Lukuvi: Kuikosoa Serikali ya CCM ni Uchochezi!!!

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
8,314
3,987
Hapa tz kumekuwa na tabia ya chama kikongwe kujaribu kuwachafua vyama mbadala kwa njia mbali mbali, moja wapo ikiwa ni magazeti iwe ya serikali au binafsi, kwa kununua waandishi wa habari nk nk, jingine limekuwa ni kuweka mapandikizi kwenye vyama vya upinzani ili wafanye matendo yasio endana na ya hicho chama mbadala.

Pia vyombo vya umma iwe polisi nk nk vimekuwa vikitumika pia kutaka kuonyesha ubaya wa vyama mbadala, na pia kuwepo na vyama mbadala ambavyo ni tawi la chama kikongwe. na sasa hivi ni kutumika kwa bunge kuonyesha kwamba vyama mbadalla havi fai, kwa mfano juzi/jana kumekuwepo na hotuba ya waziri kivuli wa mambo ya ndani ambaye kaongea ukweli wa hali ya nchi yetu ilivyo, lakini katokea waziri moja na mbunge akidai hotuba hiyo ni ya uchochezi, wakati vitendo vya kuwadhulumu watu ndio uchuchezi mkubwa kuliko huo unaosemwa na mbunge Lema, au zile hotuba za kidini zinazotumika wakati na hata baada ya uchaguzi, na hata zile makala za kimaandishi, kimaneno au kipicha kuhusu mauaji ya rwanda, vita ya kongo nk nk.

ninaomba vijana kwa wakubwa wawasaidie kuwapa elimu ndugu zetu wa chama kikongwe ili kuikomboa taifa kutokana na migogoro isiyo na tija.
 
yaani mtu anakutia kidole, yeye anataka unyamaze? ukimrudishia wewe ni mgomvi....
 
Lukuvi wanajua kabisa aligushi cheti cha f4 lakini anapewa madaraka kweli ccm mawaziri ni wezi, makatibu wakuu wezi. serikali legelege hii ndiyo rangi yake kama hamjawahi kuona basi waje tz waione inavyofanana nami namuunga mkono simbachawene aliyedai bungeni jana kuwa duniani hakuna rais kama kikwete ni kweli kila mtu analifahamu hilo simbachawene umemtukana rais kwenye fasihi kuna tamathali ya semi inaitwa tashititi ambapo unafanya dhihaka kwa mtu anajua fika mtu huyu ni malaya unamwambia aisee we ni sister kabisa hii ni kejeli kwa simbachawene kumwambia kuwa rais wetu ni mfano bora wa kuigwa hali anjua kuwa ameshindwa kuongoza kisa madaraka anategea ukuu wa mikoa na wilaya huu ni unafiki wabunge wote wa ccm wanafiki wabunge matumbo ndo maana matumbo yamewaelemea wanasinzia bungeni akiamka anapiga meza ndiyooo mia kwa mia, hata waziri akikohoa anapiga makofi huu ni ujinga
 
Kwa mnaofuatilia bunge hususni developments tokea kikao cha jana cha Bunge, naomba tusemezane ni kipi kilichosemwa ktk hotuba Mh. Lema ambacho ni uchochezi au si cha kweli kuhusiana na performance ya jeshi la polisi?
 
Kwa mnaofuatilia bunge hususni developments tokea kikao cha jana cha Bunge, naomba tusemezane ni kipi kilichosemwa ktk hotuba Mh. Lema ambacho ni uchochezi au si cha kweli kuhusiana na performance ya jeshi la polisi?

Vyote ni vya ukweli kabisa, Lema ni shujaa sana, na piaaaa ni mtu mwenye akili sana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom