Lowassa: Rais Kikwete ni jasiri, mwadilifu

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]JUMAMOSI, AGOSTI 04, 2012 05:29 NA MWANDISHI MAALUMU, MONDULI

WAZIRI Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, amemweleza Rais Jakaya Kikwete kuwa ni rais wa kwanza katika historia ya Tanzania kujali wafugaji kwa kiasi kikubwa mno na kiongozi mwenye uwezo wa kuchukua uamuzi wa kijasiri, kishujaa na kwa uadilifu.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa juzi, wakati alipozungumza katika sherehe ya kukabidhi ng’ombe kwa wananchi wa Wilaya ya Monduli waliopoteza mifugo yao kutokana na ukame uliolikumba eneo la kaskazini mwa Tanzania mwaka 2008/2009.

Lowassa, aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Rais Kikwete kati ya 2005 na 2008, aliwaambia wananchi waliohudhuria sherehe hizo: “Nimesimama kukushukuru Mheshimiwa Rais kwa msimamo wako wa kutetea wafugaji wa Tanzania. Hakuna Rais yeyote katika historia ya nchi yetu amepata kuwajali na kuwatetea wafungaji wa Tanzania kama wewe.

“Nakupongeza kwa uamuzi wako wa kishujaa, kijasiri na wenye kuongozwa na uadilifu, kama huu uamuzi wako wa kutoa kifuta jasho kwa wananchi wetu ambao walipoteza mifugo yao yote wakati ule wa ukame.”

Aidha, amempongeza Rais Kikwete kwa uamuzi wake wa kutoa kiasi cha Sh bilioni tatu za kukarabati mabwawa na madaraja yaliyoharibiwa na mvua kubwa iliyofuatia miaka ya ukame.

“Mheshimiwa Rais, kama unavyojua mvua ile kubwa iliyofuatia ukame mkubwa iliharibu sana mabwawa na madaraja yetu na nikaomba msaada wako. Nilikushuhudia wewe mwenyewe ukitoa maelekezo kwa Waziri Mkuu kuwa sisi Monduli tupewe fedha hizo na nashukuru sana tumepata,” alisema Lowassa.

Aidha, amemshukuru Rais Kikwete kutokana na Wilaya ya Monduli kupewa fedha za kuendeleza elimu wilayani humo kutokana na fedha iliyorudishwa na Serikali ya Uingereza kwa Serikali ya Tanzania kutokana na ununuzi wa rada.

“Nikushukuru pia kutokana na ule mgawo kutokana na rada change. Tumepokea fedha na tumezitumia kukarabati shule mbili za sekondari wilayani kwetu. Tunakushuru sana Mheshimiwa Rais,” alisema Lowassa.

 
Hana lolote huyo. Anabembeleza ili apasiwe kijiti mbio za urais.
 
Atabwabwaja kila awezalo ili kujisafishia njia kuelekea 2015...Eti DHAIFU ni jasiri na mwadilifu!!! lol!
 
Mchezo wa kuigiza na siasa za Tanzania .......kulindana na kusifiana!!huwezi kupata michezo kama ya Tanzania sehemu ingine yeyote
 
Wameuza mbuga yote, kwanini asiwapige na changa la macho? na anjua hao ng'ombe ni pint ya faida ya wizi uliofanyika. hii wala siyo siasa ni mazingaombwe kwa lowasa kumpa sifa huyo mwizi mwenzake. labda sasa anabidi ajikombe anajua bill za afya yake zinaweza kumzidi kimo na akafilisika. maana kwenda kutibiwa nje siyo kama kwenda mikocheni hospital. lakini watanzania tumeshawajua zao wao waungane sana na sio masikini tunashikana taratibu mpaka kieleweke.
 
Analilia kusafishwa, hajui kama amechafuka kwenye damu, sijui atasafishwa vipi, labda kwa dialysis
 
huyu huyu lowassa sio ndio alisema serikali imeshikwa na ugonjwa wa kutokuchukua hatua? leo hii tena vasco kageuka jasiri? halafu mbona majanga ya kufa mifugo yanatokea nchi nzima watu hawapewi chochote lakini huko monduli kumepewa kipaumbele jk anabembeleza nn??
 
huyu ndio mnataka awe rais 2015, watu wengine bana, eti jasiri! kwa kugawa ng'ombe! duh! kaaz
 
Duh baada ya kukutana London juzi,kuna kitu waliongea nini.Yetu macho
 
hahahahaaaaa, khekhekhekheheeheeeeee, kwikwikwikwikwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom