Lugha Rasmi Bungeni: Wabunge watumie Kiswahili au Kiingereza

Wakulaumiwa sio mheshimiwa bali sheria iliyompeleka bungeni, sheria inasema ajue kusoma na kuandika kiswahili kama alikidhi haya mahitaji hana kosa

Ishu ya pili ni ulafi wa madaraka, kama anajua uwezo wake wa kuzungumza na kuelewa kiingereza ni mdogo kwa nini anaomba nafasi ambazo zitatakiwa azungumze kiingereza?hivi akishinda hiyo nafasi na kwenda katika hilo bunge si atakuwa msindikizaji kila siku na sio mzungumzaji?
 
Hata mimi nilifuatilia...Lakini nadhani ni tatizo la ama mfumo wa mawasiliano pale bungeni, ama masikio yake kuwa na hitilafu ya kusikia vizuri, kwani alikuwa anaonekana dhahiri kujaribu kusikiliza kwa makini lakini alikuwa hasikii kinachoulizwa, hali ambayo hata wagombea wengine wawili walionekana kutatizwa hivyo. Ung'enge alioumwaga mwanzo usingemfanya ashindwe kujibu maswali yale.

kapongo ulimsikia wakati anataka kuomba swali lirudiwe? uliisikia sentensi aliyosema?
 
Huyu jamaa mbunge hafai kutuwakilisha kabisa, hii ni indicator tosha ya jinsi baadhi ya viongozi wetu tunaowachagua(sometimes kishikaji)ili wakatuwakilisha nje na wanapokuwa huko wanashindwa kabisa,hii inachanguwa na mambo kama ya huyu jamaa,unaona kabisa jamaa linataka kwenda kufukuzia posho na si kitu kingine.Kwa mnaosema eti angetumia kiswahili eti vile ni lugha ya Taifa,jamani, huyu jamaa si tu hajui kiingereze bali hata kama angeulizwa haya maswali kwa kiswahili bado angeshindwa tu.Ifike mahali watu wawe serious jamani.Mijamaa kama hawa wakichaguliwa huwa wanaenda kujaza matumbo na kufaidi deplomatic status hamna kingine,ndio sababu tunakwamaga wakati mwingine kwa mambo ya international affairs(haswa kwenye contract negotiations)kwani tunaweka watu bomu kama huyu jamaa(sijui ni mbunge wa wapi huyu?).Watu kama hawa wanapewaje ubunge?maana huyu jamaa nashindwa kumwelezea....LOL,tunao wengi aina nchin,..i LOL.....
 
Inawezekana kuna point, lakini kuna wakalimani ambao kazi yao ni kuondoa kikwazo cha lugha, na uwakilishi hautakiwi kuwekewa vikwazo vya lugha. Kinachotakiwa ni uwezo wa uwakilishi. Ukiangalia bungei kwetu kuna wabunge wengine kazi yao ni kuhudhuria tu na si kuwakilisha. So what matters most ni uwezo wa uwakilishi na kuondoa vikwazo vya lugha. Si kuongea kiingereza.

It is absolutely stupid to think that inability to express in English is a tragedy and shame, unless you there is something wrong in your head. We have so many people in Tanzania who are very fluent in English and speak like someone in oxford, but what they utter is absolutely crap. Kuna vijana wa clouds walikuwa wanaongea vizuri sana kiingereza lakini walikwenda chuo Kikuu mlimani wali-disco uwezo wao ulikuwa kuongea kiingereza tu, lakini kichwani hakuna kitu.We have plenty people who can not even express themselves well in Kiswahili, but they are are full of intellect and wisdom, hata ukisikiliza sentensi moja tu wanaongea utajua kuwa ni mtu mwenye akili timamu anaongea.

Try to listen Medvedev speak English or Hugo Chavez for that matter, unaweza kuona hata huyo mbunge yuko better. I may be wrong, lakini sioni kama kujua au kutojua kiingereza ni aibu.

Mkuu,
Nimependa sana maoni yako. Yamekwenda shule. Hata hivyo, tusi'justify' uvivu wetu wa kutojifunza lugha za kigeni na masuala mbalimbali ya kimataifa, huku tukijilinganisha na wengine. Tujitahidi sana tusome kila siku, kila wakati na kujifunza lugha zote kwa ufasaha.Kuna watu wengi ambao hawataki kujifunza, wakiwemo waandishi wa habari wa magazeti ya Kiswahili. Ukisoma makala zao za Kiswahili, utachoka. Wanarashia-rashia. Ninawashauri watu wote tupende kujisomea. Kila siku ya Ijumaa, tusome gazeti la Mwananchi, kuna mzee mmoja anaitwa Maina. Anajitahidi sana kunyoosha lugha ya Kiswahili. Kwa mfano, ni wangapi wanafahamu kwamba neno MTAALA si sahihi, bali neno sahihi ni MTALAA!? Samahani nimeandika mingi kiasi cha kutaka kutoka nje ya mada.
 
Huyo mbunge ni muingereza?........ Jibu ni la .....

Bunge alilokuwa anaongea ni la uingereza......Jibu ni la.....

Kama ni hivyo basi.....AIBU NI YA KITU GANI........
HUO NI UKOLONI WA AKILI......MBONA WENYEWE WAINGEREZA HAWAJUI KISWAHILI NA WALA THEY DONT FEEL SORRY......

KUMBE MWALIMU NYERERE ALISEMA KWELI........ALIPOSEMA KUJUA LUGHA YA BWANA MKUBWA NI FAHARI........
ONA SASA YANAYO TOKEA...........

KUHUSU BUNGE LA PAN AFRIKA INABIDI KISWAHILI KITUMIKE PIA.....
katika kuhalalisha udhaifu wetu huwa tunapenda kusema haya unayoyasema lakini kumbuka hata hao wenzetu wanaoendelea wanajitahidi kujua angalau moja kati ya lugha 3 za dunia. Hapa nasema Wachina, India, Brazil na hata baadhi ya nchi za ulaya zenyewe. Hivi unajua kuwa ENGLISH (KINGEREZA) ni official language hapa Tanzania!? ...sasa kwa nini legislator ashindwe wakati anataka akawakilishe wananchi. Hili ndilo tatizo la kufikiri "KILOLIONDO LOLIONDO". Hatungependa kuendelea kubakia hapa tulipo kwa vile na lugha tumeishalionani tatizo, unakuta mbunge ana dish/DSTV kwake lakini anaishia kwaangalia akina Kanumba hivyo kushindwa kujua hata kile kinachoendelea Ivory Coast na kwingineko.
 
Mkuu,
Nimependa sana maoni yako. Yamekwenda shule. Hata hivyo, tusi'justify' uvivu wetu wa kutojifunza lugha za kigeni na masuala mbalimbali ya kimataifa, huku tukijilinganisha na wengine. Tujitahidi sana tusome kila siku, kila wakati na kujifunza lugha zote kwa ufasaha.Kuna watu wengi ambao hawataki kujifunza, wakiwemo waandishi wa habari wa magazeti ya Kiswahili. Ukisoma makala zao za Kiswahili, utachoka. Wanarashia-rashia. Ninawashauri watu wote tupende kujisomea. Kila siku ya Ijumaa, tusome gazeti la Mwananchi, kuna mzee mmoja anaitwa Maina. Anajitahidi sana kunyoosha lugha ya Kiswahili. Kwa mfano, ni wangapi wanafahamu kwamba neno MTAALA si sahihi, bali neno sahihi ni MTALAA!? Samahani nimeandika mingi kiasi cha kutaka kutoka nje ya mada.

I second you mkuu, hata angalau angejibu maswali yake with brocken kiinglishi lakini watu waelewe anamaanisha nini!!! Huyu mbunge anyetaka kwenda PAP, hajui hata yanayotokea kwenye nchi zingine za Africa!!! Uvivu wetu umekithiri...
 
Suala la lugha gani itumike katika kuwapata wabunge wa africa upande wangu naona Kiingereza ni sahihi kabisa kama na kanuni zinasema hivyo ni sahihi. Hivi tunahitaji mwakilishi atakayeongea kiswahili tu mradi ni lugha inayotumika kule hana hata uwezo wa kubadilishana mawazo na wabunge wenzake?

Hata kama tukitetea lugha iliyotumika bado kuna mambo ya kujiuliza
1. Hivi kweli hakuwa anasikia hata maswali mbona majibu ni mbofumbofu? Hata general knowledge hapa ni tatizo maana nilitegemea kusoma majibu japo yawasilishwe kwa Kiingereza kilichovunjika vunjika
2. Huyu mheshimiwa ni msomi mwenye shahada ya Uhasibu na fedha kweli ndiyo hata kujieleza kwa maswali hayo tu anashindwa?

Hapa kuna tatizo!!!!
 
Inawezekana kuna point, lakini kuna wakalimani ambao kazi yao ni kuondoa kikwazo cha lugha, na uwakilishi hautakiwi kuwekewa vikwazo vya lugha. Kinachotakiwa ni uwezo wa uwakilishi. Ukiangalia bungei kwetu kuna wabunge wengine kazi yao ni kuhudhuria tu na si kuwakilisha. So what matters most ni uwezo wa uwakilishi na kuondoa vikwazo vya lugha. Si kuongea kiingereza.

It is absolutely stupid to think that inability to express in English is a tragedy and shame, unless you there is something wrong in your head. We have so many people in Tanzania who are very fluent in English and speak like someone in oxford, but what they utter is absolutely crap. Kuna vijana wa clouds walikuwa wanaongea vizuri sana kiingereza lakini walikwenda chuo Kikuu mlimani wali-disco uwezo wao ulikuwa kuongea kiingereza tu, lakini kichwani hakuna kitu.We have plenty people who can not even express themselves well in Kiswahili, but they are are full of intellect and wisdom, hata ukisikiliza sentensi moja tu wanaongea utajua kuwa ni mtu mwenye akili timamu anaongea.

Try to listen Medvedev speak English or Hugo Chavez for that matter, unaweza kuona hata huyo mbunge yuko better. I may be wrong, lakini sioni kama kujua au kutojua kiingereza ni aibu.

Try to understand the point bongolander, no one here is saying ability to speak/understand English is a measure of ones intellect, lakini nasisitiza LAKINI kwa position ile walikua wanataka mtu mwenye uweko wa kujieleza kwa kingereza ndo maana kanuni za Bunge, pamoja na kujua kwamba Kiswahili ni lugha ramsi, bado zinataka kingereza kitumike katika kujieleza.

Pili, Tofauti na ujerumani, china, korea,, ufaransa na nchi ambazo wanasoma kwa lugha nyingine Tanzania tunaanza kufaundishwa kingereza toka primary, ukifika secondary Kingereza inakuwa lugha ya kufundishia, sasa unapomuona mtu aliyesomea Tanzania afu anakuwa na shida ya kuongea kingereza kwa kiwango cha MPINA, swali linakuja, alifika kweli secondary?

Tatu, Watu kama mpina wanachangiaje mada unapopelekwa muswada ulioandikwa kimombo? i mean si lazima kuchangia kimombo, lakini kama anashindwa kabisa namna ile ina maana yeye ni rubber stamp tu, chochote kitachopelekwa bungeni kitapita tu, atahoji vipi kama uelewe wake wa lugha inayotumika kuandika miswada uko chini kiasi kile
 
Amesoma shule za kata. Na bado je vipi mpaka 2020 kama tutakuwa hatunyakua nchi ili kuwanusulu na shule za JK.
 
Kwa Taarifa:
Kiswahili ni Moja kati ya Lugha Rasmi katika PAP (Pan African Parliament)

Wabunge wanalijua hilo, na kabla uchaguzi haujaanza kulikua na mvutano wa Lugha gani itumike katika huo mchakato wao wa uchaguzi na hoja ya kwamba Kiswahili ni moja kati ya lugha rasmi ilitolewa.

Lakini kanuni za bunge zimesema categorically kwamba kingereza ndio lugha itakayotuma katika mchakato wa kuchagua wawakilishi wa kwenda PAP, pia katika bunge la afica kuna formal na informal discussions, hamna shida katika formal discussions kwani itatolewa tafsiri kwa lugha zote rasmi lakini baada ya hapo, according to waliokuwa wakitetea kwamba kitumike kingereza (akiwemo Membe), mtu kama hajui kingereza ataachwa nyuma, atashindwa kushirikiana na kujadiliana vizuri na wenzake

Mwisho,
Si unajua Miswada yetu yote inaendaga bungeni ikiwa haijaandikwa kiswahili, hata ule mswada wa mwisho ule ulozua makelele sana si unajua ulikuwa umeandikwa kwa lugha gani? sasa mtu kama Luhaga atachangiaje katika mswada ule? tena mswada wenyewe ulipelekwa kwa vote of urgency!

Kwa hili tuache tu waende wale wanaoweza kuwasiliana kwa kiingereza fluently, tusidanganyane bana kujua kiingereza sio kuelimilika, lakini kiingereza ni nyenzo muhimu kuelekea kuelimika. katika ulimwengu huu wa global village huwezi kutegemea nyumba mbili tu, kiswahili na kinyumbani.
 
Nimewatoa hapa nikawapeleka pale.

By JK PUR or TZ .economist univesty of Dodoma
 
Suala la lugha gani itumike katika kuwapata wabunge wa africa upande wangu naona Kiingereza ni sahihi kabisa kama na kanuni zinasema hivyo ni sahihi. Hivi tunahitaji mwakilishi atakayeongea kiswahili tu mradi ni lugha inayotumika kule hana hata uwezo wa kubadilishana mawazo na wabunge wenzake?

Hata kama tukitetea lugha iliyotumika bado kuna mambo ya kujiuliza
1. Hivi kweli hakuwa anasikia hata maswali mbona majibu ni mbofumbofu? Hata general knowledge hapa ni tatizo maana nilitegemea kusoma majibu japo yawasilishwe kwa Kiingereza kilichovunjika vunjika
2. Huyu mheshimiwa ni msomi mwenye shahada ya Uhasibu na fedha kweli ndiyo hata kujieleza kwa maswali hayo tu anashindwa?

Hapa kuna tatizo!!!!

Kumaliza, anaweza kuwa amemaliza chuo kikuu. Hakuna uhusiano kati ya Digrii nyingi (ukiondoa linguistics) na lugha. Mbona kuna 'ma-lecturer' kibao hawajui kiingereza? Kinachotakiwa hapa Tanzania, ni juhudi binafsi za kujifunza lugha za nje, kwani tunatumia sana Kiswahili. Ila kutumia Did badala ya Can, ni uzembe uliotukuka!
 
Well, tuache mzaha na kujaribu kufukia udhaifu wetu. Katika nchi hii lugha rasmi za mawasiliano bado ni Kiswahili na Kiingereza. Kiingereza ni lugha ya kufundishia na kujifunzia kuanzia sekondari hadi chuo kikuu. Hatujabadilisha sera yetu ya lugha. Hivyo hatuwezi kutetea udhaifu kwa visingizio kwamba sio lugha yetu. Ni muhimu sana nchi iwe na lugha yake na vilevile iwe na angalau lugha moja ya kimataifa. Sisi tumechagua Kiingereza kuwa ndiyo lugha yetu ya kimataifa. At minimum, tunatarajia wabunge wetu waijue lugha hii ya kimataifa sawasawa. Kama hawaijui wanatakiwa wajifunze waijuie. Kwa muda mrefu tumekuwa tukihalalisha udhaifu wetu wa lugha za kimataifa kwa sababu za kizembe. Kwamba nchi zingine pia hawajui sio sababu nzuri ya sisi kutokujua.
 
Huyo mbunge ni muingereza?........ Jibu ni la .....

Bunge alilokuwa anaongea ni la uingereza......Jibu ni la.....

Kama ni hivyo basi.....AIBU NI YA KITU GANI........
HUO NI UKOLONI WA AKILI......MBONA WENYEWE WAINGEREZA HAWAJUI KISWAHILI NA WALA THEY DONT FEEL SORRY......

KUMBE MWALIMU NYERERE ALISEMA KWELI........ALIPOSEMA KUJUA LUGHA YA BWANA MKUBWA NI FAHARI........
ONA SASA YANAYO TOKEA...........

KUHUSU BUNGE LA PAN AFRIKA INABIDI KISWAHILI KITUMIKE PIA.....

Unasemaje kuhusu miswada inayoandaliwa kwa kiingereza? Hii inamaana kuna wabunge wengi tuu hawaielewi kabisa miswada inayoletwa bungeni. Zaidi ya hapo, ni hao hao wenye uwezo wa kuhakikisha kanuni zinabadilishwa ili hata miswada na sheria viwe kwa lugha yetu ya kiswahili, lakini hawataki kufanya hivyo.

Binafsi nafurahi hili limetokea maana tumeelewa vizuri tuna wabunge wa aina gani.
 
Kwa kweli Kiingereza kinawapa taabu wabunge wengi tu hata huyo Spika Mwenyewe kinamsumbua. Wabunge wanaongea kiingereza kama chan waalimu wa shule ya Msingi tena ya kata. Hapo ndipo wajanja wachache wajuaji wanapotumia mwanya huo kutubamiza na miswada na mikataba yako ya ajabu.

Hakika majimbo mengi tu yanaongozwa na wabunge vilaza. poleni mlioichagua CCM
 
Inawezekana kuna point, lakini kuna wakalimani ambao kazi yao ni kuondoa kikwazo cha lugha, na uwakilishi hautakiwi kuwekewa vikwazo vya lugha. Kinachotakiwa ni uwezo wa uwakilishi. Ukiangalia bungei kwetu kuna wabunge wengine kazi yao ni kuhudhuria tu na si kuwakilisha. So what matters most ni uwezo wa uwakilishi na kuondoa vikwazo vya lugha. Si kuongea kiingereza.

It is absolutely stupid to think that inability to express in English is a tragedy and shame, unless you there is something wrong in your head. We have so many people in Tanzania who are very fluent in English and speak like someone in oxford, but what they utter is absolutely crap. Kuna vijana wa clouds walikuwa wanaongea vizuri sana kiingereza lakini walikwenda chuo Kikuu mlimani wali-disco uwezo wao ulikuwa kuongea kiingereza tu, lakini kichwani hakuna kitu.We have plenty people who can not even express themselves well in Kiswahili, but they are are full of intellect and wisdom, hata ukisikiliza sentensi moja tu wanaongea utajua kuwa ni mtu mwenye akili timamu anaongea.

Try to listen Medvedev speak English or Hugo Chavez for that matter, unaweza kuona hata huyo mbunge yuko better. I may be wrong, lakini sioni kama kujua au kutojua kiingereza ni aibu.

It seems you want to fool us. Hii nafasi siyo lazima apewe yeye, kama yeye aliomba akidhani ana sifa zaidi ya wabunge wengine alitakiwa aonyeshe kweli anawazidi wenzake. Hawezi kutuwakilisha wakati kuna wengine wanaomzidi yeye.
 
Kumaliza, anaweza kuwa amemaliza chuo kikuu. Hakuna uhusiano kati ya Digrii nyingi (ukiondoa linguistics) na lugha. Mbona kuna 'ma-lecturer' kibao hawajui kiingereza? Kinachotakiwa hapa Tanzania, ni juhudi binafsi za kujifunza lugha za nje, kwani tunatumia sana Kiswahili. Ila kutumia Did badala ya Can, ni uzembe uliotukuka!

unaona eeeh!
 
Back
Top Bottom