LeopoldByongje
JF-Expert Member
- Apr 28, 2008
- 372
- 13
Bado sijaelewa kwa nini binadamu wengine wana roho mbaya kiasi hii,Mtu uko kwenye maumivi yeye anafanya ufisadi hata kwenye afya yako.inatia uchungu.Ni kweli tunahitaji mabadiliko
:A S-danger:Jambo ambalo nilikuwa siamini ni kukosekana kwa maadili katika sekta ya tiba. Matabibu wengi kwenye Hospitali kubwa hawana hata chembe ya utu japo walikula kiapo kutumikia wagonjwa kwa ujuzi wao wote. Sasa sina imani nao na ninaogopa Hospitali hizo maana linalofanyika huko ni uuaji mtupu lakini kwa vile wanalindwa na sheria ndiyo maana hata wanapoua hawaonekani kuwa wametoka nje ya maadili ya taaluma yao. Amin usiamini ndio madaktari wetu na iwapo mtu ataumwa nashauri awe mwangalifu sana. Pole sana Lunyungu na ugua pole. Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye yote. Nakutakia upone haraka.