Lugha zetu ni mali ya kujivunia, ni Ujinga Kuzikwepa

Sir

Member
Aug 4, 2009
12
0
Nimekuwa nikilichunguza jambo hili ninalotaka kuzungumzia muda mrefu lakini limekuwa linanipa shida kuelewa ni nani wa kubebeshwa lawama au la.

Siku za hivi karibuni, kundi kubwa la watu hasa vijana wameamua kutokuwa na lugha wanayoifahamu kwa ufasaha wakijifikiria wao wanaenda na wakati sijui au ndio uelewa.

Utakuta mtu Mpale, Mzaramo au Mnyakyusa anafurahia kitendo chake cha kutokuweza kuelewa hiyo lugha akitoa ufafanuzi kwamba hajakulia huko na wala hapafahamu, hiyo huyo mtu unakuata pia anajifanya kutokujua kiswahili sababu amekulia nchi za nje au amesomea huko miaka kadhaa au mwingine alienda kutembea kwa wiki kadhaa.

Hii dhana ya kujivunia kutojua inatokana na nani hasa? Kama mtoto mdogo anazaliwa hajui kuongea lakini kwa jitihada binafsi anaelewa lugha na kuitumia inakuwaje mtu mzima anataabika kutokujua "Monday" inaitwaje kwa kwa kiswahili. Huyo ambaye hajui monday ni nini, amesoma ana Masters yupo bila aibu anamuuliza mpika chai ofisini ambaye anajua kabisa kwamba huyo naye kingereza ni tabu kwani elimu yake ni darasa la saba au pungufu na amekuwa bila mkanganyiko wa kizungu.

Juzi nimekutana na mtoto mdogo miaka minne pale sinza amenifurahisha sana, yeye ameamua kutumia muda wake wa ziada kujifunza lugha ya kwao kwani anaona wazazi wake nao wanajifanya hawaijui, huyo mtoto ameamua kuambatana na jirani ambaye ni kabila moja na wazazi wake kuelewa.

Kujua kitu usichokijua si ujinga, na kama una nafasi fanya ivyo si kukaa pembeni nakufurahia ujinga wa kutokujua.

Lugha ya nyumbani haujui kabisa, kiswahili fasaha matatizo, kiingereza ndo kabisa wewe unafikiri unakijua kumbe unaongea kiigereza cha malepa wa Marekani unasahau kwamba wao nje ya steji wanaongea vizuri.

Ni rahisi kusikiliza Mmarekani, Muingereza na mtu wa nchi zozote ambazo kwao kiigereza ni lugha ya kila siku ukamuelewa lakini mtanzania atajitahidi kuongelea puani au kuumauma maneno ili mradi sijui aonekane anaelewa lugha zaidi au kwamba hata ulimi wake umeisha haribika kutoweza kuongea lugha za kienyeji zisizokuwa za kisasa.

Wito wangu ni huu jivunie lugha yako na muone mtu ambaye hajui lugha ambayo hana sababu ya kutoijua kwamba ana matatizo ya akili na siyo mfano wa kuigwa.

Vijana wengi sasa hivi wametoka mavyuoni na wako kwenye mazoezi maofisini lakini huko wanajiona hakuna walichosoma kwasababu kiingereza cha kuteleza kinawapiga chenga matokeo yake wanaanza kusema elimu ya kitanzania haikidhi haja. Lugha sio elimu bali ni njia ya mawasiliano ambayo ni ya muhimu kwenye elimu. Hivyo wale wanaofunga njia ya mawasiliano kwa jamii zao za kitanzania siku moja watarudishwa huko wanakodhani ni kwao.
 
Kama unamsema huyu msichana aliyejitambulisha hapa JF kwa jina la ..N.Mwakasege, ambaye amesema yuko ..sijui Holand, siju Swiss,... huyo ni msanii, ndo maana watu wamembwatukia sana kwenye utambulisho wake!(refer Utambulisho)

Lakini kwa ujumla shida hiyo ni kubwa, ikiwa inatiwa petroli pale Dodoma Bungeni na watu wanaotegemewa kuwa ndo waelewa na wanaweza kutoa ushawishi wa juu kwa raia!
Utasikia ...`membaz wa komitii ya Miundombinu wakutane saa 8 ukumbi wa naninani sijui`...!
Ni ushambenga wa aibu!
 
Nakubaliana na Sir, kuwa lugha zetu za asili ni muhimu sana kuzitunza na kuziendeleza, kama historia na utamaduni wa taifa letu kwa vizazi vijavyo. Kuna haja ya kuundwa kwa mradi wa kudumisha na kutunza lugha hizo.
 
Back
Top Bottom