Lusinde amaliza mkutano wa kampeni ya udiwani Mpwapwa kiaina

Lusindeeeeeeee! Nani kama wewe Tanzania hii,tunakushukuru kwa kumkaribisha sHetani atawale mdomo wako na kutupatia ushindi
 
Tatizo ni sisi watanzania kuwapa madaraka wenda wazimu. Mwendawazimu kama lusinde tulitakiwa watanzania tayari tumeshaandamana kutaka avuliwe ubunge. Haiwezekani anapokea mshahara kwa pesa za kodi yetu halafu anatulipa matusi, mbaya zaidi mbele ya watoto. Sijui mke na watoto wake huwa wanamuelewaje, ingawa baba habadilishwi, lakini hakyanani kuwa na baba wa dizaini ya lusinde ni majuto. si ajabu mtoto wa lusinde hata kuitwa huwa anaitwa kwa matusi " we mbwa koko, lete maji ya kunywa hapa....".
 
  • Thanks
Reactions: MC
Jamani anawatoto

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Unacheza na Lusinde wewe? Huyo ni Mbunge wa CCM na member wa NEC ambacho ni chombo cha juu kabisa cha maamuzi cha CCM.Kama yeye yuko hivyo fikiria maamuzi ya chombo hicho yakoje?
 
Jamani anawatoto

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Tatizo sio watoto maana hawakuwa na uwezo wa kujichagulia baba,huyo mke hakumchunguza mume kabla ya kuolewa? Mrs Lusinde ulikubali vipi kuolewa na Livingstone? Au ndoa ya mkeka?
 
Wakuu wa JF mbona hatutaki kupiga hatua mbele?

Mdau ameleta mada nzuri tena muhimu katika harakati za mabadiliko, lakini inakosa jambo muhimu sana la kuambatanisha ''Substantial Evidences'' kama video, Sauti ama Picha tu.

Ni rahisi sana kwa Lusinde au magamba wenzake kuja humu ama mahali pengine na kukanusha kirahisi sana.

Embu fikiri kama habari hii ingekuja na Video, Audio ama picha tu, ladha na kumbukumbu ya habari hii ingekuwaje?

Mahali tulipo na tunakoelekea kisiasa matukio ya ajabu ajabu kama haya tunategemea kuyaona sana hivyo tuwe stand by kwa kutumia hata simu zetu za mchina kila mahali!!!
 
Mi sioni tofauti ya Lusinde na Lema labda ni itikadi za vyama tu.
 
Lusinde, mkuu ulieleta uzi alikuwa anamaanisha nini kusema hivyo, ama alifuatia na statement gani baada ya kutoa matusi hayo, aah kwake sio matusi "Statement hiyo"
 
Abaeban,

By the way, Ni kweli unachokiriport hapa JF, Please just say a word, Ni kweli au umeongeza 'munyu' kidogo?
 
bila support ya audio/video habari hii itakuwa haina mshiko saana
ushahidi ndio utamtumbukiza katika jangu kuu
 
Jana tarehe 9/10/2012 CHADEMA walizindua kampeni zao za kugombea udiwani kata ya Mpwapwa mjini iliyowazi baada ya kifo cha diwani DR. Maiseli miezi minne iliyopita.
Uzinduzi huo ulifanyika kwenye uwanja wa mashujaa sokoni Mpwapwa. Leo hii ilikuwa ni zamu ya chama tawala CCM ambao wao wanajinasibu kwamba kwao matusi siyo sera walifanyia uzinduzi wao papepale walipofanyia wenzao jana Kama kawaida itifaki ilizingatiwa, miongoni mwa waalikwa kwa minajiri ya kutia nguvu alikuwa ni mbunge wa mtera Mhe.l. lusinde mbunge wa CCM jimbo la Mtera (bwana matusi).
Wakiongozwa na MC ilifika zamu ya Lusinde kuzungumza, alipopewa nafasi alianza kwa kuuliza swali hadhila kwamba mwanaume anavyolalwa anaanza kuvua suluale au chupi, swali hilo ndilo lililofunga mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM hapa Mpwapwa, Wakwanza kuondoka alikuwani Mh Lubeleje ambae ni M. NEC mteule wakafuata watu wengine.Ndio maana nasema Lusinde ilimaliza kampeni za CCM kiaina.

My TAKE CCM wajifunze siyo kila mtu anafaaa kualikwa, wengine wanaharibu siku kabisa kama Lusinde yuko addict na matusi hawezi kuacha.

Bado sijaamini ulichokiandika kama mtu mwenye dhamana kwa wapiga kura anaweza kuongea kitu kama hicho hadharani. Ninachosubiri ni kupata habari zaidi toka vyombo vya habari ili nijiridhishe kutoa mchango wangu kutokana matusi kama hayo ya kudhalilisha jamii anayoiwakilisha.
 
Back
Top Bottom