Lowassa vs MwanaHalisi

........Peter selukamba anena!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Akili yako ni fupi unaishia kusema nani kasema na siyo nini kimesemwa...hio ni moja ya dalili ya uwezo mdogo wa akili.Serukamba huwezi kufanana nae hata kidogo....ana historia kwenye siasa ya Tanzania ambayo mtu kama wewe huwezi kufanya:
1.Alivunja nguvu ya Chadema kigoma
2.Alimdondosha DR Kaburu mpaka akafanya ajiunge na CCM
3.Mkristu wa kwanza kukubalika ndani ya himaya za ujiji na mwanga
4.Kashinda uchaguzi kigoma mara mbili
5.Kashinda kigoma pamoja na nguvu zote zilizotumika dhidi yake ambazo ni halali na haramu
Pamoja na mambo yote kati yetu nabaki kumuheshimu kama mwanasiasa bora na anaesimamia anachokiamini
 
kwa kuwa umetumwa kuja kuwasafisha watu kupitia forum hii, hata kwa kukatwa kichwa bado utaendelea kuita richmond, epa nk upupu. basi kazi yako inaifanya vizuri. Plato aliwahi sema "Wise men talk because they have something to say; fools, because they have to say something"
 
kwa kuwa umetumwa kuja kuwasafisha watu kupitia forum hii, hata kwa kukatwa kichwa bado utaendelea kuita richmond, epa nk upupu. basi kazi yako inaifanya vizuri. Plato aliwahi sema "Wise men talk because they have something to say; fools, because they have to say something"
Maneno yako yamegusa wengi. Pamoja na kuwa naamini aliyoyasame Nchimbi,J hakutumwa na Emmanuel Nchimbi, naamini pia hakutumwa maana hata Lowassa na Rostam wenyewe wanajijua kuwa ni mafisadi na wanajijua kuwa wameifikisha nchi hapa ilipo. Ni udhaifu na upofu kusema Lowassa alifanya mema na ni upofu kusifia ufisadi wa EPA (Kagoda) Richmond, Dowans kwa kisingizio cha madawati na udhamini wa ligi na Miss Yanzania. Kwanza usihusishe Vodacom (hata kama Ra ana share) na maovu ya kifisadi, hutawatendea haki wawekezaji wengine wa Vodacom. J.Nchimbi nakuaminia sana lakini kwa holi umetumbukia shimoni na naamini soon utajutia umri wako bado unahitaji kusonga mbele na si kutetea waovu. Angalia future yako kisiasa na kitaaluma ambayo haiwezi kubebwa na Lowassa na RA, wakati wao umepita hata kama unaamini walifanya vyema, ni bora ukampigia deba Emmanuel Nchimbi na hata huyo Serukamba (japo naye hasimami kama yeye) ambao ni vijana na bado wana nafasi ya kusonga mbele.
 
Ufisadi in the true meaning of the term haumaanishi kuwa lowasa ndio kiiiivyo, hebu tuwe wakweli jamani inamaana ufisadi wa nchi hii unawakilishwa na lowasa? Mbona hata sumaye alifikia hatua ya watu kumuona kama kinyesi 2000-2005? Ufisadi wake umeenda wapi? Inamaana kagoda,iptl,ttcl,loliondo gate,mchuchuma,epa,deep green,trc,uuzwaji wa nbc,mikataba mibovu,atcl,nssf-pspf scandals,sugar scandle,mishahara feki..................................zote hizi ni lowasa tuuuuuuuuuu? Anyway,kwa kuwa siasa zetu na uchambuzi wetu ni fuata mkumbo,haiko mbaya,lakini hebu tufanye tafakuri upya,mbona lowasa tu ndo zaidi na si kikwete,mkapa na wengine??? Uraisi kazi kwelikweli-just thinking aloud." fiat justitia.luat caelum"-let justice be done though heavens fall,
Naomba ufikirie kidogo tu. Kwanza uko sahihi kwamba urais ndio sababu, lakini unakosea kuona kama ni sababu ya kijinga maana unakua kipofu kuona kwamba urais ni kitu kidogo. Hivi kweli unataka tuache mtu mwenye nguvu ya kisiasa ambaye ni fisadi aje kutawala? Baada ya 2015 Lowassa hatakua issue ya nmagazeti atakua issue ya Rais ajaye kumburuza mahakamani
 
Mimi naona Huwa habari inanoga watu wanaoandikwa wakiwa Public Figures, kama wamechoka kuandikwa naomba wachague Moja, Yaani kuachana na siasa na kujihuzulu hadi Ubunge kwani kwa hivyo watakuwa hawana Mshiko kwenye Habari!! Ila kama bado wanang'ang'ania kuwa viongozi wa Umma hayo hayaepukiki!! Hivyo waliokutuma waambie wamechelewa!!
 
Mwanahalisi kiboko ndio lilonfanya niwepo hapa mimi. Kwa hivyo ondoa pumba yako hapa
Ha ha ha Kwa mara ya kwanza nimejikuta ndani ya kibanda kimoja na Malaria Sugu, Hii ni ajabu sana. Big up Mwana Halisi kwa kutuunganisha japo kwa dakika chache. Twanga kotekote, waasisi wa CCJ na Mafisadi
 
Nape hawezi kunituma mimi hata siku moja hata yeye anajua hilo.......simkubali na wala hatupatani hata yeye anajua hilo.
mlikwaruzana kwenye mbio za Ubungo nini Mkuu? Hata hivyo ni kiongozi wako kuna siku atakutuma tu labda kama hupo CCM hiyo ya Nape
 
Kwanza si kweli kwamba kila mwezi mwanahalisi lazima wamwandike Lowasa na Rostam. Umejisahau kwamba gazeti la Mwanahalisi ni Weekly hivyo linatoka sana sana mara nne tu kila mwezi na kuna matoleo yanayotoka na kuambatana pasipo kuwataja hao jamaa waliokuajiri (Sijui kama umemaliza Probation).
Mtatumia mbinu nyingi sana kumtafutia ulaji tena Lowasa lakini nakwambia kama mnakula pesa za huyu jamaa mjue kwa mara nyingine yatawatokea puani. JK anaburunda halafu anaziba masikio mnapolalamika. I tell you kwa ukali wa Lowasa kula atakula na mkithubutu kusema mtakiona.
 
Jenga hoja zako na sio umbeya hapa.....mi mi nasema kuwa uwekezaji uliofanywa na Rostam ndani ya tanzania ni muhimu kuliko hata haya majungu mnayoleta hapa.....mna laana nyinyi watu.
1.Kaleta dowans ambayo iliwapa offer ya umeme wa chini kuliko kampuni yeyote binafsi inayozalisha umeme kusini mwa jangwa la sahara.
2.Kaleta gazeti la mwananchi ambalo ndio gazeti bora tanzania katika ujenzi wa demokrrasia.
3.Anadhamini ligi ya vodacom
4.anadhamini miss tanzania
5,Analipa kodi zaidi ya bilioni 40 kwa mwaka
6.Katoa ajira kwa zaidi ya watanzania elfu tatu
7.Kajenga madarasa na kugawa madawati kwa zaidi ya shule mia tano nchini
Labda ajala chakula na walemavu tu
Nimepapenda sana hapa. Sasa Kikwete aliposema haijui Dowans alikuwa anamdanganya nani? Ndio maana Kubenea ataendelea kusomwa tena na tena
 
Si kweli kuwa kuna mambo mengi ambayo yanaibuliwa kama ambavyo unataka kuonyesha hapa.....zaidi ya kuongelea upupu wa richmond na epa ambayo yameteeokea miaka 4 iliopita kuna nini jingine la ziada zaidi ya majungu.
we timamu kweli au kichaa? Kwa taarifa yako ili gazet linaandika ishu mpya kila wiki tena adimu zinazowakela magamba hadi mkwer.e himself kwan mfano headlines wiki hii LOWASA,ROSTAM KUMZIMA KIKWETE hii haiusiani na richmond, nyingine CCM WAPANGA KUHUJUMU CHADEMA, pia kuna habari hoayoiusu CUF,acha utovu wa nidhamu ongelea unayoyajua yale ya mzalendo,uhuru na jambo leo sio mwanaHALISI
 
Jenga hoja zako na sio umbeya hapa.....mi mi nasema kuwa uwekezaji uliofanywa na Rostam ndani ya tanzania ni muhimu kuliko hata haya majungu mnayoleta hapa.....mna laana nyinyi watu.1.Kaleta dowans ambayo iliwapa offer ya umeme wa chini kuliko kampuni yeyote binafsi inayozalisha umeme kusini mwa jangwa la sahara.2.Kaleta gazeti la mwananchi ambalo ndio gazeti bora tanzania katika ujenzi wa demokrrasia.3.Anadhamini ligi ya vodacom4.anadhamini miss tanzania5,Analipa kodi zaidi ya bilioni 40 kwa mwaka6.Katoa ajira kwa zaidi ya watanzania elfu tatu7.Kajenga madarasa na kugawa madawati kwa zaidi ya shule mia tano nchiniLabda ajala chakula na walemavu tu
we sio bule unatatzo,analipa kod bil 40 na anatuibia ngapi?
 
Wadau juz j'5 nilikua naenda kijijin huko mida ya jioni, ndani ya hiace abiria 14 kwa kuwahesabu mwenyewe wote walikua na gazeti la Mwanahalisi mkononi na kila mmoja alikua anashuka kijiji chake njiani njiani huko. nikajaribu kumhoji abiria wa pembeni yangu akaniambia hao ni walim wa msingi pamoja na wakulima huko vijijini ni wasomaji wazur wa hilo gazeti na mara lifikapo kijijini husoma na kuazimwa kwa wengine kwa maana ya kwamba husomwa karibia na kijiji chote, Sifa kuu ya mwanahalisi jamaa ameniambia kuwa ni habari zake za ukweli na uchunguzi makini na kupinga ufisadi unaowatesa wa Tz.
Niliposikia hayo NIKASEMA UKOMBOZI UNAKARIBIA.
BiG UP Kubenea na timu nzima.
SASA HAWA WANAODAI NI GAZETI LA UDAKU HIYO SI KWELI. Waache Akili za Kigamba gamba.
 
Poor you mtoto wa fisadi. There is something called 'journalism freedom and credibility' Lowassa, kikwete, au Rostam no differences here. Ukifanya uhujumu wa Taifa tutakuandika na this is our justice system. Tunajua usalama wa taifa, prosecutor office na ffu Tanzania kazi yao ni kuwaandama na kuwaweka jela chadema na hasa Mbowe na Dr Slaa. This is how we will prosecute criminals, by hang them on journalism and social media until we get True Constitution and Equal rights in Tanzania. Sorry for feel lonely and selfish.

We will not stop.


Nimeangalia kwa makini sana gazeti la Mwanahalisi kwa zaidi ya miaka mitatu mfululizo bila kukosa na leo nasema kwamba Mwanahalisi ni gazeti maalumu lililoundwa kwa ajili ya kumshughulikia Edward Lowasa na Rostam Aziz.Siku ambayo hawa watu wawili hawatakuwepo basi na gazeti letu kipenzi litakuwa limekufa pia.Leo niko tayari kupinga na mtu yeyote kuwa “KAMA MWANAHALISI LIKIKAA MWEZI MMOJA TU HALIJAANDIKA HABARI YA LOWASA BASI NITATOA KWA NILIOPINGA NAE SHILINGI MILIONI MOJA” japo ni hela nyingi kwangu ila nina uhakika haziwezi kunitoka kw kuwa Mwanahalisi wanamuota mchana na usiku Edward Lowasa……….Kwa kweli Lowasa ni mvumilivu sana ningekuwa mie ningekuwa nimeshafungwa jela kwa kumshughulikia mtu mbaya kabisa ,siwezi kuchezewa namna hii.:angry:
 
Wakuu naona kama kuna watu ambao wamewekwa maalum kwa ajili ya kupoteza au kumaliza umaarafu/umakini/target halisi ya blog yetu ya JF.wanajua kabisa kwamba watu wengi(nje na ndani ya nchi) wawe ni raia au sio raia wa Tanzania huwa wanapata ukweli wa hali halisi ya mambo yanayotokea Tanzania.Pia hawa watu wanaweza kutoa misimamo yao kuhusu Tanzania kwa kupata habari kupitia hapa JF.Before kuvunjwa kwa kamati kuu ya CCM kila kitu kilikuwa ok kama kawaida hapa JF lakini baada ya kuteuliwa uongozi mpya CCM na kujaribu kuunda kamati ya kutathmini sababu za CCM kupoteza muonekano,moja ya sababu za hiyo kamati ilikuwa ni blog ya JF.wamediriki mpaka kudanganya kuwa JF ni mali ya CDM.ukweli wa mambo kuhusu JF unajulikana na hata CCM wanaujua vizuri kabisa ila wanakataa kuukubali kwasababu ya zao wenyewe.sasa viongozi wapya wa CCM wameamua kutuharibia maana na lengo halisi la JF.nasema hivyo kwasababu baada ya kuisoma hii mada iliyotolewa na huyu jamaa( a.k.a Nchimbi J) nakubaliana kabisa na mawazo yangu ya awali kuwa kuna nia mahsusi ya kumaliza interest ya watu kuingia JF kwa wao kupandikiza watu ambao hutoa mada za kizushi/ kimajungu/ kichochezi/kifitina/ kipelelezi au za kutengeneza ambazo zitaharibu au kupoteza interest ya watu kuangalia JF.Hapa jamvini tumezoea kusoma mawazo au misimamo ya baadhi ya viongozi wa serekali au wa upinzani kwenye mada ambazo zimekuwa zinawagusa wao au vyama vyao kwasababu JF imekuwa ni sehemu ambayo watu wenye itikadi mbalimbali za kisiasa/kidini kutoka ndani na nje ya nchi wamekuwa wanatoa au kuchangia mada na kuamini kwamba wada zao zitawafikia watu wengi zaidi especially walioko nje ya nchi.sasa kwasababu CCM ni chama/taasisi isiyo na mwelekeo au administration imeamua kutatua au atleast kuonekana wanafanya kazi kwa kuingiza watu wajinga hapa JF.ni tricks za kijinga mno ila zitakuwa na madhara makubwa baada ya muda kwasababu members wengi ambao wamekuwa wanachangia na kutoka mada hapa JF wataacha baada ya kuona hoja nyingi zinazotolewa au kuongelewa hapa hazina maana.Mfano mmoja ni magazeti ya UHURU na MZALENDO.watu waliacha kununua yale magazeti baada ya kuona kwamba hayakuwa yanaandika issues za maana.sasa members wote wenye nia njema na JF naomba tusaidiane namna ya kuwatambua na kuwasuta au kuwaignore hawa vibaraka ambao wametumwa kujaribu kuharibu maana halisi ya JF blog.wamekuwa mashuhuri sana pia kwenye kutoa mada nyingi ili kuwafanya watu wawe busy au kuchoka.Mod naomba mawazo yako pia.Be blessed!
 
hello r u from magamba family?
kumbuka Kubenea ashawah kutaka kuuwawa au nawe ulishiriki? Kwan tetes zilizopo ni kuwa jamaa alihusika ktj issue nzima.usijaribu kupaka rangi upepo,aliyeanza kumdili ni Mwalimu Nyerere,mwanahalisi ni mwendelezo wa kazi ya Nyerere.usitumike kwa manufaa ya ndoto za mtu mbinafsi na asokuwa na chembe ya huruma kwa masikin wa Tanzania.aliwaumiza watanzania kwa kulipwa sh mil 152 kila siku ktk ya umasikin huu.jaman acha mwiz apigiwe kelele hadi intellegensia wamkamate.akikamatwa mwanahalis halitamwandika tena.
 
Maneno yako yamegusa wengi. Pamoja na kuwa naamini aliyoyasame Nchimbi,J hakutumwa na Emmanuel Nchimbi, naamini pia hakutumwa maana hata Lowassa na Rostam wenyewe wanajijua kuwa ni mafisadi na wanajijua kuwa wameifikisha nchi hapa ilipo. Ni udhaifu na upofu kusema Lowassa alifanya mema na ni upofu kusifia ufisadi wa EPA (Kagoda) Richmond, Dowans kwa kisingizio cha madawati na udhamini wa ligi na Miss Yanzania. Kwanza usihusishe Vodacom (hata kama Ra ana share) na maovu ya kifisadi, hutawatendea haki wawekezaji wengine wa Vodacom. J.Nchimbi nakuaminia sana lakini kwa holi umetumbukia shimoni na naamini soon utajutia umri wako bado unahitaji kusonga mbele na si kutetea waovu. Angalia future yako kisiasa na kitaaluma ambayo haiwezi kubebwa na Lowassa na RA, wakati wao umepita hata kama unaamini walifanya vyema, ni bora ukampigia deba Emmanuel Nchimbi na hata huyo Serukamba (japo naye hasimami kama yeye) ambao ni vijana na bado wana nafasi ya kusonga mbele.
Kwanza niweke rekod vema kuwa mimi situmwi na mtu yeyote na wala sijasema nawakilisha mawazo ya mtu hapa.........ni mawazo yangu na akili yangu.wewe unaona dowans ni ufisadi ni sawa mimi naona dowans ni ukombozi kwa kuwa wameleta umeme na umeme wao wlikuwa wakiuza bei rahisi kuliko iptl,songas na aggreko.hapa ndio nataka tuanzie kubisha kuwa tunataka hata kama watu wachini walikosea lakini ktk makosa yao wakaleta umeme kwa bei ya chini ndio wanakuwa maadui wetu wa maisha au ni yule ambae anatuuzia umeme wa megawts 80 kwa sh mil mia sita kwa siku na bado mko kimya.........kweli huu ni unafiki wa ajabu sana.usipotoshe sijaongelea vodacom hapa.mimi sina haja ya kuwa mwanasiasa kwa kuwa mnafiki na kutokuwa mkweli kama unavyotaka kuonyesha hapa
 
mlikwaruzana kwenye mbio za Ubungo nini Mkuu? Hata hivyo ni kiongozi wako kuna siku atakutuma tu labda kama hupo CCM hiyo ya Nape
hapana sijawahi kugombea ubunge na wala nafasi yeyote ndani ya CCM kama chama.ni vile tu kuwa uwezo wa nape ni mdogo kwa nafasi aliyonayo.
 
Kwanza niweke rekod vema kuwa mimi situmwi na mtu yeyote na wala sijasema nawakilisha mawazo ya mtu hapa.........ni mawazo yangu na akili yangu.wewe unaona dowans ni ufisadi ni sawa mimi naona dowans ni ukombozi kwa kuwa wameleta umeme na umeme wao wlikuwa wakiuza bei rahisi kuliko iptl,songas na aggreko.hapa ndio nataka tuanzie kubisha kuwa tunataka hata kama watu wachini walikosea lakini ktk makosa yao wakaleta umeme kwa bei ya chini ndio wanakuwa maadui wetu wa maisha au ni yule ambae anatuuzia umeme wa megawts 80 kwa sh mil mia sita kwa siku na bado mko kimya.........kweli huu ni unafiki wa ajabu sana.usipotoshe sijaongelea vodacom hapa.mimi sina haja ya kuwa mwanasiasa kwa kuwa mnafiki na kutokuwa mkweli kama unavyotaka kuonyesha hapa

- Duh! Lahaulaa!

William @ NYC, USA.
 
Back
Top Bottom