Lowassa, Rostam waumbuana

Kama wanataka kujisafisha kwa nini waunde mtandao au wategee serikali na watu wengine ndio wafanye hivyo? Tangu lini mtu mwenye kujiweza kiakili timamu akaenda msalani na kufanya majambozi humo msalani na kuondoka bila kusafisha choo au kujisafisha yeye mwenye na kutegemea watu wengine waje wafanye kazi hiyo? kama akitegemea watu wengine wafanye hivyo atakuwa ni mvivu wa kufikikiri au amefirisika kimawazo...

Nimwambie tu yeyoye aaliye na nina ya kujisafisha ni namna mbili.
1. Aende mahakamani na kuomba judicial review ya yale yote yaliyofanywa na bunge... kama bunge litaonekana kwamba utafiti wake uliuwa na walakini, basi uamuzi utakuwa wake wa muuomba hiyo Judicial review... anaweza kufungua kesi nyingine ya madai dhidi ya bunge au serikali kwa niaba ya bunge apewe fidia... huki ni kujisafisha number 1.#

2. Aitishe mkutano wa waandishi wa habari , alete au atoe vielelezo vyote (Counter- evidence) ambazo ni haziwezi kupingika kama zikisimama zenyewe... nina maana kwamba ushahidi atakao utoa uyajibu maswali yote yaliyotolewa na kamati ya mwakyembe...
Ushahidi huu uwe ni proof beyond resonable doubt na sio on balance of probabilities maana yalisemwa juu ya mafisadi ni mengi sana...
 
Pamoja na matumbo yote haya na ujinga wa hali ya juu eti mtu anakuja hapa anasema CCM safi na itashinda kwa kishindo ? Labda watangazwe na Tume kama kawaida lakini si kusema Watanzania can buy those stories of theirs .Shame on you CCM Pinda na wengineo.
 
kuna msemo waingereza wanapenda kuutimia "punda mwenye kujua ujanja mmoja tu" ndio CCM inavyoonekana, sasa wameshaingia na mbinu ya kutumia neno la uzembe wa kazi hii ndio line watakayo ifuata inavyoonekana kuwatoa walio juu.

utasemaje mkubwa alikuwa mzembe wakati job description ni kutoa maamuzi ya mwisho baada ya kuangalia information ulizonazo, sasa leo uta semaje ulidanganywa na walio chini yako, kwani richmond ni wizi shilling 1000. hebu waache hadithi chanzo lazima kiwe juu na sio chini kama wanavyoipeleka hii shutuma. Maskini ya mungu sijui akina nani ndio wanao tayarishwa kama mbuzi wa mifano.

kamati yenyewe inakuja na majibu ya upuuzi hivi na hiyo kamati basi inapoteza tu muda, kwani basi atakutunga uongo ni kazi hivyo inachukua mwaka mzima kusema fulani alikua mzembe tu na fulani nae ni mzembe hivyo hivyo aiiiiiiiii.
 
jamani huyu Lowassa anataka kuwa nani kwenye nchi hii, hiyo heshima aliyopewa ya kuwa pm wa muda si inamtosha
 
Aa wapi bwana!

Pamoja na vishindo vya Tembo, Simba na Nyati kutawala Nyika, Siafu( Watanzania) wakichachamaa nyika hazikaliki na vishindo vyote hukoma.
Watoto wetu ndo wataua soo hizi tulizo zianzisha sitegemei jipya kutoka ndani ya kizazi hiki kilicho chanzo cha kila songombingo nchini Tanzania.
 
Unajua ninawashangaa sana nyie wananchi. EL hajapewa nafasi ya kujieleza nyie so far mmesikia taarifa ya upande mmoja lakini tayari mna shout: ASULUBIWE ASULUBIWE.

Mie bado ningependa kumsikia RA na EL wana lipi la kusema, ile kamati ya Mwakyembe haikuwatendea haki kutowahoji vizuri na kupata maelezo yao.
 
Unajua ninawashangaa sana nyie wananchi. EL hajapewa nafasi ya kujieleza nyie so far mmesikia taarifa ya upande mmoja lakini tayari mna shout: ASULUBIWE ASULUBIWE.

Mie bado ningependa kumsikia RA na EL wana lipi la kusema, ile kamati ya Mwakyembe haikuwatendea haki kutowahoji vizuri na kupata maelezo yao.

Kila jambo lina ukomo wake.
Fikiria tu kwamba hata uwe mwema na mwenye afya njema kwa kiwango cha juu, lazima uonje mauti na kufikia tamati.
EL na RA wapewe nafasi ili waongee nini?
Hii ni sawa na kujaribu kuwapa fursa kukata rufaa ya vifo vyao vya asili.
Ni vema kuupa mzoga wa punda uhai kuliko kuwapa fursa hawa ndugu.
 
kazi ipo ila kuna siku mafisadi watapotea kama upepo, lkn tujiulize je hatuwezi? Kama tunaweza kwanini hatufanyi, mafisadi tunawachagua wenyewe kwa hiyari bila kulazimishwa, na tuseme basi inatosha kwa kuwanyima kura,
Mungu ibariki JF
Mungu ibariki Tz
 
If it is found to be true that RA uses his paper for propaganda reasons the people should stop buying his papers on news stands. The less circulated and read his newspapers are the less his propaganda can spread. The only problem is how do we achieve this.
sidhani kama hiyo itakuwa njia sahihi ya kupigana na ufisadi...
 
Jamani mimi nimebahatika kuishi nje ya nchi, nimeona jinsi viongozi waliofanya makosa serikalinim jinsi wanavyoshugulikiwa, hawa wakinalowasa serikali ingetakiwa iwasimamishe shughuli zote zinazohusihana na serikali, ubunge pia wangetakiwa wavuliwe wawe wananchi wa kawaida,ni upumbavu kumuacha mtu kama huyu aendelee kuwawakilisha wananchi bungeni.
 
Unajua ninawashangaa sana nyie wananchi. EL hajapewa nafasi ya kujieleza nyie so far mmesikia taarifa ya upande mmoja lakini tayari mna shout: ASULUBIWE ASULUBIWE.

Mie bado ningependa kumsikia RA na EL wana lipi la kusema, ile kamati ya Mwakyembe haikuwatendea haki kutowahoji vizuri na kupata maelezo yao.
Mkuu achana nao hao kabisaaaaaa tangu mchakato wa kamati ya Richmonduli ilipoanza kazi hawa jamaa wanakwepa kukutana nayo na wanakwepa kusema ukweli.
Mara wanakimbia mara wako safari. Wakitoka safari hawataki kuonekana kwenye tume, sasa si watawala tena lakini hawataki kusema bado ukweli, na kwa kuwa ukweli tunaujua na mwingine tuliuacha ili tusiivue nguo sirikali hata usemeje hawawezi kuja kujitetea.
Wao ni wezi na mafisadi wa kimataifa.
 
Unajua ninawashangaa sana nyie wananchi. EL hajapewa nafasi ya kujieleza nyie so far mmesikia taarifa ya upande mmoja lakini tayari mna shout: ASULUBIWE ASULUBIWE.

Mie bado ningependa kumsikia RA na EL wana lipi la kusema, ile kamati ya Mwakyembe haikuwatendea haki kutowahoji vizuri na kupata maelezo yao.
Lowassa alikuwa mtu wa kwanza kutoa mchango wake baada ya ripoti ya Mwakyembe kuwasilishwa. Utetezi wake tuliusikia na tumeuelewa, apatiwe nafasi gani tena? Huyo Rostam si aliikimbia tume?
 
mimi nadhani sasa Watanzania hatuna jipya kuhusu nhawa jamaa RA na EL, kila siku hizi habari zinarudiwa rudiwa tu, mimi nadhani hapa suluhisho zuri ni kutafuta njia ya kuwafikisha hawa jamaa mahakamani, sasa sijuhi mtu kama mengi ambaye anao ushaihidi huu wote anashindwa kuchua initiative ya kuwapeleka hawa jamaa mahakamani
 
Enzi zileza JF Bila TISS kulikuwa na nondo si kawaida lowassa Magufuli anasema kaimarishe chama kimekufa
 
Back
Top Bottom