The Infamous
JF-Expert Member
- May 11, 2009
- 731
- 121
wakati wa mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2005, nakumbuka kila mtanzania alikua anakereka na kustaajabika kuwa aliyekuwa waziri mkuu wa serikali ya ccm 1995-2005 mh frederick sumaye alikua anataka kugombea urais kwa kupitia ticket ya ccm.
Mapungufu yake mengi tuliyaona na kuyajua, tuhuma kubwa zikiwa alikuwa akichukua mashamba ya watu kwa nguvu au kwa njia ambazo hazikua halali [these were mere allegations].pia na hela alizotumia wakati wa safari moja alienda marekani naomba mnisaidie kwa kumbukumbu nzuri.
Upande mwingine alichomoza el, ambapo ni kama watanzania tulijisahau sijui au ah? Au ndo ujinga wetu?, maana ni kama alionekana ni mtu msafi kwa mda wa kipindi kile cha mchakato wa uchaguzi 2005. Watu wote tulijua kuwa atakuja kuwa waziri mkuu lakini wachache tuliohoji umakini wake na utendaji wake kazi, hususan tukikumbuka el alikataliwa na alikuwa hakubaliki na mw nyerere kwa kuwa na utajiri mkubwa pasipo kawaida.
Wakati ule [2005] ulikua ukiwalinganisha el na fs ni kama lowasa ali edge ahead, na honestly media ilikua sana against fs.
Sasa tunajua a-q if not z ya el, je kuna ya fs ambayo hatuyajui ambayo yana uzito unao fanana na el au kumzidi.
Tukipima mizani yao nani kamzidi mwenzake mpaka sasa kwa ufisadi?
Nani anaweza ku-come back au anaweza kuwa the come back king, maana najua wote wana hamu ya kuingia kwenye uwanja wa siasa ila maji yamewazidi shingo...
hivi tanzania hii hatuna viongozi wengine zaidi ya lowasa na sumaye mpaka tufikirie come back yao, wao wamepita na mda wao umekwisha waje wengine afterall wote wanakashfa kibao ya nini kuwafikiria, warudi vijijini kwao wakalee familia na kulima.