kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
MCHEZAJI filamu za Bongo, Mohamed Miwkongi maarufu kwa jina la Frank, amesema kuwa lugha ya kiingereza ni kikwazo kikubwa na huwapiga chenga wasanii wengi wa filamu za Bongo.
Frank alisema kuwa wasanii wengi wa filamu za bongo hawaelewi vizuri kimombo na hushirikishwa kwenye filamu bila ya kujua maudhi na maana ya majina ya filamu hizo.
Frank alisema kuwa waigizaji wengi wanaokautana na matatizo hayo ni
wale wanaoshirikishwa kwenye filamu zenye majina ya Kiingereza.
"Wasanii wengi wanashiriki tu kwenye filamu, lakini hadi anamaliza
kucheza kipande chake hajui maudhui ya filamu yenye wala maana ya jina
la filamu aliyocheza," alisema Frank.
"Utakuta msanii anaambiwa kuna filamu inaitwa Avenger au Off Side
tunaomba ushiriki, tunakubali bila ya kujua maudhui (mtiririko) waala
maana ya jina",
"Ukikutana na msanii atakuambia kuna Avenger inakuja", alisema Frank.
"Ukimuuliza maana ama maudhui yake hajui," aliongeza Frank.
Frank alisema kuwa kwakuwa wasanii wengi wa Tanzania lugha ya Kiingereza imewapiga chenga, ni vyema kwa waandaaji wa filamu hizo kuwaeleza kwanza maana ama maudhui ya filamu hizo kabla ya kuwapa sehemu za kucheza ili waweze kuelewa kinachoendelea.