Wa kusoma
JF-Expert Member
- Jul 30, 2011
- 3,454
- 2,975
Ukipenda waweza kuiita tetesi, news alert, breaking news au vyovyote upendavyo. Lkn habari zilizonifikia kutoka chanzo changu cha habari kilichoko ikulu na bila shaka yoyote ni mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali ndg. Utoh ameteuliwa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na katibu mkuu kiongozi mzee Luhanjo aliyestaafu december 1, 2011. Inasemekana kwamba Utoh alipendekezwa na Luhanjo mwenyewe kabla ya JK kukubali mapendekezo hayo.
My take: Ikumbukwe wote hawa walikumbwa na kashifa ya Jairo na inasemekana uteuzi wa wakuu wa mikoa na wilaya, na makatibu wakuu wa wizara mbalimbali umefanywa na Luhanjo kwa kuwaweka maswahiba wake.
Nawasilisha wakuu.