Lowassa: Wakining'oa NEC nitaeleza ukweli kuhusu Richmond

Wakati makundi mawili hasimu yale yanayomuunga na kutomuunga Lowassa yakitunishiana misuli kuhusu kuvuliwa gamba kwa kutumia kashfa ya richmond, lowassa amenukuliwa na watu wake wa karibu akisema huu utakuwa wakati mwafaka kwake kusema kila ukweli anaoujua kuhusu richmond.

Chanzo: Tanzania Daima
Kumbe hiki ndicho chanzo cha habari yako!! Ngoja nipite tu!:closed_2:
 
ugumu wa roho yake hauna maana ktk nchi hii. hatuhitaji watu wenye roho ngumu ktk kuliharibu taifa badala yake tunawahitaji watu wa aina hiyo ktk kutetea na kuiendeleza nchi hii kutoka ktk lindi la umasikini wa kipato na akili ambao umetamalaki miongoni mwa watz wengi mijini na vijijini
 
Royals umeongea kuna kitu bana otherwise wangemshinikiza, jamaa kashika pabaya mchezo umechezwa ila yeye amejitoa muhanga kwa niaba
 
Wakati makundi mawili hasimu yale yanayomuunga na kutomuunga Lowassa yakitunishiana misuli kuhusu kuvuliwa gamba kwa kutumia kashfa ya richmond, lowassa amenukuliwa na watu wake wa karibu akisema huu utakuwa wakati mwafaka kwake kusema kila ukweli anaoujua kuhusu richmond.

Chanzo: Tanzania Daima

Kabla ya kusema ukweli wake na baadaye kuwa rais??? ni bora kwanza ukamshauri akamjibu swali lake lililomshinda la yule mtoto wa Mwanza aliyemuuliza kwanini wazee hawaachii ngazi serikalini kupisha vijana?
 
Ndicho nilichowambia Mkandara hicho,EL kashikilia kwenye kamali...Kutachimbika kama ni kweli,trust me!

Mwakyembe around or not,someone still holds the wild cards.

Kumbuka kulikuwepo na ripoti mbili na Mwakyembe aliitoa ile ya kumchafua EL...

EL alisema wakimwaga mboga yeye atamwaga ugali. Aliahidi wakimuvua gamba yeye atawaonyesha watanzania mahali alipo BALALI. Hii ndio mimi naisubiri kwa hamu.
 
Wakati makundi mawili hasimu yale yanayomuunga na kutomuunga Lowassa yakitunishiana misuli kuhusu kuvuliwa gamba kwa kutumia kashfa ya richmond, lowassa amenukuliwa na watu wake wa karibu akisema huu utakuwa wakati mwafaka kwake kusema kila ukweli anaoujua kuhusu richmond.

Chanzo: Tanzania Daima
Mwizi na Mpuuzi kabisa huyo Mzee,kwanini hakusema kipindi kile alichojiuzulu aje aseme leo?Hakuna mtu mwenye imani nae,kama ni bingwa wa kujisafisha basi akajisafishe kwanza PEPONI ndo tutamuona mkweli na amedhamiria.Otherwise NO.
 
EL wanakuonea sasa tekeleza lile uliloahidi kwamba wakikuchezea tu, hatafanya ajizi, utatuonyesha mahali walipomficha BALALI
 
Kama habari hii ni kweli basi tunaelewa yafuatayo;
Lowasa hafai kabisa kuwa kiongozi kwa vile sio mkweli na hapiganii haki ya raia. Pia rafiki yake ambaye ndiye Raisi sio mzalendo maana pamoja na katiba kumlinda maisha yake yote baada ya kipindi chake cha uraisi ni mtu mwenye tamaa na mwizi wa rasilimali alizoapa kuzilinda.
 
utatuonyesha mahali walipomficha BALALI

Hili sio la msingi kwa watanzania kama anajua haya na amekaa kimya kwasababu anafaidikia basi huyu sio mtu sio wa kuaminika hata kidogo, anategemea sympathy ya watanzania kwa ajili ya utukufu wake na sio kusaidia Tanzania..Heri akimwagwa aendelee na shughuli zake kimyakimya..
 
Hivi kumbe kuna binadamu wamechanganyikiwa kabisahivi unawezaje kuanza kushawishi watu eti EL ni msafi na unasema amekomaa kisiasa,kama una maslahi naye huna sababu ya kuwaonyesha wengine,kula hizo mia mbili miambili kisha kaa kimya,au ujira wako unatokana na kuingia jamnvini na kuandika andika uppuzi?hivi kweli unawezaje kunisadikisha niseme jamaa ni mwadilifu na msafi sana wala hajawahi kufanya shambulio la kimbali kwa kupora rasilimali za taifa hili,hajawahi kusababisha vifo vya kina mama wajawazito,hajawahi kusababisha watoto kukaaa chini kwenye vumbi na sakafu bila madawati,hajawahi kusabisha watu kukoa maji safi na salama,hajawahi kupora kiujanja ujanja jasho la mwananchi masikini kwa kujipatia fedha hizo kwa hila?Hivi si huyu huyu Richard Monduli au ?NO WAY mimi sidanganyiki ki rahisi hivyo naomba na watanzania wengine tusikubali kuongepewa.Kama anataka tumpime kwa uwazi basi ayaseme yote aloifanyia nchi hii ambayo ni ufisdai bila kujali alishirikiana na nani ayaseme wazi yote tarehe kwa siku na mwaka na wale alioshirikiana nao,hapo anaweza kusamehewa na kisha kumuomba akapumnzike kwake monduli,lakini bila hivyo bado sana
 
Lowasa apigwe chini hana lolote kama ana siri nzito kwanini hakuitoa kabla anapigwa chini ndio anatishia nyau
 
EL alisema wakimwaga mboga yeye atamwaga ugali. Aliahidi wakimuvua gamba yeye atawaonyesha watanzania mahali alipo BALALI. Hii ndio mimi naisubiri kwa hamu.

Jamani Balali si amefariki au????????????????????????????????????
 
Kama hii ni kweli basi huyu jamaa anazidi kuonyesha jinsi asivyostahili kuwa Rais wa nchi yetu 2015. Yaani kuna madudu yalifanyika kuhusiana na mkataba wa Richmond/Dowans naye anayajua lakini kaamua kutuficha Watanzania miaka yote hii.

Sasa anaona maslahi yake yanataka kuharibika ndio anataka kutueleza nini kilichojiri!!!! Mwalimu aliona mbali sana pale aliposema huyu jamaa hastahili kabisa kuwa Rais wa nchi yetu.

Aliyaficha for the sake of nationa security sasa wenzake wanamfukuza ili wayaendelezee kwa kasi zaidi, ari zaid na nguvu zaidi weka hadharani lowassa with or without you nchi imesha amua kulianzisha
 
He kumbe lowassa anamjua aliye muua nyerere na ushahidi wa picha, sauti na mikanda, what else do you know mr lowassa, heee maskini kumbe alitakiwa afe kabla ya uchaguzi wa 2005
 
katika logic yakawaida, kwa anayoyataka Lowassa lazima aseme hivyo ili aonekane msafi, yani hahusiki na richmond
 
Back
Top Bottom