LUBUVA: Walioshindwa kwenye uchaguzi waache kujitangaza kuwa walishinda

Wewe jinga la Nyumbu mpaka Leo haujui kwa nini walikamatwa!!!!


Vijana Wa chagadema, wengine walikuwa raia Wa kigeni walikuwa hawakusanyi matokeo .


Walihack account ya tume na kuanza kuchakachua matokeo.
Ushahidi wa kuhack uko wapi? Mimi na wewe nani nyumbu? Mwenyekiti wenu kasema yote nyumbu na misukule ni kina nani.
 
Ushahidi wa kuhack uko wapi? Mimi na wewe nani nyumbu? Mwenyekiti wenu kasema yote nyumbu na misukule ni kina nani.
Chezea mkwere weye, yule halali na siri lazima atayaanika yoote.tuvute subira tu atatueleza hata issue ya escrow ilikuwaje
 
Nawalaumu wazazi wako walio kulea
heri yangu kuliko wakwako waliokutelekeza.. nadhani hamu yako nisirudi tena kuchangia si ndio ? naweza kufanya hivo but sio kwa kukuridhisha wewe ila najua invisible yuko very close na unaweza kunipatia ban ya hovyo , bora nipigwe ban nikiwa nimekoseana na yeyote kuliko wewe chizi maarifa. Adios
 
heri yangu kuliko wakwako waliokutelekeza.. nadhani hamu yako nisirudi tena kuchangia si ndio ? naweza kufanya hivo but sio kwa kukuridhisha wewe ila najua invisible yuko very close na unaweza kunipatia ban ya hovyo , bora nipigwe ban nikiwa nimekoseana na yeyote kuliko wewe chizi maarifa. Adios
Wewe huna akili zaidi ya kurusha matusi hapa jukwaani,au unadhani hiyo ndio njia muafaka ya kufikisha ujumbe kwa kikwete kuwa nawe ni mpigania chama?wacha kuwa na akili ya kiwavi kama huyu
1454936005433.jpg
 
Lowasa na wafuasi wake hawana akili hiyo. Akili zote zinaelekezwa kwenye namna ya kukwepesha majipu yao yasitumbuliwe.
Kwa maoni yangu, Jaji Lubuva anayo hoja.

Lowassa anapaswa kuendesha siasa za hoja akiwa anafahamu kwamba siasa bila uwongo inawezekana. Kuna hoja nyingi hazina mtu wa kuzishikia bango. Mfano ni matatizo katika sekta ya afya, elimu, itikadi ya kitaifa, oikonomia (uchumi) na utawala. Kila eneo atafute hoja moja kubwa na kuifanyia kidedea. Atalisaidia sana Taifa. Mfano:

Katika AFYA: Katika sekta za Afya ya wastaafu, wazee, walemavu, mama na mtoto kuna changamoto lukuki leo. Lowassa, akifanya utafiti, anaweza kulisaidia Taifa kwa kuchokonoa eneo hili angalau mara moja kila mwezi.

Katika ELIMU: Rais Magufuli aliahidi "elimu bila malipo." Utekelezaji wa ahahdi hii umeanza lakini modus operandi yake inazua maswali kuliko majibu. Lowassa, akifanya utafiti, anaweza kulisaidia Taifa kwa kuchokonoa eneo hili angalau mara moja kila mwezi.

Katika ITIKADI ya kitaifa: Kwa kuangalia safari yetu kutoka "Azimio la Arusha," kupitia "Azimio la Zanzibar" hadi "Azimio la Mkapa Kuhusu Tanzania ya 2025," ni wazi kwamba Tanzania ya leo inasumbuliwa na ombwe la itikadi ya kitaifa. Na bila itikadi ya aina hii, Watanzania hatuwezi kuwa na ramani ya mabadiliko (theory of change) kuelekea Tanzania Mpya kwa mujibu wa Magufuli. Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, yaani mixed economy, katika zama za leo inapaswa kuwa na sura gani katika mazingira ya Tanzania? Lowassa, akifanya utafiti, anaweza kulisaidia Taifa kwa kuchokonoa eneo hili angalau mara moja kila mwezi.

Katika OIKONOMIA (uchumi): Rais Magufuli alisema "Tanzania ya Magufuli itakuwa nchi ya viwanda." Mpaka sasa hatujasikia akizindua angalau kamati ya kuandaa "Industrial Policy" ili hatimaye aweze kutoa mwongozo kuhusu jambo hili. Lowassa, akifanya utafiti, anaweza kulisaidia Taifa kwa kuchokonoa eneo hili angalau mara moja kila mwezi.

Na katika UTAWALA: Rais Magufuli aliahidi kuunda "serikali ndogo" kuliko aliyoikuta wakati anaingia madarakani. Je, kuna tofauti yoyote ya maana kati ya idadi ya watumishi wa umma kabla na baada ya Magufuli. Lowassa, akifanya utafiti, anaweza kulisaidia Taifa kwa kuchokonoa eneo hili angalau mara moja kila mwezi.

Mpaka hapo, Lowassa anayo angalau hoja moja kila wiki!
Siasa bila uwongo zinawezekana!

Kwa kweli, sisi tunapenda siasa za hoja. Ile nadharia kwamba "ukitaka kuwa mwanasiasa mzuri inabidi uuone ukweli kama mama mkwe wako," imepitwa na wakati.

Baadhi ya Maaskofu, walikuwa wakiamini hapo zamani kwamba, "What is good and evil, righteous and sinful, constructive and deconstructive in human history usually is intertwined in complicated ways," na kwamba, "Practices and institutions of our common life are an ambiguous mixture of good and bad, sometimes in ways that are difficult to separate or even see."

Hata hivyo, hawa nao siku hizo wameanza kuondoka katika kambi hiyo yenye harufu ya KImachiaveli. Huenda wamegundua kwamba kama "Mungu ni Ukweli," basi, ili kubaki Askofu ambaye ni halifa wa Mungu huyo ni lazima ujitenge na uwongo kila mahali, kila wakati na katika mahusiano yako na kila mtu. Kusema uwongo ni kukanusha uwepo wa Mungu! Hivyo, kaulimbiu lazima ya kila Kuhani lazima iwe: Telling truth every where, every time and to every deserving subject.

Lowassa akisimamia vizuri kauli yake kwamba: "Nimepoteza pambano, lakini sio vita," akaendeleza vita ya hoja zisizokanushika, anaweza kushinda. Lakini, hoja zinazokiuka kanuni ya ukweli hazitamsaidia kushinda pambano hata moja, achilia mbali kushinda vita.

Kwa sasa ngoja niishie hapa, halafu niwatafute Dk. Slaa na Maria Sarungi. Kuna jambo nataka kuwauliza kuhusu uchaguzi wa mwaka 2010....
 
Mzee wangu alikuwa niwa kuheshimiwa kijiji kizima, alikuwa mpole Na mwenye huruma, alikuwa mpenda haki, alikuwa ana penda kutembelea hosp na kusaidia watu chakula pamoja Na pesa za matibabu, kila binadamu ana mapungufu yake ila Mzee wangu hakuwa mnafiki wala mchumia tumbo, Mungu amlaze pahala pema.


Ameen.

Kama kweli jifunze kutoka kwake, mdomo mpana hufinya masikio.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva amewataka wanasiasa walioshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu waache kujitangaza kuwa walishinda, akisema wanapotosha wananchi.

Kauli hiyo ya Jaji Lubuva imekuja siku chache baada ya aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa kudai kuwa kama si matokeo kuchakachuliwa, alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwa sababu wananchi walishaichoka CCM na wakawa wanataka mabadiliko.

Lowassa alisema hayo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari ofisini kwake, akisema yeye na Ukawa walishinda kwa kishindo isipokuwa matokeo yalivurugwa makusudi ili CCM iendelee kubaki madarakani.

Jana, akiwa kwenye mkutano wa tathmini kati ya NEC na asasi za kiraia kuhusu utoaji elimu kwa mpigakura uliofanyika Dodoma, Jaji Lubuva alisema uchaguzi umeshapita na kilichobaki sasa ni kufanya kazi tu.

Bila ya kutaja jina la mwanasiasa huyo, Jaji Lubuva alisema kama kuna mtu alishindwa katika uchaguzi uliopita, ajipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

“Hata wananchi wanawashangaa kwa kuwa wao ndio walioamua ni nani anafaa kuwaongoza,” alisema Jaji Lubuva.

Alisema kuwa NEC ilikuwa inapokea matokeo ya uchaguzi kutoka majimboni na kuyasoma kama yalivyotumwa na katika hilo hakuna wakala hata mmoja wa chama ambaye aliyapinga matokeo hayo.

“Sasa nashangaa kuna baadhi ya wagombea wanaotaka Tume ifukuzwe kazi eti tu kwa sababu wao hawakushinda. Naomba ifahamike kwamba katika kila uchaguzi duniani kuna kushinda na kushindwa.

"Sasa kama kila atakayeshindwa atataka tume ifukuzwe kazi hapatakuwa na tume ya uchaguzi kwa sababu kila atakayekuwa anashindwa atakuwa anataka tume ifukuzwe kazi,” alisema Jaji Lubuva.

Chadema, ambayo iliungana na vyama vitatu kuunda Ukawa, iliitaka NEC kusitisha utangazaji matokeo ikidai kuwa kilichokuwa kikitangazwa ni tofauti na takwimu walizokusanya kutoka majimboni. Lakini NEC ikaendelea kutangaza.

Baadaye, Chadema ililalamika ikidai kituo chao cha kukusanya na kujumlisha matokeo kilivamiwa na polisi na kompyuta kuchukuliwa na hivyo kuvuruga ufuatiliaji wao wa matokeo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa huduma kutoka NEC, Emmanuel Kavishe alisema kuwa Tume inafanya kazi kwa mujibu wa sheria na Katiba na kwamba hata siku moja haijawahi kumpendelea au kumuonea mtu yeyote.

Katika uchaguzi wa urais, John Magufuli alipata kura milioni 8.8 huku Lowassa akipata milioni 6.07.
“Sasa nashangaa kuna baadhi ya wagombea wanaotaka Tume ifukuzwe kazi eti tu kwa sababu wao hawakushinda. Naomba ifahamike kwamba katika kila uchaguzi duniani kuna kushinda na kushindwa"NUKUU YA JAJI LUBUVA.Salam hizi ziwafikie wote wanaohusika popote pale walipo.
 
3. Iweje watu wa Haki za Binadamu na wa CHADEMA wanyang'anywe vifaa vyao wakati wa CCM waliokuwa wanafanya zoezi hilo hilo kwa maudhui hayo hayo waachwe?

Hapo pekundu... Unao uhakika kilichokuwa kinafanywa na timu ya CDM+LHRC pale Double View Hotel Sinza, kwa upande mmoja, na timu ya CCM pale Mlimani City, kwa upande mwingine, ni "zoezi hilo hilo kwa [malengo] hayo hayo"?

Utafiti wangu unaonyesha kwamba kuna tofauti kubwa kati ya kambi hizi mbili. Ninafahamu kwamba timu ya CDM+LHRC ilikuwa na NIA OVU na walishaanza kutekeleza.

Wasingedhibitiwa Taifa hili lingeingia katika umwagaji wa damu mkubwa. Tuache kuficha ukweli bila kuona mdhara ya ukimya wetu. Ukweli utatuweka huru...
 
hili zee vipi nalo,...
liende zake ukooo.,..
limeshiliki kuiba kula linablame nini sasa,...
halina busara kabisa,.
likae kimyaaaaa
shut up mzeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
na liuparra rako kavu
 
Hapo pekundu... Unao uhakika kilichokuwa kinafanywa na timu ya CDM+LHRC pale Double View Hotel Sinza, kwa upande mmoja, na timu ya CCM pale Mlimani City, kwa upande mwingine, ni "zoezi hilo hilo kwa [malengo] hayo hayo"?

Utafiti wangu unaonyesha kwamba kuna tofauti kubwa kati ya kambi hizi mbili. Ninafahamu kwamba timu ya CDM+LHRC ilikuwa na NIA OVU na walishaanza kutekeleza.

Wasingedhibitiwa Taifa hili lingeingia katika umwagaji wa damu mkubwa. Tuache kuficha ukweli bila kuona mdhara ya ukimya wetu. Ukweli utatuweka huru...
1 Nina uhakika

2. Umetumia vigezo gani na viashiria gani huru kufanya huo utafiti wako na kuthibitishwa na nani?

3 Hoja za vitisho si muafaka wakati huu wa utandawazi wakati kila kitu kiko hadharani. Ushahidi ni ile kauli yenu ya taarifa za intelligencia za upande mmoja huku wengine waakati huo huo taarifa za intelligencia zinakuwa haziwahusu.

Kunishawishi naomba niambie mimi na wanaJF wote maendeleo ya kesi inayowakabili CDM+LRHC.

Umedhihirisha upungufu mkubwa wa uwezo wa kutosha wa kutoa mbadala zenye ushahidi zaidi ya kutetea usichokuwa na ushawishi nacho
 
1 Nina uhakika 2. Umetumia vigezo gani na viashiria gani huru kufanya huo utafiti wako na kuthibitishwa na nani? 3 Hoja za vitisho si muafaka wakati huu wa utandawazi wakati kila kitu kiko hadharani. Ushahidi ni ile kauli yenu ya taarifa za intelligencia za upande mmoja huku wengine waakati huo huo taarifa za intelligencia zinakuwa haziwahusu. Kunishawishi naomba niambie mimi na wanaJF wote maendeleo ya kesi inayowakabili CDM+LRHC. Umedhihirisha upungufu mkubwa wa uwezo wa kutosha wa kutoa mbadala zenye ushahidi zaidi ya kutetea usichokuwa na ushawishi nacho

Twende taratibu. Timu ya CDM pale Double view Hotel (Sinza) ilibumba na kusambaza mitandaoni matokeo ya urais kwa Jimbo la Ubungo, etc. Lakini, kwa upande wa Ubungo, hata Kubenea (MB) akiulizwa leo hii aseme kama alijua mgombea urais wake Lowassa alikuwa amepata kura ngapi kabla ya yeye kuondoka kituo cha majumuisho atasema "hapana." Alipewa taarifa baadaye. Kwa hiyo, hana ground ya kufanya refutation. Hali ilikuwa hivyo nchi nzima isipokuwa Arumeru kwa Joshua Nassari pekee!

Pale Ubungo, mara tu baada ya yeye kutangazwa mshindi Kubenea alikimbilia mitaani kusherehekea. Mawakala wake waliondoka naye. So, timu ya Double view ilipata wapi data za Urais Ubungo kama zilivyosambazwa mitandaoni? Forgery tupu!

Yote haya yalitokea kwa sababu kuu ni moja kuu. Kampeni Meneja wa Lowassa, John Mrema, alitakiwa kusambaza fedha za mawakala nchi nzima lakini hakufanya hivyo. Hata fungu la wagombea Ubunge nalo alilizima.

Nakumbuka siku moja saa nne usikupale Mwanza, Lwakatare aliambiwa ajibanze kona fulani kusubiri uwezeshaji kutoka kwa John Mrema, lakini alishtuka ni saa sita usiku na Mrema haonekani wala kupatikana kwenye simu. Hali ilikuwa hivyo nchi nzima. Tuachane na "usanii wa kura ziliibiwa." Tufanye post-mortem na kutambua majipu yalipo ili yatumbuliwe. Vinginevyo tunapinga ngoma majini...

Kwa ufupi Lowassa alitapeliwa na campaign team yake. Anapaswa kuufahamu ukweli huu hata kama ni mchungu.

Inatosha kwa leo. Sitaki kuendelea nikaongelea kuhusu wale vijana kutoka Israeli, Ufaransa na China...
 
Back
Top Bottom