LUBUVA: Walioshindwa kwenye uchaguzi waache kujitangaza kuwa walishinda

Twende taratibu. Timu ya CDM pale Double view Hotel (Sinza) ilibumba na kusambaza mitandaoni matokeo ya urais kwa Jimbo la Ubungo, etc. Lakini, kwa upande wa Ubungo, hata Kubenea (MB) akiulizwa leo hii aseme kama alijua mgombea urais wake Lowassa alikuwa amepata kura ngapi kabla ya yeye kuondoka kituo cha majumuisho atasema "hapana." Alipewa taarifa baadaye. Kwa hiyo, hana ground ya kufanya refutation. Hali ilikuwa hivyo nchi nzima isipokuwa Arumeru kwa Joshua Nassari pekee!

Pale Ubungo, mara tu baada ya yeye kutangazwa mshindi Kubenea alikimbilia mitaani kusherehekea. Mawakala wake waliondoka naye. So, timu ya Double view ilipata wapi data za Urais Ubungo kama zilivyosambazwa mitandaoni? Forgery tupu!

Yote haya yalitokea kwa sababu kuu ni moja kuu. Kampeni Meneja wa Lowassa, John Mrema, alitakiwa kusambaza fedha za mawakala nchi nzima lakini hakufanya hivyo. Hata fungu la wagombea Ubunge nalo alilizima.

Nakumbuka siku moja saa nne usikupale Mwanza, Lwakatare aliambiwa ajibanze kona fulani kusubiri uwezeshaji kutoka kwa John Mrema, lakini alishtuka ni saa sita usiku na Mrema haonekani wala kupatikana kwenye simu. Hali ilikuwa hivyo nchi nzima. Tuachane na "usanii wa kura ziliibiwa." Tufanye post-mortem na kutambua majipu yalipo ili yatumbuliwe. Vinginevyo tunapinga ngoma majini...

Kwa ufupi Lowassa alitapeliwa na campaign team yake. Anapaswa kuufahamu ukweli huu hata kama ni mchungu.

Inatosha kwa leo. Sitaki kuendelea nikaongelea kuhusu wale vijana kutoka Israeli, Ufaransa na China...
Endelea tafadhali hizo hoja zipeleke kwa watakaozisilkiiza. Facts on the ground are different and you are confirming them in the first paragraph
 
Back
Top Bottom