabadiliko.

Napenda tena kurudia kwamba si lazima askari mfanye kile ambacho wakubwa wenu wanataka na kuwaamuru kufanya. Tunaweza kusimama imara na kutetea haki za Watanzania tukiwamo na sisi askari. Niliwahi kugoma kutii amri ya kukamatwa na kuwekwa rumande.

Lakini pia mifano ni mingi na nisingependa kuchukua mifano kutoka nchi za Ulaya kama Uingereza ambako tulishuhudia wananchi wakiandamana mitaani na askari wao hawakuwahi hata kumpiga kofi tu mwandamanaji hata mmoja.

Walipohojiwa na vyombo vya habari walisema dhahiri kwamba waandamanaji ni raia halali wenye haki ya kufanya kile wanachokifanya kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi yao. Katiba ya Tanzania na sheria za nchi hii zinatoa haki kama zile za Uingereza. Tofauti ni utekelezaji wa matakwa hayo ya kikatiba na kisheria. Watawala wa Uingereza wako tayari hata kung'oka madarakani ili kutekeleza matakwa ya nguvu ya umma.

Lakini wale wa Tanzania wako tayari kung'oa uhai wa raia wengi ili mradi kuzuia nguvu ya umma inayodai haki na wananya hivyo kwa sababu ya hofu ya kung'oka madarakani, jambo ambalo hawataki kabisa kulisikia. Na ndugu zangu askari napenda kuwaambia kwamba yote yanafanywa na watawala wetu kwa kuwategemea nyinyi.

Wanaminya haki zenu nyinyi wenyewe, haki za wazazi wenu, dada na ndugu zenu, marafiki zenu, jamaa zenu na majirani zenu. Chukulia mfano rafiki zangu Mtaki na Edwin. Tumesoma wote shule ya msingi pale Magu.

Nilichaguliwa kujiunga na Mazengo Sekondari, shule kubwa na ya muda mrefu ambayo sasa imegeuzwa kuwa chuo kikuu bila mabadiliko ya majengo.

Shule iliyokuwa na maabara nne kwa maana ya maabara ya baiolojia, kemia, fizikia na jiografia. Ilikuwa ni sekondari ya ufundi na hakuna karakana ambayo haikuwapo.

Shule iliyokuwa na walimu wa kutosha, vyumba vya kutosha vya madarasa na vya kulala mabwenini.

Katika bweni la Ujamaa kwa mfano, nilikokuwa naishi mimi, kuna vyumba kadhaa havikuwa na watu. Darasa la Form IVA ambalo nilikuwamo lilikuwa na wanafunzi 21 tu darasani.

Na mazingira mengine mengi ambayo sitaweza kuyataja hapa ambayo yanafanya wanafunzi wa leo wa Chuo Kikuu cha Mt. John wajiulize kama kweli ile ilikuwa ni shule ambayo haina maktaba wala vitabu vya kutosha, na mengineyo mengi mnayoyafahmu.

Nikafaulu kwa kiwango cha daraja la juu lililoniwezesha kuendelea mpaka chuo kikuu na kupata kazi nzuri kwenye Umoja wa Mataifa.

Rafiki zangu nakumbuka mlivyoamua kujiunga na Jeshi la Polisi si kwa sababu mlipenda kazi hiyo ama kwamba mlikuwa na wito wa kuwa polisi kama mnavyodanganywa kwamba jeshi ni wito.

Nakumbuka mlijiunga huku mkilalamika kwamba mnalazimika kujiunga huko kwa sababu kiwango chenu cha ufaulu hakiwapi fursa ya kazi bora zaidi ya hiyo. Lakini mimi nawafahamu vizuri. Najua uwezo wenu wa darasani. Mliathiriwa na mazingira ya hovyo ya shule mlizosoma.

Rafiki zangu nyinyi wote leo ni wakuu wa vituo vikuu vya polisi vya wilaya katika wilaya za Mbozi na Igunga.

Leo hii mimi nimeacha kazi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kushiriki vema katika mapambano ya kutafuta ukombozi wa taifa hili.

Wadogo zenu na wadogo zangu mnawajua wako katika juhudi za kutafuta maisha lakini ni magumu. Wengine walikosa kabisa nafasi ya kujiunga hata na hiyo Magu Day.

Wakaishia Bulima na Kinango, ambako hali ilikuwa mbaya zaidi. Wakafeli kabisa na leo wanahangaika hapa na pale lakini watawala wanawawekea mazingira magumu mno ya kuendesha maisha.

Na sasa chukulia nao wametambua hali yao duni inasababishwa na watawala walafi na walaghai. Wamejaribu kutumia njia za kidiplomasia kudai haki zao wanakutana na watu wanaitwa wakuu wa wilaya na mikoa.

Wanaamua kuandamana, mnashiriki kuamrisha askari walio chini yenu kuwapiga na kuwaweka rumande na hatimaye kuwafungulia kesi za kubumba!

Askari wetu igeni mfano wa askari wa Misri! Pale wananchi walipoamua kuandamana kukomesha utawala wa kidhalimu wa miaka 30 chini ya Hosni Mubarak, askari waliwalinda badala ya kuwapiga.

Walikataa kwa sababu hata wao walikuwa wakiumizwa na Mubarak lakini zaidi ya hayo, waliokuwa wakiandamana walikuwa ni dada zao na ndugu zao na marafiki zao.

Hivi sasa nchi iko njia panda. Ugumu wa maisha umeongezeka mara nne na zaidi. Watawala hawalioni hilo wala hawajishughulishi kurekebisha hali ya mambo hususan hali ya uchumi.

Wako busy na kujiandaa kwa uchaguzi wa 2015. Mawaziri wako busy na kampeni za kuteuliwa kuwa wagombea wa urais kupitia chama tawala hapo 2015 na rais naye yuko busy kuandaa mtu wake ambaye anadhani akimrithisha jumba jeupe la pale Magogoni atasema mwacheni Ndugu Kikwete apumzike kwa amani.

Taifa limeamua kuandika katiba mpya, rais na serikali yake na chama chake wameamua kuuteka mchakato ingawa haikuwemo kwenye ilani yao ya uchaguzi ili tu waturudishie katiba ya mwaka 1977 na kuipa jina juu ya jalada KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2014.

Natambua juhudi zinazoendelea hasa zikiongozwa na CHADEMA kujaribu kumkumbusha rais kwamba katiba iko juu yake na katiba ni mali ya wananchi na yeye anaajiriwa kwa katiba hiyo na si yeye kujiandalia katiba ili atawale kwa ulaini.

Lakini juhudi za kidiplomasia zikishindikana hapo ndipo itabidi haki ya watu idaiwe kwa maandamano na hapo askari wote tuungane na kuwa kama Misri, kwa kuwa Katiba mpya ni kwa masilahi yenu pia! Jaribuni kutafakari!


My take;
Hivi huu si mwanzo wa wa udikteta? Uhuru wa mawazo unaolindwa na katiba uko wapi? Leo ni Samson Mwigamba kesho ni nani? Mimi niliyeandika makala ile kwa ufipi JF au ni mtandao wote wa JF?

Pili, Hivi ni haki serikali ya kutumia sheria ya uchochezi iliyotungwa enzi za ukoloni ambayo wameikopi na kuipaste na kwa faida ya nani? Tunaadimisha miaka hamsini ya uhuru gani kwa staili hii
?
 
Ina maana polisi wa Tanzania hawana akili wala utashi wa kuamua nini cha kufanya na kipi waache? Kama sio kudhalilisha polisi wa wa kawaida ni nini? Polisi wa Tanzania wanapata orders toka kwa huyu bwana aliyeandika makala? Wale walioua Nyamongo, Arusha nao walipata orders toka kwa huyu mwandishi?

Jambo moja lililo wazi ni hili: Viongozi wa Tanzania including wakubwa wa polisi wanaamini watanzania ni ma-mbumbumbu, hawajui mbele wala nyuma na hivyo mtu akipaza sauti ya kufunua maovi wanayofanya hawa wakubwa haraka haraka wanasema 'anachochea'.
Kuendelea kumshikilia huyu mwandishi kwangu ni sawa na kama polisi wanatutukana sisi watanzania.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
basi bodi nzima ya uhuru publication na al nur wangekuwa jela kabisa

Mkuu Inko. hapa uchochezi unakuja ikiwa maslahi ya magamba yanaguswa lakini kama uchochezi huo ni kwa faida ya magamba inakuwa sio uchochezi hata kidogo!
 
Duuuu kazi kwelikweli yaani serikali ye2 nizaidi ya malaika haitakiwi ikosolewe kbs.

aangalie wasije wakamjeri muro..

Naona taratibu wanaanza ku2rudisha enzi zile za ukoloni.Wanataka 2waogope polisi kama ......2kiwaona 2ni mbio.
 
Aliyesimama katika haki siku zote ataonekana mshindi. Mwigamba atashinda hizi hila za wakoloni weusi kama ambavyo Jeri Mro ameshinda! Hata kama watataka kutunyamazisha watanzania wote kwa kuwa wao wanadola inayowalinda hakika mawe na vilima vyote vitaongea badala yetu! It is a matter of time!
 
Nafurahi sana navyoona kila kukicha waendesha mashtka wa serikali ndio wanaongoza kwa kushindwa kesi coz kesi nyingi ni za kubambikiana na zingine zinafunguliwa na makonstebo vilaza wasiojua lolote kuhusiana na sheria.
Mwisho wa kesi hii jeshi la polisi litaumbuka kama Kova alivyoumbuka kwenye kesi waliyombambikia Jerry Muro.
 
Afande; Wewe ni mjinga kama mama yako.

Askari; Ndio Afande,

Duu! hii nimeipenda. Kama mafunzo yanaandaliwa hivyo unategemea kupata askari anayetumia akili yake kweli?
 
Ina maana polisi wa Tanzania hawana akili wala utashi wa kuamua nini cha kufanya na kipi waache? Kama sio kudhalilisha polisi wa wa kawaida ni nini? Polisi wa Tanzania wanapata orders toka kwa huyu bwana aliyeandika makala? Wale walioua Nyamongo, Arusha nao walipata orders toka kwa huyu mwandishi?

Jambo moja lililo wazi ni hili: Viongozi wa Tanzania including wakubwa wa polisi wanaamini watanzania ni ma-mbumbumbu, hawajui mbele wala nyuma na hivyo mtu akipaza sauti ya kufunua maovi wanayofanya hawa wakubwa haraka haraka wanasema 'anachochea'.
Kuendelea kumshikilia huyu mwandishi kwangu ni sawa na kama polisi wanatutukana sisi watanzania.

Hapo ndipo activist watanzania wananiacha hoi mambo kama haya hawa hamasishi watu ku-demonstrate aah; na hili ndilo linalo endeleza kiburi cha watawala. Ilitakiwa on the spot kesho yake watu wako mtaani wakimtetea huyo mwandishi/mwenyekiti whoever kabla ya chama cha siasa kuanza kuhamasisha watu.
 
Makamuzi,
sisi tulio na ID za kweli lazima tuwe tayari kwa lolote kwa mwenda huu ikiwa ni pamoja na kubambikiwa kesi za kughushi kama mwigamba.


Hii (Intimidation) ndiyo silaha kubwa CCM wanayotumia kutawala nchi hii bila hivyo wasingekuwa madarakani leo hii...watu wananyamaza kwasababu ya kuogopa ku-fall victim huku kukiwa hakuna wakukutetea maana wanajua hata huko kwenye activists wamejaza vibaraka wao wanao walambisha utamu wa asali ili kupunguza makali ya maisha. Wakati mwingine ni wale waliokosa ajira so kwavile imewalazimu kuwapo hapo kama sehemu ya ku-earn living na siyo kama sehemu ya kutetea minorities. Simaanishi wote lakini walio wengi!
 
Askari wakiwa mafunzoni wanaonewa sana na kupewa adhabu za kikatili kwa kujidanganya wanafunzwa ukakamavu kumbe mafunzo hayo yanawaathiri kisaikolojia na kugeuka kuwa mafunzo na maandalizi ya kuwatendea raia vitendo vya kikatili.
 
Watawala wameacha kazi zao za kiofisi wanahaha kujua nani kasema nini na nani ni mfuasi wa nani! huwezi nyamazisha watu wote sababu ya madaraka yako na huwezi pendwa na wote hata uwe nani? waliomchukia masiha hamkuwasoma hamkumbuki Herode na Pilato walipatana kwenye bifu lao baada ya kumuhukumu Yesu na hii ni baada ya kujua wote walikuwa wanamchukia?
Polisi isiyojitambua ni janga kwa raia wenye udhubutu.
 
Back
Top Bottom