MTK
JF-Expert Member
- Apr 19, 2012
- 8,928
- 6,849
Nampa pole za dhati Ndugu Godbless Lema. Nilikuwa pale Viwanja vya Jangwani Dar es salaam siku ya Uzinduzi wa Vuguvugu la Mabadiriko (Movement For Change). Maelfu na maelfu ya vijana walionyesha mapenzi makubwa na huruma nyingi kwake.
Walionyesha kukubaliana na dhana iliyonyuma ya Waraka wa Lema kuwa Mh Lema alidhulumiwa kwa kunyang'anywa Ubunge. Ushauri wangu kwake Mh Lema ni kuwa aandike Waraka wa Pili wa Lema na katika waraka huu wa pili aeleze kwa kirefu na kwa uwazi juu ya mkutano wake na Rais anaosema ulifanyika Osterbay 2010: nani aliomba uwepo mkutano, ulifanyika wapi, na yepi yaliyozungumzwa.
Namuomba aweke wazi mazungumzo yao na mazingira ya kufanyika kwake. Katika mahakama hii ya nguvu ya umma ni vizuri umma ujue kwa kina kwa nini Mh Lema anadhani anaweza akadhurika ikiwa mkuu amekasirishwa na yeye Lema kutotekeleza waliyokubaliana Osterbay 2010.
Ndugu yangu Nico Eatlawe nakuomba uusome Waraka wa Lema kama unavyosoma Waraka wa Mitume wa Yesu, "between the lines," na pole vile ukuwepo pale Jangwani Dar es Salaam maana vijana kwa maelfu na maelfu wamemkubali Mh. Lema na Waraka wake ni njia nzuri ya kujiami dhidi ya madhara yanayoweza kumpata kutokana na kukubalika huko.
Kukubalika kwa Mh. Lema Arusha Mjini sasa kumesambaa nchi nzima baada ya kunyanganywa Ubunge na ili si jambo dogo. Kumbuka Mh Zitto Kabwe umaarufu wake uliubuka kutokana na kusimamishwa Ubunge tu kwa muda lakini Mh. Lema amepigwa na kudhalilishwa na polisi , amewekwa rumande na Mh. Livingstone Lusinde alikejeli kuwekwa kwake rumande.
Na mwisho wa siku akanyanyanganywa Ubunge mara tu baada ya kuonyesha anapendwa pia hata Arumeru Mashariki. Huyu wako wapambe wa wakubwa wa nchi bila shaka wanaweza wakajituma kumwenyesha hata sumu. Tusipuze uwezekano huu. Tumpe moyo Mh Lema.
Kumbuka mambao mbali mbali yaliyowahi kuwasibu msusuru wa watu mbali mbali toka Gavana Balali, Harrison Makyembe, Rostam Aziz hadi Edward Lowasa...Mh. Lema anapendwa sana na vijana wa kijiweni na wanamwamini...Tumpe Mh Lema moyo aendelee kuwaelimisha hawa vijana wa kijiweni...
Tusimzidishie uchungu wake wa haki kwa kudhulumiwa na uonevu wote ambao amepata hadi sasa kwa kumuhukumu hata kabla hajatusimulia kisa kizima tangu Osterbay Oktoba 2010 hadi Arusha tarehe 5 Januari 2011 hadi juzi kuvuliwa ubunge katika mazingira ya kisheria tatanishi.
Mungu si Athumnai bwana, ipo siku ukweli utashinda uzandiki!!! Ishara kuu yenye kuashiria nyota njema ni kukubalika kwa Mh. Lema kwa maelfu na maelfu ya vijana wa nchi hii.
Mwl. Lwaitama
Mimi naamini kwa dhati kabisa kabisa kwamba sasa kiama kinainyemelea nji hii kwa sababu kufuatia waraka wa GJL kwa JK na hayo aliyoyaainisha katika waraka huo umesababisha taharuki miongoni mwa wanachama wa CDM hususani vijana ambao wameonyesha kukunwa kwa kiasi kikubwa na misimamo ya GJL; kwa hiyo basi endapo lolote baya litamtokea Lema hata la kawaida tu la kimungu mungu; itakuwa vigumu sana kwa vijana wengi kukubali au kuamini kwamba GJL amedhurika kawaida hivi hivi na kwa sababu hiyo ile njozi ya JK kwamba Arusha imerejea katika amani itapotea kabisa na moto huo kusambaa nji nzima. Wapenda amani wote tumuombe Mungu pande zote busara itumike ili amani ishamiri.
Wataalamu wansema hivi; UKITAKA AMANI PIGANIA HAKI, penye dhuluma amani haistawi hata kidogo, kama nadanganya fuatilieni yanayojiri Tahrir square Cairo ambapo licha ya Dikteta Hosni Mubarak kuhukumiwa kifungo cha maisha bado vijana wanaamini haki haikutendeka kwa hiyo Tahrir square imeanza kufurika upya kudai haki itendeke; and that is a recipe for chaos.