Lowassa tena!.... Usiku wa manane ndani ya Kumbi za Starehe

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,277
8,492
Kuelekea 2015 tutaona mengi ikiwa na pamoja na sharubu za simba kuchezewa na swala.

LOWASSA.jpg


Rhobi Chacha na Musa Mateja
Waziri Mkuu Mstaafu aliye pia Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Ngoyai Lowassa, ameipamba fani ya burudani kwa rangi ya aina yake, Ijumaa lina mkanda mzima.

Lowassa aliyezoeleka katika kilinge cha siasa, usiku wa Jumanne wiki hii alinaswa ‘laivu' katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, kulikokuwa na maadhimisho ya miaka mitano ya Nyumba ya Kukuza Vipaji Bongo (THT).

LOWASSA-1.jpg


Katika usiku huo, mbali na maadhimisho ya THT, pia wasanii sita waliokuzwa na nyumba hiyo, kila mmoja alizindua albamu yake.

Wasanii hao ni Estelina Sanga ‘Linah', Elias Barnabas ‘Barnaba', Amini Mwinyimkuu, Ally Mataluma, Lameck Ditto ‘Dogo Ditto' na Mwasiti Almasi.

Lowassa alishuhudia mpango mzima kwa Linah kuipua albamu yake ‘Atatamani', Barnaba akazindua kitu chake ‘Kichwa Changu', Amini ‘Yameteka Dunia', Mataluma ‘Mama Mubaya', Mwasiti ‘Siyo Kisa Pombe' na Ditto ‘Wapo'.

SAA 3:30 USIKU:
LOWASSA AINGIA UKUMBINI
Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na mapaparazi wetu, Lowassa aliyekuwa mwalikwa maalum, ‘alitimba' ukumbini humo majira ya saa 3:30 usiku akiambatana na ‘mai waifu' wake, Regina.

watuuu.jpg


Baada ya kukanyaga sakafu ya ukumbi huo, Lowassa na mkewe walikwenda moja kwa moja katika meza ya mgeni rasmi ambaye alikuwa Waziri wa Habari, Vijana na Michezo, Emmanuel Nchimbi kisha ‘wakajisevia siti'.

SALAMU, STORI ZATAWALA MEZA KUU
Mara walipojihakikishia eneo la kukaa, Lowassa na mama Regina waliwasabahi waliowakuta mezani kisha stori mbili tatu zikachukua nafasi kabla ya kuendelea na ratiba ya tukio husika.

SAA 3: 45 USIKU:
LOWASSA ASHUSHA FUNDA LA MAJI
Baada ya kimya cha dakika kadhaa, Lowassa na meza kuu walishusha funda moja la maji huku nderemo na vifijo vikitawala wakati vijana wa THT Dancers walipopanda jukwaani kufungua burudani.

mwasiti.jpg

SAA 6:45 USIKU:
LOWASSA AFURAHIA SHOO
Katika tukio la aina yake, Lowassa alionekana akishangilia kwa msisimko wa hali ya juu huku akipiga makofi, aliposikia ‘ngoma' ya Mataluma inayokwenda kwa jina la ‘Kariakoo'.

SAA 6:50 USIKU:
LOWASSA, NCHIMBI WASHUHUDIA VIJANA WA KILEO
Tukio lingine la kusisimua ni lile la vijana wa kileo waliovaa na kupendeza waliokuwa wakicheza mbele ya Waheshimiwa Lowassa na Nchimbi bila kujali uzito wa ‘wakubwa' hao.

SAA 7: 15 USIKU
BARNABA, LINAH WAITWA KUSALIMIA MEZA KUU
Hali haikuwa shwari kwa wasanii wa THT waliokuwa nyuma ya jukwaa ‘back stage' baada ya ‘mdada' mmoja (jina halikupatikana mara moja) kuwafuata Barnaba na Linah kisha kuwapeleka kusalimia meza kuu.

Hata hivyo, baada ya zoezi hilo kuliibuka minong'ono miongoni mwa wasanii wenzao kuwa kwa nini waitwe wao tu?

7:30 USIKU:
MEZA KUU WAONDOKA UKUMBINI
Shangwe zilifikia kikomo baada ya msanii Mataluma kumaliza shoo ambapo Lowassa na meza kuu walifunga virago na kuondoka ukumbini hapo huku wakiacha shoo ikiendelea.

SAA 7: 45 USIKU
AY, FLAVIANA WABAMBWA
Katika kumalizia matukio yaliyogonga vichwa, msanii wa Bongo Fleva, Ambwene Yesaya ‘AY' alibambwa akiwa ‘klozi kimtindo' na mwanamitindo wa kimataifa, Flaviana Matata. Paparazi wetu ‘aliwafotoa' lakini wakashtukia ‘mchezo'.

AY alionekana kukwepa picha na baadaye aliihama meza ‘akizuga' kupiga stori na ‘presenta' wa Radio Clouds FM, Hamisi Mandi ‘B12'.

maunda.jpg


SAA 8:15 USIKU:
SAFARI YA KUELEKEA MZALENDO PUB YAANZA, MVUA YADONDOKA
Mapaparazi Wetu, Issa Mnally na Shakoor Jongo waliokuwa katika Ukumbi wa Mzalendo Pub, uliopo Millennium Towers, Kijitonyama kulikokuwa na tafrija iliyokwenda kwa jina la Celebrities Party, wanaripoti kuwa, mastaa walidondokewa na mvua iliyoharibu mambo.

Katika ‘pati' hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan, mastaa walikosa eneo la kujikinga mvua kwa kuwa ‘kiwanja' hicho hakina paa, hivyo kila mtu akatambaa kivyake.

Hata hivyo, mvua hiyo haikudumu muda mrefu ambapo baada ya kukatika watu walirejea ukumbini hapo na kuendelea kupata burudani hadi mwisho.
 
Hivi hadi muambiwe mara ngapi kwamba mafisadi Ulimwengu mzima huu sasa umegeuka ndogo sawa ili nafasi ya ndani ya kiatu chako tu?? Kumbe hamuelewi kwamba Wananchi tumewashika korodani na sasa kila kona kunabana?
 
Achana na Lowassa, matatizo ya nchi hii ni boss mkubwa na wapambe wake wamesababisha ila naona kila mtu anamuandama Lowasa
 
Tatizo wabongo wengi huwa hatupendi kuwa wadadisi zaidi wa mambo. Fisadi lowassa fani yake aliyoisomea chuo kikuu cha Dar es Salaam ni Sanaa ya Jukwani.

Na hapo ukumbini usiku wa manane Mlimani City ndiyo haswa taaluma yake, haki ya nani tena. Kwa bahati mbaya hiyo ni fani ambayo hajawahi kuifanyia kazi popote duniani wala kumuingizia senti tano mfukoni lakini leo hii ni bilionea; unanusa kitu gani hadi hapo Mdanganyika?

Na kweli kama alivyowahi kusema mwenyewe, yeye na Kikwete hawakukutana barabarani ndio waachanie babarani. Jamaa walikutana kwenye sanaa JK akiwa ni mcharaza nyuzi huku EL akiendeleza zile za Mr Yebo kulee hall 4.
 
anaenda kufurahia ushindi wa polisi ktk mapambano yalio pelekea raia wetu wazalendo kuu awa kidhalim.
 
Kama alialikwa kama mgeni rasmi cha ajabu ni nini? angetaa kuja simngesema kadharau!! jamani jamani
 
Tatizo liko wapi?

Lowassa anayo haki kama mtanzania mwingine kustarehe kama anavyotaka!

Udaku wa Global Publishers bana!
 
mie nimetamani kumjua huyo mdada alievaa top nyekundu,....jamani jamani...pweeehh
 
Mungejua EL alipigwa mkwara na Lamwai kuwa hawezi ku- argue na wacheza sindimba, alikamata benchi hadi leo, shauri yenu kama mnaajira za kidole, Mshikaji hana hamu na EL!
 
Huyu kijana hapa mbele aliyekaa na huyu dada alieachia utamu kiana ni karmbua kafunga macho? na viatu vyake ni viaonekana vikali sana

watuuu.jpg
 
Ondoa hii crap peleka kwenye jukwaa la celebration, kwani Lowasa(licha ya ufisadi wake) harusiwi kushiriki kwenye mitoko mbalimbali? msitujazie thread za kitoto hapa kwenye jukwaa la siasa. kwani hicho kigazeti cha udaku si ndio kilichoandika leo kwamba Bakwata inaongozwa na mkristo?
 
Jamani kwani Lowassa naye hana haki ya kustarehe??? Vitu vingine havina tija kuvizungumzia
 
Back
Top Bottom