Lwakatare ajipanga

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,163
Wilfred Lwakatare ameandika barua akiomba kujiuzulu nafasi za uongozi zake zote alizokuwa nazo ndani ya CUF. Lengo lake ni kujikita jimboni kuelekea uchaguzi mkuu
 
Wilfred Lwakatare ameandika barua akiomba kujiuzulu nafasi za uongozi zake zote alizokuwa nazo ndani ya CUF. Lengo lake ni kujikita jimboni kuelekea uchaguzi mkuu

Duu, hili ni bonge la pigo kwa wana CUF!
ila nimtakie heri ktk maandalizi ya kuichukua nafasi yake ya ubunge aliyo taperiwa 2005.
 
Nadhani ni haki yake kujiuzulu,na sidhani kama ni pigo kwa chama chake! Katika kila chama kila mtu ni muhimu,alikuwepo mwalimu nyerere na sote tulidhani ni muhimu sana katika nchi yetu,mwalimu alifariki na nchi ikiwa katika ufisadi mkubwa na hali hiyo in aendelea hadi leo.Nadhani cuf wanaweza peke yao bila lwakatare,bila lipumba na hata bila maalim wanaweza kwenda mbele kwani wana structure nzuri kuliko vyama vote vya upinzani.
 
ni kweli kwamba amejiuzulu ili kujipanga na uchaguzi tu?
kwamba akiwa kiongozi wa kitaifa hawezi kujiandaa kushinda uchaguzi tena katika jimbo ambalo amewahi kuwa mbunge wake,na ambalo amelitembela hivi karibuni na kupata mapokezi makubwa[angalau dalili ya kukubalika],
hivi hakuna sababu nyingine kweli ya uamuzi wake huu
 
katika suala la kujiuzulu ili ajiandae na uchaguzi hilo ni jambo zuri kwa kuwa itampa nafasi ya kuwa na wapiga kura wake kwa muda mrefu, saaafi sana na wengine waige kutoka kwake
 
Lwakatare ni vigumu sana kushida Ubunge kupitia CUF bila kuwepo ushirikiano wa vyama vya siasa.Ushauri wangu kwake ni kwamba kama anataka Ubunge ahamie Chadema au CCM.
 
chadema ndio walioua upinzani historia hataacha kuinyooshea kidole hawa maana ni waroho wa madaraka na wasiojua siasa ni maoportunist tu

washindwe na wa legee kwa nguvu za jf
 
chadema ndio walioua upinzani historia hataacha kuinyooshea kidole hawa maana ni waroho wa madaraka na wasiojua siasa ni maoportunist tu
washindwe na wa legee kwa nguvu za jf

Kulikoni ? Ama ulitaka kusema washindwe na walegee kwa nguvu za Mtu wa Pwani - hiyo ingeeleweka. Ninavyoelewa ni kwamba katika upinzani ni ndani ya Chadema tu mambo makuu matatu yamewezekana.
1. Kubadilika kwa uongozi wa juu.
2. Kupatikana kwa mafanikio endelevu - positive growth.
3. Kuelimisha na kuhamasisha wananchi (mfano operation "sangara")
Kama kwa vigezo hivi kuna vyama vinaathirika, hilo mbona jambo zuri tu - afadhali vife kabisa vibakie viwili au vitatu.
Vyama uchwara ni miradi ya Chuo Cha Mafisadi.
 
mtu wa pwami labda utuambie wameua kwa namna gani. hapo labda tutakuelewa.
 
Nkisikia habari za mwanamaguzi anahama upinzani na kujiunga na chama tawala napata kama kichefuchefu hivi.
 
Nkisikia habari za mwanamaguzi anahama upinzani na kujiunga na chama tawala napata kama kichefuchefu hivi.

Usicheze na njaa maana hiyo inawakimbiza mkuu. Na wakifika huko utawasikia wanavyojikanyaga.
Ukimsikia huyu Tambwe, Amani Kaburu na yule mzanzibari katibu wa chama majizi aliyeko Kigoma wakizungumza, unaweza kujiuliza kama wana akili timamu.
 
Nadhani ni haki yake kujiuzulu,na sidhani kama ni pigo kwa chama chake! Katika kila chama kila mtu ni muhimu,alikuwepo mwalimu nyerere na sote tulidhani ni muhimu sana katika nchi yetu,mwalimu alifariki na nchi ikiwa katika ufisadi mkubwa na hali hiyo in aendelea hadi leo.Nadhani cuf wanaweza peke yao bila lwakatare,bila lipumba na hata bila maalim wanaweza kwenda mbele kwani wana structure nzuri kuliko vyama vote vya upinzani.
Waachine madaraka ya ngazi za juu kama CHADEMA na CCM.
 
Back
Top Bottom