Lowassa vs Sumaye

Semenya

JF-Expert Member
Sep 5, 2009
572
51
wakati wa mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2005, nakumbuka kila mtanzania alikua anakereka na kustaajabika kuwa aliyekuwa waziri mkuu wa serikali ya CCM 1995-2005 Mh Frederick Sumaye alikua anataka kugombea urais kwa kupitia ticket ya CCM.

Mapungufu yake mengi tuliyaona na kuyajua, tuhuma kubwa zikiwa alikuwa akichukua mashamba ya watu kwa nguvu au kwa njia ambazo hazikua halali [These were mere allegations].Pia na hela alizotumia wakati wa safari moja alienda marekani naomba mnisaidie kwa kumbukumbu nzuri.

Upande mwingine alichomoza EL, ambapo ni kama watanzania tulijisahau sijui au ah? au ndo ujinga wetu?, maana ni kama alionekana ni mtu msafi kwa mda wa kipindi kile cha mchakato wa uchaguzi 2005. Watu wote tulijua kuwa atakuja kuwa waziri mkuu lakini wachache tuliohoji umakini wake na utendaji wake kazi, hususan tukikumbuka EL alikataliwa na alikuwa hakubaliki na Mw Nyerere kwa kuwa na utajiri mkubwa pasipo kawaida.

wakati ule [2005] ulikua ukiwalinganisha EL na FS ni kama lowasa ali edge ahead, na honestly media ilikua sana against FS.

sasa tunajua A-Q if not Z ya EL, je kuna ya FS ambayo hatuyajui ambayo yana uzito unao fanana na EL au kumzidi.

Tukipima mizani yao nani kamzidi mwenzake mpaka sasa kwa ufisadi?

Nani anaweza ku-come back au anaweza kuwa the come back king, maana najua wote wana hamu ya kuingia kwenye uwanja wa siasa ila maji yamewazidi shingo...
 
Kwangu mie naona hakuna mwenye unafuu maana ingekuwa twatumia Quran kuwaelezea basi tungesema wote ni haramu maana hakuna cha nguruwe mdogo wala mkubwa kama ni nguruwe ni nguruwe tu. Sijui huyu kachafuka kidogo au sana hayo ni maneno ya kujifariji tu. Kuku ni Kuku Jogoo ni jina tu.

Wakubwa Allah awe nanyi.
 
lowasa alitumia mchezo mchafu wa kumchafua mwenzake ikaonekana kama yeye msafi vile,
 
I hate badly the two of them! Wote wana makosa yao makubwa na ya kiufundi ambayo hayavumiliki, ukiwemo ufisadi na ubabe madarakani!
 
hiyo ya ubabe wote wamejaaliwa kuwa nao, na hawana tabia ya kufuata utawala bora
 
Pinda ndo safi maana yeye si fisadina anatuonea donge tunaovaa suti zetu kwa kuwa nchi hii ni masikini hivyo tuvae mashati ya batiki
 
Semenya,

..Sumaye ana afadhali kubwa sana kuliko Lowassa.

..off course alikuwa na mapungufu yake, lakini vilevile magazeti ya Lowassa na JK yalikuwa yakimwandama tangu ateuliwe Waziri Mkuu kwa muda wa miaka 9 .

..tangu aondoke madarakani ameshinda kesi ya madai dhidi ya gazeti lililoandika habari za uongo na kashfa dhidi yake.

..Tanzania tunahitaji kiongozi mwenye upeo na uelewa wa mambo kuliko Frederick Sumaye. lakini ukinishikia bastola na kuniambia nichague kati ya Lowassa na Sumaye, kwa kweli nitalazimika kumchagua Sumaye.

NB:

..mnakumbuka Sumaye na Dr.Idris Rashid walivyochukua mikopo toka PPF wakati Mataka akiwa DG? magazeti ya wanamtandao yaliandika suala lile kama kashfa na kuwa Sumaye hafai kuwa waziri mkuu. sasa mbona leo mtandao haohao wamewapa nyadhifa nzito Dr.Rashidi na Mataka?
 
Mkuu huna haja ya kushikiwa bastola wala fimbo. Kwa ufisadi na siasa chafu, Sumaye na Lowasa ni kama giza na mwanga ama mbingu na dunia. Kama FS angekuwa fisadi kama EL, na jinsi alivyoandamwa na vyombo vya habari, lazima EL angemsihi swahiba wake JK wamtie ndani!
 
Nikipata proof ya ufisadi wa Sumaye nitamchukia, TRA wana slogan kuwa Sumaye angekuwa fisadi basi kipindi kile angekula hela za kodi mpaka basi.

Ukweli ni kuwa JK na EL walitumia mchezo mbaya kuwachafua akina Sumaye, na watanzania wengi tukaingia king,

Leo ukiwauliza watz wengi ufisadi wa Sumaye sio kuwa wamesahau, bali hawajui, ni kama vile ule upepo wa JK chaguo la Mungu, ni tumain jipya n.k

Sumaye is far better than EL,however he may not qualify to be PM even today so as Pinda!
 
Semenya,

..Sumaye ana afadhali kubwa sana kuliko Lowassa.

..off course alikuwa na mapungufu yake, lakini vilevile magazeti ya Lowassa na JK yalikuwa yakimwandama tangu ateuliwe Waziri Mkuu kwa muda wa miaka 9 .

..tangu aondoke madarakani ameshinda kesi ya madai dhidi ya gazeti lililoandika habari za uongo na kashfa dhidi yake.

..Tanzania tunahitaji kiongozi mwenye upeo na uelewa wa mambo kuliko Frederick Sumaye. lakini ukinishikia bastola na kuniambia nichague kati ya Lowassa na Sumaye, kwa kweli nitalazimika kumchagua Sumaye.

NB:

..mnakumbuka Sumaye na Dr.Idris Rashid walivyochukua mikopo toka PPF wakati Mataka akiwa DG? magazeti ya wanamtandao yaliandika suala lile kama kashfa na kuwa Sumaye hafai kuwa waziri mkuu. sasa mbona leo mtandao haohao wamewapa nyadhifa nzito Dr.Rashidi na Mataka?

Umenena mkuu,mwenye ushahidi tosha wa ufisadi wa Sumaye , kama upo, autoe hadharani.
 
Umenena mkuu,mwenye ushahidi tosha wa ufisadi wa Sumaye , kama upo, autoe hadharani.
Linganisha tu MALI alizokuwa nazo FTS kabla hajawa WM na miaka kumi baada "kustaafu" UWM. Staili alootumia Sumaye na wanasiasa wengine wengi tu akiwemo EL ni ngumu sana kuitolea ushahidi hapa lakini kama umewahi kuwa mwajiriwa wa TAASISI yoyote ya UMMA utakuwa unaelewa mabilioni ya taasisi hizi yanavyotafunwa na MAWAZIRI, MANAIBU WAO kupitia tenda hewa nyingi na over pricing ya bidhaa na huduma kwenye taasisi hizi.
 
mimi nilikua najiuliza sana 2005, Maana EL ilikuwa inajulikana wazi kuwa ni fisadi papa toka zamani sijui hali ile iligeuzwaje bwana, ikaonekana kama sumaye ni fisadi kuliko hata EL...na mpaka sasa sijapata ufisadi wa FS.....
 
Kweli kabisa sumu ya mende ni nafuu kuliko sumu ya nyoka, lakini zote ni sumu zinazoua. Watanzania wa sasa sio kama wa zama zile, ambapo maschool mates walikuwa wachache wasomi na walikumbukana kutokana na uprefect wa enzi zao.

Kwa sasa mtu aonekane mkweli na mwoga kuchezea mali ya umma, tena ajisikie vibaya kuona wananchi wake wanateseka ilhali sio lazima wateseke kiasi hicho kwa hali ilivyokaa.

Bora kuwa na mizengwe upite na kupinda, maana mateso ya wananchi yanakutoa machozi hadharani. Hata kama ni kuigiza wakikuangalia usoni washindwe kuelewa kama ni kweli au ni maigizo.

Leka
 
tatizo udikteta ukiingia ndo hivyo watuwatakua wanazipiga mpaka mwisho
 
Back
Top Bottom