Lowassa ni mtendaji wa kuaminiwa!

Tumeshamwona tumemjua hatumuhitaji tena, wapo wachapa kazi na waadilifu kuliko wengi sana yeye.Tuige mfano wa Ulaya mtu anapochafuka tu anatupwa mbali na ikibidi sheria inachukua mkondo kwa njia hiyo kwanza italeta uadilifu na uwajibikaji wa kweli,tukiendela na utaratibu huu wa kurudishana na kusafishana ndio kwanza tutakuwa tunapalilia ujangili.Tanzania ina nguvu kazi kubwa sana hatuna haja ya hofu ya kupotea kwa jangili!
 
Za mwizi 40, Kama wanajua kusoma alama za nyakati nadhani watakua wameandaa wapi kwa kukimbilia...
 
Ndugu wanajamii, katika viongozi watendaji Lowassa yupo.

Tuaangalie shule za kata; hii ilikuwa ni wazo la Lowassa ili watoto wetu wasome karibu na nyumbani, baada ya kuondoka shule hizo za kata hazikuendelea kabisa,majengo yanabomoka walimu hakuna alitilia mkazo sana....hizo pesa za richmond nafikiri alipeleka huko...

Huyu ni mtu ambaye jamii yake kubwa haijasoma na alikuwa anafanya kwa watanzania wote....huyu ndie kiongozi aliyekuwa na wazo na wazo lake likawa zuri ...sio Mungai aliyearibu mitaala ya shule zetu akafuta michezo na kuleta mtaala mbovu....

Lowassa alijiuzulu kwa kitu kinachoitwa ministerial responsibility na sio kwamba ilizibitika kaiba yeye, ndugu yetu karamagi kwani mnamsikia that was a real culprit, fungueni macho, bora anaeiba na kutumia na aliyewaibia kuliko yule anaekwenda marekani kuponda raha.

Hivi huyu jamaa ni lini mtaacha kumpamba?huyu alisha haribu hawezi kusafishika kamwe,mnajisumbua tu!
EL should stay aside for now!aghrrrr
 
Baba Ju afadhali ungesema LOWASSA ni mwizi wa kuaminiwa. Tulimwamini akatuibia bila kujali umaskini wetu. Hatuhitaji mwizi aende zake.Ni MP inatosha.
 
muda mwingine tuangalie reality na tusifungwe mawazo yetu kwa tofautti za chama
 
Unajua Imran ni nani au una quote sura bila kujua maana. Dont play with holy book man, Stick to the point hapa Janvini. Mwendo wa kuwaandama mafisadi na sio dini.

Najua ninachokifanya na namjua Imran kupitia hicho unachokiamini
 
Ndugu wanajamii, katika viongozi watendaji Lowassa yupo.

Tuaangalie shule za kata; hii ilikuwa ni wazo la Lowassa ili watoto wetu wasome karibu na nyumbani, baada ya kuondoka shule hizo za kata hazikuendelea kabisa,majengo yanabomoka walimu hakuna alitilia mkazo sana....hizo pesa za richmond nafikiri alipeleka huko...

Huyu ni mtu ambaye jamii yake kubwa haijasoma na alikuwa anafanya kwa watanzania wote....huyu ndie kiongozi aliyekuwa na wazo na wazo lake likawa zuri ...sio Mungai aliyearibu mitaala ya shule zetu akafuta michezo na kuleta mtaala mbovu....

Lowassa alijiuzulu kwa kitu kinachoitwa ministerial responsibility na sio kwamba ilizibitika kaiba yeye, ndugu yetu karamagi kwani mnamsikia that was a real culprit, fungueni macho, bora anaeiba na kutumia na aliyewaibia kuliko yule anaekwenda marekani kuponda raha.

Upembuzi MajiTaka huo.

Waziri mkuu kwa dhamana yake ana uwezo wa kuchukua Fedha kwa ajiri ya Shughuli Fulani na kuzipeleka katika shughuli nyingine kwa maandishi bila kuiba. Hoja haijitoshelezi wala haileti maana kwa Waziri mkuu kuiba fedha ili afinance shughuli fulanii.

Hizo shule za Kata zimejengwa na wananchi kwa shinikizo kubwa pia watu wengi kuishia jela bila kuwa na kosa.
Watu wamenyang'anywa mifugo yao, mazao yao na kulazimishwa kufanya kazi bila ujira na CCM kuchakachua kwamba yenyewe ndo imetoa fedha. Wizi mara mbili.

Watu mnongea kwa data za kupikwa kana kwamba wajomba zenu,mama zenu wadogo na binamu zenu wote wanaishi Oysterbay.
hizo shule hata mimi nimezitolea mchango wa $200 bila hivyo Mtendaji wa kata alikuwa yuko tayari kuja kubeba dume la ng'ombe pale ushwazi kwa mdingi wangu.
Shule Wajenge wananchi Sifa apate Mwizi Lowassa na CCM yake.

Jambo lolote lile duniani, zuri au baya, linahitaji organisation.
Lowassa comperatively ni ni mzuri katika Organisation 100 times Kikwete,.Lakini amekuwa akitumia uwezo huo negatively.

Maharamia wa Mafia au Yakuza ni wazuri sana kwenye Organisation kuliko Utawala wa serikali nyingi sana Duniani.
Uwezo wao wa kuratibu mambo umewawezesha kuendesha shughuli zao kwa mafanikio makubwa.
Moja ya mafanikio Mafia ni Mikataba yetu na Makampuni ya kigeni na ya ndani katika shughuli za kiuchumi. Sasa hatuwezi kuanza kujenga hoja ya kuajiri Mafia katika utawala ili kujenga Tanzania eti kwa sababu wamefanikiwa katika shughuli zao za kimafia.

Mafanikio ya kundi la Mafia ni Maafa yasababishayo umasikini, ujinga na maradhi katika kona zote za Dunia.

Please usilete hoja yenye mnuko wa maji taka hapa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom