Lowassa to strike back ; Mbowe to quit chairmanship?

Wajamani EL sio mjinga kiasi hicho mpaka aje ampinge JK 2010. Huu ni ukweli.

Ila for sure kama Mungu akitupa/akampa uhai EL ataingia ulingoni 2015.
 
Aliyewagonganisha jk na el alitumia ziara za el kwa nchi nzima, impact ya ile ziara ya kwanza kama kiranja mkuu ndiyo wasanii wakaifanyia kazi na kum spin, nasisitiza sana kuwa muungwana jk amegombanishwa na el na maadui wa lowasa waliomuona ni ganzi ya kumfikia jk. Sidhani kama ile principal " in politcs hakuna permanent friendship /uadui -kinachodumu ni masalahi" imesahaulika kwa hasa kwa jk, lowasa ktk hali hiyohiyo anapaswa kuiangalia kwa hekima sana principal hii.

Malecela is too smart ktk hilo na ni wazi 2010-mtera anayo tena
 
Mahali tulikofikia TZ katika medani ya uongozi tunahitaji kumsikia EL anasemaje, maana mujngwa amekaa kimya mno. Uwongo ukiongewa muda mrefu bila kukanushwa unageuka kuwa ukweli. Mpaka sasa EL amesema hakufanya kosa lolote katika Richmond bali alijizuru kuiokoa serikali. JK anasema hausiki. Karamagi anasema hausiki na ndiyo maana hapelekwi mahakamani.

Kiutawala ni heri ya shujaa aliyekufa kuliko mwoga anayeishi. EL has better chances as we go foward kwa sababu ya vaccuum ya uongozi.
Na Lowassa hajajitokeza hadharani kusema kuwa ahusiki kwa sababu hana jambo lolote ambalo anaweza kutuambia kama ushahidi wa kuonyesha kutohusika wkake. Anajua wazi kuwa kila mmoja anafahamu jinsi alivyohusika, na kusema uwongo kwake hivi sasa kutamuweka pabaya zaidi ya alipo
 
Mimi nashindwa kuelewa kwa nini watu wanakuwa waoga kwa EL kujitokeza hadharani na kusema ni kwa namna gani hausiki.Kama hausiki watanzania watajua kwa kupima maelezo yake.Nionavyo mimi watanzania wamepevuka kiasi kwamba wanaweza kuchambua pumba na ngano halisi.

Kutokumpa EL nafasi ya kujieleza sio sahihi tunamnyima haki yake ya msingi kabisa aliyopewa tena na Muumba ya kujitetea kabla mtu haujahesabika kuwa mkosa.Hata katiba yetu ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania inadhibitisha hilo.

Hapa jamvini tunatetea sana demokrasia na tunajua kwa hakika kuwa haki ya mtu kujieleza ni nguzo muhimu sana kwenye demokrasia.Kama kweli tunapreach what we believe na sii tuu tunapreach what we don't believe kuhusiana na demokrasia basi EL apewe nafasi ya kujieleza ndipo watu wa muhukumu.

Kuna wanao sema kuwa ni fisadi,kama wana data zake wana haki ya kusema hivyo.Lakini linapokuja suala la utendaji hakuna anayeweza kupinga kuwa anaubora maradufu zaidi ya muungwana aliyeko mjengoni.Mimi sitaki kuamini tu yale tunayoyasoma kwenye ripoti ya kina Mwakyembe au anachosema Salva Rweyemamu au Katibu Mkuu Kiongozi kwani hii ni ripoti ya upande mmoja.Nataka nipate fursa ya kumsikiliza na EL anasema nini juu ya Richmond.

Kama yeye naye hausiki,mkuu wa kaya hausiki,karamagi hausiki,Msabaha hausiki na RA naye hausiki tutapenda kujua Richmond ililetwa na nani na ilipataje tenda ya kusupply umeme kama haikuwa na bigshort aliyeipigia debe.

Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,tumuache EL ajieleze na ndipo hapo tupitishe judgement.Kwa uwezo uliopo hapa jamvini nina uhakika kuwa akijieleza judgement itakayotolewa itakuwa ya haki kwani watu hapa data wanazo.
 
Kachero, Lowassa alipata nafasi ya kujieleza hakutaka kufanya hivyo akaamua kususa; baadaye akajitokeza kwenye TV angalia kwenye http://www.youtube.com/mwanakijiji na utaona line ya maelezo yake kabla hajakatizwa. Lakini yeye mwenyewee na wapambe wake wanaamini wanao ushahidi wa kutosha kabisa wa kuonesha kuwa mhusika mkuu wa sakata hilo ni JK kwani EL anadai alijaribu mara kadhaa kuipinga Richmond lakini alikuwa overruled na JK.

So the line of his defence itakuwa kama hivi:

"Binafsi nilitambua matatizo ya Richmond kuwa x,y, z nikawasiliana na Ikulu na kuwaeleza reservation yangu lakini kwa barua namba x,y wakaniambia niendelee na hili. Na nilipoona kuwa hawa jamaa hawafai niliandika barua m,n kueleza ikulu kuwa hii kampuni haifai. Nilifanya DUE DILIGENCE (taking aim at what Luhanjo said) ya Richmond na sikuridhishwa nao na nikawaambia Ikulu (isomeke Kikwete) kuwa hii kampuni ni ya kilaghai. Lakini nilipewa jibu na Ikulu kuwa hali ni mbaya ya umeme na hivyo tuwaingize tu lakini tusiwalipe malipo ya awali (downpayment). Hivyo, kimsingi nilifanya jukumu langu lakini mambo mengine yalitolewa maamuzi yaliyonizidi mimi (Rais)".
 
Lowassa kukanusha au kutokanusha kuhusika ktk kashfa ya Richmond amechelewa. Hata kama kuna Wabunge watakaomsaidia kukanusha, wamachelewa. Majority ya umma wa Watanzania wanaamini alihusika na hawatamsamehe kwa kuchangia kwake ktk kututumbukiza zaidi ktk lindi la umaskini.

Huenda Lowassa akicharuka na kuungwa mkono na Wabunge walioko ktk mtandao wake, ataweza kuigawa CCM na kuwa tishio kwa J.K. mwaka wa 2010. Wana mtandao wake wamhimize wakati ukiwa muafaka.

Kuhusu Freeman Mbowe kuachia ngazi kama Mwenyekiti wa Chadema itakuwa ni jambo la kusikitisha kweli. Kama mwanaJF Gagnija alivyotamka hapo awali, Mbowe amedhihirisha ni kiongozi bora wa chama cha siasa, zaidi hata yeyote wa CCM, tangu Tanzania iingie ktk mfumo wa vyama vingi. Akiachia uenyekiti Chadema, uongozi wa CCM watasherehekea na nina hakika kuna wanaCCM wanaochochea Freeman aachie ngazi. Chadema chukueni tahadhari. CCM wajanja sana.

Chadema kimeonyesha kinaweza kubadilisha uongozi wa juu kitaifa bila kugawanyika. Bila shaka kinaweza kuteuwa Mgombea Urais kutoka miongoni mwa viongozi wake, bila kuwa na ulazima wa kumteuwa Mbowe.

Mwana JF Mwita Maranya amemtaja Dr. Kitila Mkumbo kama Mtanzania anayeweza kuwa Mwenyekiti wa Chadema. Mimi simjui, na nadhani siyo MwanaChadema mwenye wadhifa wa juu sana. Hata hivyo CHADEMA hakina shida ya kupata wanachama maarufu kitaifa au hata kimataifa. Watanzania wanaovalia suti za combati kutokana na kukereketwa kwao na uanachama wa Chadema wako wengi: waume kwa wanawake, jasiri , wazalendo, waadilifu na wasomi. Mmoja wao anaweza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti endapo Mbowe ataachia kiti. Mwingine, au huyo huyo, anaweza kuteuliwa na CHADEMA kuwa Mgombea urais.

Nilivyosema hapo mwanzo, Edward Lowassa, kutokana na kuhusika ktk kashfa ya Richmond na ushiriki wake na wahusika wengi wa kashfa nyingine kama za EPA na ufisadi kwa jumla, jina lake ni chafu. Licha ya kwamba Chadema wanaweza kumkaribisha kuwa mwanachama, kama Mtanzania yeyote anayesaini fomu ya kuomba uanachama, itakuwa ni foolhardy kumteua kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema. Wazo la Samwel John eti Lowassa ataleta ushindi kwa Chadema ni naivity in the extreme. Historia ya Lowassa haiwezi kushangiliwa na wanaChadema.
 
Kusema ukweli haitakuwa rahisi kwa EL kurudi tena kwenye ulingo wa siasa (kugombea President wa TZ) kama atabaki kuwa back bencher (hata kama akirudi bungeni 2010).
Political influence inapungua kila siku inavyopita na age is also taking its toll.
Ukiangalia sana age group yake wont be appealing to wapiga kura wakati huo.
Competion for political leadership kwa sasa na hasa huko baadaye ni kubwa na ni vijana ambao wako kati ya 30 - 40 watakao kuwa na nafasi nzuri 2010 na 2015.
 
Kuna habari ambazo bado mwandishi wetu hajapata uhakika nazo na hivyo kubakia kuwa ni tetesi ,inategemewa kuwa kabla ya mwezi huu kwisha kuna mabadiliko makubwa yatakikumba chama cha Chadema kwa baadhi ya viongozi wake kuachana na Chama hicho kutokana na malumbano ya chini kwa chini yanayorindimba ndani ya Chama hicho. Habari zaidi kwa watu wa Chadema ambao wapo hapa JF ,tunaona kimya kimekuwa kikubwa bila ya shaka yeyote ile wanachokificha sasa kinaanza kuja juu.

Baridi inayoonekana kuzizima hapa JF na kuwakaba wana Chadema kiasi ya kuwafanya waonekane kuwa ni bidhaa adimu kutokana na michango yao ya kasi na kukisifu chama chao ,sasa mambo yanawaendea vibaya na kuona kuwa kumbe hawana chama zaidi ya waganga njaa.
Mambo bado lazima lazima barabara mtaiita njia.
 
Si jambo la kusherehekea hili wewe. CHADEMA, CUF, TLP au chama chochote cha upinzani kikifa au kupata matatizo ni janga la kitaifa. Hapa si suala la CHADEMA bali ni demokrasia na utawala bora TZ.
 
kwa hali ilivyo sasa sidhani kama hii hali ni nzuri kwa kuwa CHADEMA ndio kama chama ambacho kina nguvu na ambacho angalau kinaisumbua CCM sasa kama kinaelekea kufa tena katika kipindi ambacho tunaelekea uchaguzi mkuu, kama ni kweli tuwaombee warudi katika amani na utulivu
 
Mwiba,
chadema nilianza kuona wanapoteza muelekea wa kuleta mabadiliko ya kidemokrasia baada ya kuanza kupambana na vyama pinzani badala ya CCM, vilevile badala ya kupigania kuipiku CCM kwa ufuasi na kukubalika kwa watu, wanapambana na CUF ambayo wana"advantage" kubwa ya kimuundo wa upnzani kuliko chama chochote cha siasa. MM naomba hizi ziwe tetesi tu, kwani bado Tanzania inahitaji kuwa na upinzani wenye nguvu zaidi kisiasa kuliko ilivyosasa na chadema wanaweza wakijipanga vizuri na kukubali kubadilika.
 
Unajua kifo cha Chadema nilikiona zamani sana ,hamuwezi kuwa na chama halafu ndani yake wakawemo mabepari ,sasa matokeo yake ndio hao wengine wananenepa na wengine wanakonda.
 
Kachero, Lowassa alipata nafasi ya kujieleza hakutaka kufanya hivyo akaamua kususa; baadaye akajitokeza kwenye TV angalia kwenye http://www.youtube.com/mwanakijiji na utaona line ya maelezo yake kabla hajakatizwa. Lakini yeye mwenyewee na wapambe wake wanaamini wanao ushahidi wa kutosha kabisa wa kuonesha kuwa mhusika mkuu wa sakata hilo ni JK kwani EL anadai alijaribu mara kadhaa kuipinga Richmond lakini alikuwa overruled na JK.

So the line of his defence itakuwa kama hivi:

"Binafsi nilitambua matatizo ya Richmond kuwa x,y, z nikawasiliana na Ikulu na kuwaeleza reservation yangu lakini kwa barua namba x,y wakaniambia niendelee na hili. Na nilipoona kuwa hawa jamaa hawafai niliandika barua m,n kueleza ikulu kuwa hii kampuni haifai. Nilifanya DUE DILIGENCE (taking aim at what Luhanjo said) ya Richmond na sikuridhishwa nao na nikawaambia Ikulu (isomeke Kikwete) kuwa hii kampuni ni ya kilaghai. Lakini nilipewa jibu na Ikulu kuwa hali ni mbaya ya umeme na hivyo tuwaingize tu lakini tusiwalipe malipo ya awali (downpayment). Hivyo, kimsingi nilifanya jukumu langu lakini mambo mengine yalitolewa maamuzi yaliyonizidi mimi (Rais)".

Nakubaliana na wewe Mzee MJJ kuwa hofu yao wanaomzuia EL kujitetea ni kwa sababu anaweza kuthibitisha kuwa muungwana ndiye aliyeibeba Richmond mpaka hapo ilipofika na endapo ikidhibitika hivyo muungwana naye si atakuwa kwenye wakati mgumu kisiasa na hao wanaosisitiza sasa hivi ajiuzulu watapata rungu la kumtwanga nalo kichwani.

Na hapa ndipo panapokuwa patamu,siku zote tumesema kwamba viongozi tulionao hawana mioyo dhabiti ya kuwajali watanzania na kuwaletea maendeleo.Walio wengi wanajali maslahi binafsi na ni wabadhirifu wa rasilimali za nchi.

Mimi ningependa EL ajitokeze wazi wazi na kusema nani yuko nyuma ya Richmond Devl Company na kutoa udhibitisho ili tuone mtafaruku wa kisiasa utakaojitokeza.Baada ya hapo ndipo wananchi walio wengi watafahamu mbivu ni zipi na mbichi ni zipi kwa kuwa mpaka sasa kinachoendelea ni kiini macho tuu.
 
Mbowe kasikia harufu ya Ankara kwenye Ubunge. Mnakumbuka CDF inakuja....an easy money for smart guys.
 
Kachero, Lowassa alipata nafasi ya kujieleza hakutaka kufanya hivyo akaamua kususa; baadaye akajitokeza kwenye TV angalia kwenye http://www.youtube.com/mwanakijiji na utaona line ya maelezo yake kabla hajakatizwa. Lakini yeye mwenyewee na wapambe wake wanaamini wanao ushahidi wa kutosha kabisa wa kuonesha kuwa mhusika mkuu wa sakata hilo ni JK kwani EL anadai alijaribu mara kadhaa kuipinga Richmond lakini alikuwa overruled na JK.

So the line of his defence itakuwa kama hivi:

"Binafsi nilitambua matatizo ya Richmond kuwa x,y, z nikawasiliana na Ikulu na kuwaeleza reservation yangu lakini kwa barua namba x,y wakaniambia niendelee na hili. Na nilipoona kuwa hawa jamaa hawafai niliandika barua m,n kueleza ikulu kuwa hii kampuni haifai. Nilifanya DUE DILIGENCE (taking aim at what Luhanjo said) ya Richmond na sikuridhishwa nao na nikawaambia Ikulu (isomeke Kikwete) kuwa hii kampuni ni ya kilaghai. Lakini nilipewa jibu na Ikulu kuwa hali ni mbaya ya umeme na hivyo tuwaingize tu lakini tusiwalipe malipo ya awali (downpayment). Hivyo, kimsingi nilifanya jukumu langu lakini mambo mengine yalitolewa maamuzi yaliyonizidi mimi (Rais)".
Mzee wangu wee! hivi kweli watu wanafikiria kuwa JK atakuwa mjinga kiasi hicho kweli!
Yaani yeye aruhusu Richmond iingie nchini kisha aruhusu Uchunguzi ufanyike na kamati ya Bunge (watu wanaomuunga mkono) wasimamie na waifanyie kazi ipaswavyo kisha ipelekwe kwake na bila kuisoma atoe amri ipelekwe Bungeni na yeye anakuja huko Chimwaga!..Jamani hivi kweli kuna watu wamesha sahau sakata lile lilivyopamba moto?...

Mbali na yote yeye awe mhusika akitegemea Lowassa atakubali kufa peke yake! mbali na kwamba Lowassa alimfuate Ikulu na kilio kikubwa, Jk amtolee nje wakati akijua wazi kwamba yeye JK ndiye mhusika na sii Lowassa, hii inaingia akilini kweli!..kisha basi pamoja na kugeukwa huko huyo Lowassa akubali kujiuzuru ili anaaze upya kivyake vyake vita dhidi ya JK mwenye deal lililomwangusha..
Jamani tuwe tunatazama shilingi kwa pande mbili.. JK anaweza kuwa mjinga lakini sii mjinga hivyo!..
Mbali na yote haya ebu turudi nyuma tusome hongera zetu wakati Mwakyembe alipomwaga radhi bungeni. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/15858-ripoti-ya-mwakyembe.html

Leo hii huyo Sitta aliyehakikisha uchunguzi unafanyika, Mwakyembe aliyewasilisha starehe kwa wananchi na JK aliyetoa ruksa wanaonekana nuksi machoni mwa Wadanganyika.. Hivi kweli tutaweza kupata Uhuru wa kweli nchii hii! ikiwa haya ya juzi tu tayari tumekwisha sahau...
Trust me, mkuu wangu sii ajabu hata wewe utakuja itwa fisadi, wee subiri tu wala sii muda utaonekana una share GM, au ndio umesababisha GM kufilisika..
 
Lowassa kukanusha au kutokanusha kuhusika ktk kashfa ya Richmond amechelewa. Hata kama kuna Wabunge watakaomsaidia kukanusha, wamachelewa. Majority ya umma wa Watanzania wanaamini alihusika na hawatamsamehe kwa kuchangia kwake ktk kututumbukiza zaidi ktk lindi la umaskini.

Huenda Lowassa akicharuka na kuungwa mkono na Wabunge walioko ktk mtandao wake, ataweza kuigawa CCM na kuwa tishio kwa J.K. mwaka wa 2010. Wana mtandao wake wamhimize wakati ukiwa muafaka.

Kuhusu Freeman Mbowe kuachia ngazi kama Mwenyekiti wa Chadema itakuwa ni jambo la kusikitisha kweli. Kama mwanaJF Gagnija alivyotamka hapo awali, Mbowe amedhihirisha ni kiongozi bora wa chama cha siasa, zaidi hata yeyote wa CCM, tangu Tanzania iingie ktk mfumo wa vyama vingi. Akiachia uenyekiti Chadema, uongozi wa CCM watasherehekea na nina hakika kuna wanaCCM wanaochochea Freeman aachie ngazi. Chadema chukueni tahadhari. CCM wajanja sana.

Chadema kimeonyesha kinaweza kubadilisha uongozi wa juu kitaifa bila kugawanyika. Bila shaka kinaweza kuteuwa Mgombea Urais kutoka miongoni mwa viongozi wake, bila kuwa na ulazima wa kumteuwa Mbowe.

Mwana JF Mwita Maranya amemtaja Dr. Kitila Mkumbo kama Mtanzania anayeweza kuwa Mwenyekiti wa Chadema. Mimi simjui, na nadhani siyo MwanaChadema mwenye wadhifa wa juu sana. Hata hivyo CHADEMA hakina shida ya kupata wanachama maarufu kitaifa au hata kimataifa. Watanzania wanaovalia suti za combati kutokana na kukereketwa kwao na uanachama wa Chadema wako wengi: waume kwa wanawake, jasiri , wazalendo, waadilifu na wasomi. Mmoja wao anaweza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti endapo Mbowe ataachia kiti. Mwingine, au huyo huyo, anaweza kuteuliwa na CHADEMA kuwa Mgombea urais.

Nilivyosema hapo mwanzo, Edward Lowassa, kutokana na kuhusika ktk kashfa ya Richmond na ushiriki wake na wahusika wengi wa kashfa nyingine kama za EPA na ufisadi kwa jumla, jina lake ni chafu. Licha ya kwamba Chadema wanaweza kumkaribisha kuwa mwanachama, kama Mtanzania yeyote anayesaini fomu ya kuomba uanachama, itakuwa ni foolhardy kumteua kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema. Wazo la Samwel John eti Lowassa ataleta ushindi kwa Chadema ni naivity in the extreme. Historia ya Lowassa haiwezi kushangiliwa na wanaChadema.

Mkuu hapo umenena,
Freeman akienda gombea ubunge itakuwa vyema sana kuongeza mpambano ndani ya jumba, Kupata mwenyekiti kwa CHADEMA si tatizo, kwani imesheneni watu makini sana, mfano pia yupo Prof. Baregu, anafaa sana kushika nafasi hiyo, lakini pia ataua kabisa ile sumu inayo pandikizwa kwamba Chadema ina ukabila.
 
Let's wait and see what happens.

Hi everyone; I'm back.

Some updates and new information:

- We had advised M to write the original report in English but he refused arguing that this one was for the regular Tanzanians consumption so there was no need to put in Engglish. But, after a number of Human Rights Organisations have inquired about it our team is now working on releasing an English summary of the report. It should take us about seven days.

- We have noticed some interesting patterns on the part of Lowassa and his team. All the evidence and intelligence we have collected point to the reality that Lowassa is going to categorically deny wrong doing in the Richmond Affair and would put total blame absolutely on Kikwete. They have had another meeting with some of their supporters in the past few hours on which way to go especially after Luhanjo's ridiculous defense and indictment of Kikwete's role in the whole affair.

- Once he strike back at Kikwete and the people who have accused him of improprierty and corruption it is expected the act to usher a permanent rupture of his strategic friendship with Kikwete. This will officialy divide CCM into two camps as the party moves towards general election next year. The recent announcements about possible canditates are just a preludes of the oncoming collision between Lowassa's camp and Kikwete's.

- Meanwhile as Chadema is moving towards its general election in a month or so there is a strong indication that Mbowe would finally give up the chairmanship to someone else. However, there are some people who still believe he should lead the party towards general election while others believe that the time has come for a new leadership to lead the party towards victories next year. He is expected to run for a parliamentary seat.
 
Back
Top Bottom