NGULI
JF-Expert Member
- Mar 31, 2008
- 4,803
- 637
Kwa wafwatiliaji wa mambo ya siasa hasa kipindi hichi cha mabomu huko Mbagala kimecha vinywa wazi hasa kiongozi wa mkoa Mr. Lukuvi anavyo jieleza kwa waandishi wa habari .....aliulizwa mzee mbona madhara yanasemekana ni mengi (hasa lile bomu lilolipuka last wk saa 11 jioni) akasema ni kawaida tu wanasafisha eneo na wananchi wakiona kitu chochote cha chuma watoe taarifa, mtangazi wa TBC akambana zaidi mbona hapa tunaona watu zaidi ya 20 wamelezwa hapa wodini Temeke Hospital? na bado wengine wanaletwa huku? huoni kama madhara ni makubwa akasema wananchi wanatakiwa wazoee kama wale wa air port ya mwl .Nyerere mbona wao hawazimii na ndege zinakelele kama hayo Mabomu? Hichi ni kimeo kingine tena kwenye hii serikali ya CCM mkuu wa mkoa kwa kauli hizi sidhani kama ni sahihi, na sitashangaa kuona nyingine nyingi za ajabu ajabu na hii jamii yetu sio wafwatiliaji wa misemo au semi za viongozi wetu nyingi ni tete sana.