Lucky or NOT...??

kipimo ni matarajio.......................na kulinganisha na ulichonacho.......................matokeo ni mafanikio au kuyakosa mafanikio...........nionavyo sisi hudhani ya kuwa tuna sauti juu ya maisha yetu.............................lakini ukweli ni kuwa safari zetu zilipangwa na Muumba kabla dunia hii haijaumbwa.......Daniel 4:32-37 na Ephesians 2:10
kweli kaka wanadamu huwa tunajisahau sana huwa tunasahau kuwa mungu ndo muweza, mi kwa upande wangu huwa namshukuru mungu kwa kila jambo.
 
mamkwe mzima wewe

kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa mema mengi aliyonijalia ni kwa bahati ya pekee amenijalia kuniondolea machungu niliyokuwa nayo na bado anaendelea kunipigani na kunisimamia..............siwezi kusema kwa nguvu zangu nimewazi kitu ni kwa nguvu zake aliye juu......kwanza anakupa akili ya kutafuta na namna ya kutumia......wakati mwengine unajaliwa bahati ya kupata kama alivyosema MBU lakini unakuwa huna maarifa ya jinsi ya kutumia mwisho wa siku unakuja sema huna bahati ukumbuki ulipata bahati hiyo ukaichezea..........na wengine hawajapata bahati ya kuwa na kile anachotamani kuwa nacho lakini kwa namna nyingine anabahati ambayo mwingine anaitamani.......
 
  • Thanks
Reactions: BAK
apolo1.jpg
...hawa 'nyoka' wanakamata 'mawe' ya mamilioni ya fedha...ila ndio hivyo tena...wanasafisha jina kwa kununua makreti ya bia kukoshea magari yao wanayoyanunua hapo kwa papo... pesa zikiisha wanarudi migodini kuanza upya kusaka bahati zao..!

waulize vijana wa mererani, mbuguni na kwingineko...ni wangapi wanaobahatika...
kisha jifikirie na tanzania yetu hii tuliojaaliwa 'bahati' ya kila maliasili...taifa bado li masikini.

Umenikumbusha jamaa aliwahi kupata mawe akaingia baa akafunga milango wote waliokuwepo walikunywa na kula mpaka kukakucha bili kwake..........leo ukimwona anatia huruma anagongea nauli ukimnyima anakwambia wee niliwahi kushika pesa kuliko hizo zako na hakufanya lolote
 
Umenikumbusha jamaa aliwahi kupata mawe akaingia baa akafunga milango wote waliokuwepo walikunywa na kula mpaka kukakucha bili kwake..........leo ukimwona anatia huruma anagongea nauli ukimnyima anakwambia wee niliwahi kushika pesa kuliko hizo zako na hakufanya lolote

...kwenye mapenzi hivyo hivyo....mtu anapata mke/mume wa maana, halafu anaichezea bahati yake...siku ya siku wakishaachana utamsikia...wewe mimi ndio niliokuanza, hata ukiwa na mtu mwingine nitakuharibia!...

hapo atamlaumu nani ati hana bahati?
 
  • Thanks
Reactions: BAK

...kwenye mapenzi hivyo hivyo....mtu anapata mke/mume wa maana, halafu anaichezea bahati yake...siku ya siku wakishaachana utamsikia...wewe mimi ndio niliokuanza, hata ukiwa na mtu mwingine nitakuharibia!...

hapo atamlaumu nani ati hana bahati?

Nakubaliana nawe Mkuu Mbu halafu akishaharibu ndio anabaki kujuta na kama tujuavyo majuto ni mjukuu...Bahati ipo sana tu hapa duniani. Utaona watu wanaweka efforts zile zile katika kazi, biashara, mapenzi n.k. na baadhi mambo yao yanawanyookea kila siku na raha tele ndani ya roho na wengine kila siku ni kutoona mafanikio katika baadhi ya sehemu hizo nilizozitaja au kwenye kila kitu.



 
Last edited by a moderator:
nakubali na nina amini bahati zipo me binafsi siku kama mbili zilizopita nilipokuwa eneo la kazi nilipoteza kiasi kikubwa cha pesa ambazo ni za boss wangu, nilisali sala zote coz nilijua lazima ntafungwa,kumbe kunamteja hakulipa pesa baada ya kuchukua kias kikubwa cha bidhaa wakati bos anakuja kufunga hesabu yule mteja akaja kulipa pesa yaani sikuamin so namshukuru sana Mungu..bahat zipo jaman
 
Back
Top Bottom