Lowassa, Sitta, Kilango wapata pigo kubwa!!!!

Kambi ya wale wanaojiita wapambanaji dhidi ya ufisadi ndani ya chama tawala cha CCM imepata pigo kubwa kufuatia matokeo ya uchaguzi wa ubunge jimbo la Arumeru mashariki na chaguzi za udiwani katika kata 8 tofauti. Kambi hiyo ilitoa wafuasi wake watatu kushiriki katika kampeni za chaguzi hizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumsaidia mkwe wa Lowassa, Siyoi Sumari. Samuel Sitta ambaye ndio kiongozi wa kambi hiyo alipiga kambi jijini Mwanza na kuongoza kampeni katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Kirumba na kushindwa kuwashawishi vilivyo wakazi wa Kirumba ambao walimchagua mgombea wa CHADEMA kuwa diwani wao. Naye Anne Kilango alipiga kambi huko kiwila kuongoza kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya Kiwira lakini naye aliangukia pua kwani mwisho wa siku mgombea wa CHADEMA aliibuka mshindi dhidi ya mgombea wa CCM. Kama hiyo haitoshi, Christopher Ole Sendeka alikuwa mmoja wa wana ccm walioshiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki lakini pia ushawishi wake na ule wa Lowassa na wengine wa ccm haukutosha kubadili mawazo ya wananchi wa Arumeru ambo bila ajizi wamemchagua Joshua Nassari wa CHADEMA kuwa mbunge wao. Matokeo hayo kwa ujumla ni pigo kubwa kwa kambi ya Lowassa na Sitta ambaye wakati Fulani alionekana kuaminiwa na wananchi hasa wakati huu ambapo Samuel Sitta ameshaeleza nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Sasa wananchi wameonesha kwamba hawana imani hata na wana CCM wanaojipambanua kama wapinga ufisadi. Sasa nani aaminiwe katika CCM????!!!!!!!

Aliaminiwa Mwl Nyerere na Karume tu,Waliobaki ni sawa na fisi kumkabidhi zizi la mbuzi
 
Back
Top Bottom