Lugha za kichina: Kuna haja ya kuingiza kwenye mitaala mashuleni?

Mtanzania1

JF-Expert Member
Dec 30, 2010
1,168
167
WanaJF uchumi na teknoloia ya china unakuwa kwa kasi kubwa. Wamefikia hali hiyo kwa kutumia lugha zao hasa katika upande wa teknologia. Hivi hakuna haja ya kuingiza lugha zao katika mitaala ya shule zetu kama vile yalivyo masomo mengine ya lugha kama kifaransa ili angalau tuweze kupata habari hasa za kiteknolojia kutoka kwao?
 
Wachina ni tofauti na wazungu, wachina wanauza bidhaa kama simu na kutafuta mali ghafi kwenye nchi zingine ni wao wa kujifunza hizo lugha husika. Wazungu wamejikita kwenye mambo ya utafiti na masuala ya demokrasia na utawala bora, kwa kupitia wazungu, wasomi wetu wanapata ajira kwenye miradi ya utafiti na serikali pia wanachota hela kwa wazungu kupitia masuala ya utawala bora na demokrasia. Ukichunguza kwa makini utagundua 95% ya wasomi wetu hujipatia mkate wao kupitia wazungu kwenye miradi mbalimbali iwe NGO au utafiti. Pia kumbuka wanachangia bajeti za serikali zetu za kiafrika na hata vyama vya siasa. Mchina kajikita zaidi kwenye biashara.
 
Hawa sasa ni ndugu zetu inabidi tuanze mapema kujifunza maana kariakoo wamejaa sana, mtaani kwetu wameanza kuuza bar. Sasa maelewano kidogo ya shda.
 
Back
Top Bottom