M aandamano makubwa yaandaliwa kumpokea mbunge cecilia palesso wa chadema

mwakajilae

Member
Mar 11, 2011
58
46
Mbunge mpambanaji Cecilia Pareso aliye apishwa hivi karibuni katika bunge lililopita huko Dodoma,leo ameandaliwa mapokezi makubwa wilayani Karatu,yanayoratibiwa na Baraza la Vijana la Chadema Karatu ikiwa ni hitimisho la kiapo chake cha mwisho kwa wananchi, katika safari ya kuwatumikia na kuwawakilisha.Maandamano hayo makubwa yanaambatana na msururu mkubwa wa piki piki takribani miamoja kuanzia Mto wa Mbu kuelekea Karatu kijijini aliko zaliwa.Msafara wake umeambatana na uongozi mzima wa Chama mkoa wa Arusha.Kutafanyika mkutano mkubwa wa hadhara kijijijini hapo.

Matarajio ya wakazi wa Karatu ni makubwa kutokana na ujasiri,msimamo na uzalendo ambao mara nyingi alikuwa anausimamia akiwa diwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Nifaraja ndani ya Chama cha Chadema kumpata mbunge machachari anaye kwenda kuungana na Mh Halima Mdee na wengine wengi katika wabunge wa kike wanaowasha taa ya mapambano ya kuonesha uongozi pasipo kujali jinsia yao iliyokolezwa na tamaduni za mfumo dume.
Kitaaluma Mh Cecilia Paresso ni Mwanasheria mwenye Shahada ya Kwanza.
Tutegemee makubwa kutoka kwa mwanaharakati huyu hivi karibuni.
 
Ngoja niwahi kumchumbia, namfahamu sana, tulipotezana kitambo....
 
bosi wenu zitto amesema hakuna muda wa maandamano wala kupongezana ni kuingia kazini moja moja... huyo mbunge anachojipongeza ni nini wakati kuna watu jimboni mwake mpaka leo hii hawana umeme wala maji...chadema sometimes wana double standards sana:thinking:
 
Natamani wangetumia muda huo kufanya shughuli za kujiletea maendeleo

Gamba hajifichi utamuona kwenye post zake kama wewe.inamana mpaka leo wenzako hawajakupa hata sehemu ya kutuibia pole.sijui unataka walete maendeleo yapi sikuhiyo toa mfano
 
Back
Top Bottom