Lugha yetu

Msaada tofauti ya kiongozi na mtawala nashindwa kutofautisha

.
Kiongozi --- leader, guide.

Mtawala --- ruler, administrator

Mpaka hapo nafikiri utakuwa umeshapata tofauti.

Ila kwa kuongezea tu ni kwamba

Kiongozi ni yule anayewaongoza watu kwa kufuata sheria, kwa upendo, kuwajali na huku akijua kuwa wanaelekea wapi watu anaowaongoza na pia yupo tayari kukubali kukosolewa na ni msikivu kwa watu anaowaongoza.

Mtawala ni kinyume cha hayo hapo juu.

Yeye hajali nini wala nini. yeye anataka yale tu anayoyataka ndio watu wafanye, hataki kusikia maoni ya watu wengine, ukipishana nae mawazo anaweza hata kukufunga, kukupatia adhabu - hajali wewe unafikiriaje juu ya suala lolote. Na tawala zote zile dhalimu huwa ni zile ambazo mtawala anakuwa Dikteta

Yeye anatawala kwa amri.

Sasa nafikiri utakuwa umepata mwanga ... nyingine ongezea wewe.
 
Back
Top Bottom