Luhanjo kamsafisha David Jairo hana tuhuma yoyote ya Rushwa

Na kama taratibu za kutowa fedha zilifutwa nini kitakacho fuata?
Arafat unaonekana kuwa na data za kutosha kuhusu Jairo, ila kwa sasa hajasafishwa popote! Labda ndio ndoto zako hizo ashafishike!
 
ni kama Rost tam tutaishia kumuita mwizi lakin hamna sheria yeyote ya kumfunga.

Umenena hivyo ndivyo itakavyo kuwa na mwisho wa siku hakuna atakalofanywa ndio maana sioni haja kutumia fedha zingine za walipa kodi kufanya uchunguzi wa kumpaka mtu mafuta.

Unakumbuka uchunguzi wa Richmond na Hoseah tuliishia kambiwa hakuna shaka mambo shwari kabisa baadaye weakleaks wanatoa Hoseah alikatazwa na Bossi wake juu ya rushwa kubwa ina maana kuwa Bossi wake amemuagiza ashughulikie rushwa za walal hoi tu!
 
Arafat unaonekana kuwa na data za kutosha kuhusu Jairo, ila kwa sasa hajasafishwa popote! Labda ndio ndoto zako hizo ashafishike!

we unadhani nini kitakachofuata? Kwa taarifa yako siku zote kosa lako likisha wekwa kwa Mamlaka yako ya Nidhamu basi kama lilikuwa kosa la jinai ndio tayari limefutwa.

Ukimpiga Mkeo na kumvunja mguu alafu mwendesha mashita anakwambia nyie ni mke na mme mkashuruhishane yaishe maana yake nini? au akifungua kesi chini ya sheria ya ndoa kudai talaka badala ya shambulio we uoni kuwa anakuepusha na kosa la msingi ulilolifanya?
 
Mkuu wangu Arafat nimekupata vizuri..
Kweli kabisa lazima Jairo asafishwe ili uchunguzi usiwafikie wale wanaopokea posho hizi ama Jairo atakuwa bangusilo kama ilivyotokea ktk sakata la Richmond. Mara zote viongozi wanapojiuzulu ama kusimamishwa kazi ni kupisha wasiingilie uchunguzi unaofanyika dhidi yao, lakini tumeyaona ktk sakata la IPTL, rada, Meremeta, Richmond na mengine mengi yasiyo na idadi ambako viongozi wamejiuzulu ama kusimamishwa lakini uchunguzi ukakoma pia kisha hao viongozi watuhumiwa kuhamishiwa nafsi nyingine za uongozi.. Wanapeta kama watu wasiokuwa na hatia yeyote..

Na ndio maana tunapata taabu sana na watu kama Lowassa, Chenge, Meghji, Karamagi na wengineo ambao walitakiwa kushtakiwa na wasafishwe mahakamani sio kesi kuishia chini chini kiasi kwamba wanarudi taratibu ktk uongozi. Ni mchezo wa CCM toka mwalimu Nyerere na kama kawaidsa ya utamaduni wao wanapokezana madaraka, mtu anaharibu hapa anahamishiwa sehemu nyingine hali mtu huyo ni mtuhumiwa ktk kazi yake ya awali...
Hii ndio Tanzania yetu na tunaipenda sana, labda tujikumbushe na wimbo huu kabla ya miaka 50, Uchungu wa upendo unaweza kuzua hamasa ya kudai haki ili sheria ichukue mkondo wake..

"Tazama ramani utaona nchi nzuriii, yenye mito na mabonde mengi ya nafakaa.
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri, nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzaniaa.
Maisha yetu haya yangekuwaje sasa, utumwa wa nchi Nyerere amekomeshaa.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa utumwa wa nchi Nyerere ameukomeshaa....."".

Aaaah! wala siendelei maanake inauma sana.... Utumwa, maisha na majira yetu ndio kwanza yanarudi ktk ukoloni mamboleo...
 
Wewe ni mgumu kuelewa sijui kwanini, unachojaribu kusema ndicho walicho kifanya wakina Luhanjo, kwa mujibu wa sheria za Utumishi wa Umma Luhanjo ni Mamlaka ya Nidhamu lakini nidhamu inayoongelewa hapo si makosa ya kijinai mbona huelewi.

Mtu akisha fanya makosa ya Kijina hapaswi tena kushughulikiwa na mamlaka ya kinidhamu dogo anashughulikiwa na vyombo vya dola kwa mujibu wa makosa husika. Unataka kusema wewe ukiuwa mtu Luhanjo atazua husikamatwe na kukupa Likizo ya siku kumi na kukuchunguza kama una makosa ya kinidhamu?

Kwa taarifa yako ukisha sikia makosa ya kinidhamu basi tayari kasafishwa kama hujui na hapo ndipo husipo pa elewa.

Kwa style hii ngoja niache uendelee na hoja zako Mkuu.
 
Mkuu wangu Arafat nimekupata vizuri..
...
Na ndio maana tunapata taabu sana na watu kama Lowassa, Chenge, Meghji, Karamagi na wengineo ambao walitakiwa kushtakiwa na wasafishwe mahakamani sio kesi kuishia chini chini kiasi kwamba wanarudi taratibu ktk uongozi. Ni mchezo wa CCM toka mwalimu Nyerere na kama kawaidsa ya utamaduni wao wanapokezana madaraka, mtu anaharibu hapa anahamishiwa sehemu nyingine hali mtu huyo ni mtuhumiwa ktk kazi yake ya awali...
Hii ndio Tanzania yetu na tunaipenda sana, labda tujikumbushe na wimbo huu kabla ya miaka 50, Uchungu wa upendo unaweza kuzua hamasa ya kudai haki ili sheria ichukue mkondo wake..

"Tazama ramani utaona nchi nzuriii, yenye mito na mabonde mengi ya nafakaa.
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri, nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzaniaa.
Maisha yetu haya yangekuwaje sasa, utumwa wa nchi Nyerere amekomeshaa.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa utumwa wa nchi Nyerere ameukomeshaa....."".

Aaaah! wala siendelei maanake inauma sana.... Utumwa, maisha na majira yetu ndio kwanza yanarudi ktk ukoloni mamboleo...

Mkuu Mkandara na shukuru sana kwa kuangalia hili swala kwa jicho la ndani zaidi, hakika tunatakiwa kujipanga barabara kabla ya 2015 nini cha kufanya na hasa juu ya swala la wizi wa kura sioni kama tunajiandaa nalo, hatuwezi kuwa na Taifa ambalo wezi wa kuku ndio wanateswa magerezani na hata kupewa kesi za uongo wakati watu wanao ujumu Uchumi wa Taifa wanatembea kifua mbele na kutuchoma vidole machoni tunapo wauliza kuliko? Hati kwa sababu wame wanunua Maafisa wetu katika vyombo vya dola kwa hizo fedha zao za wizi na hivyo vyombo vimekuwa sehemu ya uhalifu huu.

Wanajuwa kuwa Uchunguzi huu utaleta uozo kama ule wa Richmond ambao wakina Mwakyembe waliishia kusema kuna mambo tumeyaacha ili kusaidia serikali hisianguke what was that kama si kuwa wizi wa Richmond ulikuwa wa Viongozi kuibia nchni waliokabidhiwa?

Tanzania ni sehemu ya ajabu sana yani mtu anayekabidhiwa nchni ambaye anaishi bure kwa kodi za raia wa nchni hii ambaye amepewa uhakika wa kutunzwa hadi milele kwa kodi ya nchni ni lana gani inampata mpaka anashiriki tena kuibia hili Taifa maskini, angalia Wabunge pamoja na zile kelele za Posho zipunguzwe kumbe bado wakati wa kupitisha Bajeti wana hongwa ndipo ipite! hawa ni binadamu waliokamilika au ni Genus-homos?
 
Mleta mada hujui kitu.. Hata kuandika risiti hujui. Nenda ama rudi shule

Moja ya vitu ambavyo nilipojiunga Jamii Forum sikujua kuwa ni vingi ni KUFURAHISHA.....Hii niliyo highlight nayo imenifurahisha:)
 
Si mbaya...walau mmeelewa alichotaka kusema. Remember, Inglish iz not our motherland , tamthiliya za kidhungu tunaelewa kwa kuangalia sura na reaction za watu tu....not so much maneno. House girl wetu alikua anaelewa picha za kihindi ile mbayaa!!!!
Back to Topic!!!
Mkuu mi niliiona nikaamua kukausha
 
Mkuu wangu Arafat nimekupata vizuri...

Mkandala kwa hali ya kawaida kama haki ingetendeka walipaswa kuanzisha uchunguzi wa makosa ya jinai na hasa uhujumu wa Uchumi na Rushwa, maana unapo honga ili bajeti ipitishwe hapo kuna siri nzito sana ya hujuma maana haingii akili kama unaweza kuonga wabunge wapitishe kitu ambacho kipo kwa maslahi ya hii nchni hata kidogo!

Kwa viongozi wanao heshimu na kuogopa utaratibu na sheria za nchi mtu ambaye ana mamlaka ya kushauri Mtuhumiwa wa makosa ya jinai achukuliwe hatua na Mamlaka yake ya nidhamu ni DPP na hii ni baada ya kujiridhisha bayana kuwa pamoja na kosa lililopo bado itakuwa ni kupoteza muda kupereka kesi mahakamani kulingana na usafi wa ushahidi uliopo, maana hawa ni watu hatari ambao mara nyingi wanavuruga ushahi kwa gharama yoyote na hata kwa kumpoteza mtu kama walivyo mpoteza Balali; Luhanjo hana mamlaka yoyote ya kuzuia tuhuma za jinai zisifanyiwe kazi na vyombo vya dola bali ni matumizi mabaya ya mamlaka kama kawaida yao.

Hapo ndipo kwenye kumsafisha Mkuu
 
Si mbaya...walau mmeelewa alichotaka kusema. Remember, Inglish iz not our motherland , tamthiliya za kidhungu tunaelewa kwa kuangalia sura na reaction za watu tu....not so much maneno. House girl wetu alikua anaelewa picha za kihindi ile mbayaa!!!!
Back to Topic!!!

Posho za Jairo zinafanya kazi nini?
 
hii nukuu mbona kama imechakachuliwa vile, sio 'Like sands through the hourglass so are the Days of our Lives..'​ mwongozo wako tafadhali

Mkuu mi niliiona nikaamua kukausha

Si mbaya...walau mmeelewa alichotaka kusema. Remember, Inglish iz not our motherland , tamthiliya za kidhungu tunaelewa kwa kuangalia sura na reaction za watu tu....not so much maneno. House girl wetu alikua anaelewa picha za kihindi ile mbayaa!!!!
Back to Topic!!!

Siajelewa mnafanya mawasiliano gani Wakuu!
 
Kumbe mambo yenyewe ndo haya

Asante sana Luhanjo

images
 
Si kucomment mwanzo lakini sasa nimsifu Arafat kaonyesha ni kwa namna gani anajua karata zinavyochezwa, kama ni chase upo juu.
Waliokuwa wanakupinga wajitokeze sasa maana walifikiri
 
politics! politics! politica! politics! politics! politics! politics! politics! politics! politics!
 
Kumbe mambo yenyewe ndo haya

Asante sana Luhanjo

images

Siku zote ukishasikia tuhuma za jinai zinachunguzwa na Mamlaka ya Nidhamu ujuwe kuwa ndio imefutwa tayari, siyo jinai tena kama wangekuwa na nia thabiti ya kuchua hatua wange ruhusu vyombo vya dola kuchunguza na kama hakuna kosa basi DPP ndie angemsafisha lakini ukisha mpa nyani kesi ya ngedere unategemea nini?

Hakuna kosa Mkaguzi wa Mkuu angeweza kuona maana kazi yake ni kukagua uhasibu na kama kumbukumbu zimekwa sawa basi! Ukiangalia huu mjadala ndio unaweza kupata picha halisi ya uwezo wa wataalam wetu.
 
Back
Top Bottom