Lowassa,Sitta na Membe kweli wanamaanisha kuhusu tatizo la ajira kwa vijana?

bubukapoka

Member
Oct 29, 2011
11
1
Hello guys,
Hivi karibuni tumewasikia baadhi ya viongozi wakilipigia kelele suala la ukosefu wa ajira kwa vijana wa Tz wakiwemo Lowasa,sita na Membe kwa nyakati tofauti,Najiuliza maswali mengi juu yao,
-Hilo tatizo wameliona leo tu miaka iliyopita halikuwepo?
-Wameshindwa kabisa kulijengea mikakati ndani ya serikali yao na chama chao na hivyo kuamua kupiga kelele mitaani?
-Wameshindwa kutambua ya kwamba ufisadi na ombwe la uongozi ktk serikali na chama chao ndio kiini cha tatizo?
-Wameshindwa kubaini ya kwamba kwa kuwa wao ni sehemu ya chama na serikali ni sehemu ya tatizo? au
-Ndio ule unafiki unaosemwa,lengo likiwa ni kuwavuta vijana wawaamini ili kukamilisha ndoto zao za kwenda Ikulu?

Tutafakari kwa makini juu ya hawa watu?

Think Gray not Green?

Nawasilisha.
 
Mkuu,

FISI mdogo, FISI mkubwa na FISI aliekubuhu, wanatofauti gani? Watatu hao ni FISI wanaweza wakatofautiana Umri, Kimo na Umbile lakini tabiana Maumbile ni yaleyale. Tamaaaaaaaaaaaaaaaa tuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!
 
Mgomba ambao haukutoa ndizi kwenye ardhi ya rutuba kutegemea ubebe ndizi bora jangwani ni uongo mweupe. Tujiulize ktk nafasi zao za sasa ngazi ya jimbo wamewafanyia nini hao vijana? Kama wameshindwa kuikabili changamoto ya vijana wasiozidi elfu 80 watawezaje kuikabili ya vijana zaidi ya milioni 18?
 
Wanataka kuwin popularity kwa vijana ili kujiweka vizuri kisiasa!! Wameshaona 2015 ni vijana ndo watakaoamua nani aingie magogoni!!
 
Ziko lugha zinazoweza kutumika kwa watu ambao wanajifanya weupe kumbe wao ni weusi. Lugha hizi ni pamoja na unafiki, uzandiki, uongo na kuwafanya wenzio wajinga.wote hao wamelitumikia taifa hili kwa nafasi za juu kabisa wakiwa na nafasi kubwa tu kuliko watanzania wengine kuchangia katika kuleta mabadiliko. Na kuwa wamo katika vyombo muhimu na kwa kuwa bado wana nafasi ya kushauri katika kuleta mabadiliko kupiga kelele nje kunatushangaza sisi watu tunaofikiri. Hivi wametuona wajinga sana au wanafikiri vichwa vya watanzania vimesimama kufanya kazi au.... ama.... au. Waache michezo ya kuigiza Watanzania tunaumia na wao kwa sababu hawana ushauri kuhusu tatizo la ajira kwa vijana then they are part of the Problem. Kelele wanazopiga ni Bluf tu kujisafisha na kujenga mazingira ya kuingia katika kinyang'anyiro cha urais 2015 Poleni mwee!
 
Kimsingi ukosefu wa ajira kwa vijana ni tatizo dunia nzima,ili uweze kupata sapoti ya vijana angolea matatizo yao,hivyo basi mwanasiasa yoyote makini ni lazima aongelee tatizo la ajira
 
Watu wakikaa kimya tunalalamika! wakiongea pia tunalalamika na kuwaona wanafiki! mnataka hao kina lowasa na wenzake wafanyeje ili muwaaminii? au mnataka waongee kwa m.a.t.a.k.o ndio mtajua kuwa wanamaanisha? acheni hizo jamani!
 
Back
Top Bottom