Lugha maridhawa. KISWAHILI

Mwanahisa

JF-Expert Member
Jun 29, 2012
1,382
510
Msaada tutani tafadhali.

Kandambili, hilo neno mbili linahusiana na tarakimu ya namba 2?

Je (sandals) au Open shoe kwa lugha yetu sanifu ni nini?
 
Mwanahisa kwa mujibu wa Kamusi ya TUKI

sandal n = ndara; makubadhi, kandambili, malapa.

~led
adj liovaa ndara.
 
Preta aksante, Dotworld je TUKI wanasemaje juu ya neno mbili, kwasababu ziko mbili nikimaanisha JOZI au ni kushabihiana kwa maneno tu?
 
Last edited by a moderator:
kUMEKUWA NA MCHANGANYO WA TAFSIRI TOFAUTI KWA MANENO HAYA,
AGHALABU.......?
YUMKINI...........?
UPEMBUZI YAKINIFU.........?
MARIDHAWA....................?
MURUA............................?
 
kUMEKUWA NA MCHANGANYO WA TAFSIRI TOFAUTI KWA MANENO HAYA,
AGHALABU.......?
YUMKINI...........?
UPEMBUZI YAKINIFU.........?
MARIDHAWA....................?
MURUA............................?

Aghalabu====Mara nyingi
Upembuzi yakinifu===Mchanganuo
Maridhawa=====Maridadi, nzuri, yakupendeza,Safi,Njema,siha nzuri
Murua======Safi , njema, maridadi,pendeza,enye afya.

Masahihisho nayapokea
 
Preta aksante, Dotworld je TUKI wanasemaje juu ya neno mbili, kwasababu ziko mbili nikimaanisha JOZI au ni kushabihiana kwa maneno tu?

Hiyo mbili kwenye kanda mbili, ni zile kanda mbili zinazounganika kwenye kidole.

Yaani unakuwa na sehemu ya flat unapoweka unyayo wako, na zile kanda [mbili] zinazoshikulia unyayo wako usiondoke kwenye kiatu

Hiyo ndio asili ya mbili kwenye kandambili, na sio maana ya jozi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom