Lowassa ni msafi, Lakini kuna kitu hiki...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Feb 16, 2011.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,663
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 48
  Naamini watu mtaweza kukipakua na kutoa maoni yenu...

  Kumbuka: Nyaraka hizi ni za SIRI KUBWA
   

  Attached Files:

 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 19,301
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 38
  dahhh nimebanwa na pumzi..ngoja kwanza
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  thanks invissible .... wenzetu wazungu wapo very careful... unapotaka kununua au ku invest lazima wajue kama pesa hiyo umeipata kihalali na siyo kwa ufisadi .... this is a piece of work we are supposed to take into our systems
   
 4. Udadisi

  Udadisi JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2011
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,359
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 38
  "Siri Yako Usimwambie Mtu" - Freshi Ya Shamba
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,663
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 48
  Hahaha, mkuu taratibu... Nilimwangalia majuzi nikadhani bora nyaraka hizi tugawane na kulinganisha na kauli yake ya majuzi ambayo ni wazi inaashirikia mbio za kuelekea 2015
   
 6. AIZAK

  AIZAK Senior Member

  #6
  Feb 16, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  how do i open it?
   
 7. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  Yaani wanatufanya Watanzania hamnazo, na hao jamaa sijui kama tutafika
   
 8. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #8
  Feb 16, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,051
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 48
  Hii inazidi kuthibitisha kuwa Lowassa ni Fisadi wa viwango vya kimataifa. Ina maana wangekuwa wanasajiliwa, bila shaka Lowassa angekuwa fisadi wa kulipwa, tena kwenye klabu kubwa kubwa...
   
 9. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #9
  Feb 16, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,051
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 48
  Alafu kwa hela alizona nazo, badala ya kumrithisha mwanae elimu, uadilifu anamrithisha ufisadi. Hivi Huyo kijana wake tutegemee nini 'akishakomaa' kwenye hiyo tasnia... Tanzania itapona kweli!?
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,898
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Msishtushwe .....ni vijisenti tu.
   
 11. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 470
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa Lowasa mbona anajidai mmasai huku anasema kazaliwa mwanza??!!!
  AU NDO MAMBO YA UONGO ILI AWEZE KUTUCHANGANYA VIZURI??
  Hao wana laani ya nyerere
   
 12. L

  LAT JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  huyu ni Frederick Edward Lowasa..mtoto wa waziri mkuu wa zamani Edward Ngoyai Lowasa
   
 13. N

  Nanren JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,571
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 38
  Mwanaye na mama yake.
  Halafu bila aibu analeta wapambe hapa JF kumpigia debe kwa ajili ya 2015. The guy is a FISADI big time.
   
 14. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2011
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 550
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haya mambo tusubiri tuone, maana hiyo kampuni ya Integrated ni ya Wasomali ambao ni matajiri sana wana kampuni makubwa nje, lakini hebu tuangalie siri ya biashara za Wasomali kushamiri kwa kasi katika miji ya Dar es Salaam na Mombasa na hali ya sasa ilivyo, je Usalama wetu uko wapi?

  Naambiwa hawa Intergrated wanannua majumba ya watu na viwanja kwa fujo maeneo ya Kurasini karibu na bandari yetu, je, watu wa TISS mpo? Mnalijua hilo maana hata watu nyeti wamelazimika kuuza nyumba zao huko maana jamaa wanatoa Cash kwa bei utakayo wewe
   
 15. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,407
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 38
  Lowassa kashajinyea kambi mwenyewe... 2015 anapotezwa... He has the money but his dream will never be realized and as a result he will die a miserable man... And thats how life really works folks...
   
 16. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #16
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,663
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 48
  Well,

  Added part II of the so called 'SIRI KUBWA'
   
 17. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,426
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha. Angalau hivyo vijisenti wangekuwa wanaviwekeza huku huku vingesaidia uchumi wetu kwa namna fulani.
   
 18. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,122
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 38
  Ndg yangu Invisible kwa kazi yote hii nzuri uliyo fanya, pamoja na hawa jamaa wa SCD, kwa nchi kama hii ya TZ nani amvishe paka kengele. TAKUKURU wapo picha tuu si hiyo ni kazi yao??????? Tanzania tumekwisha!!!!!!!!!
   
 19. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2011
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 550
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa hiyo part II ndio kiboko, sasa Lowassa na mkewe walifanya biashara gani na hao Wasomali hadi wawadai milioni 450/= sasa hapo ndio mujue kuna kazi amewafanyia na hayo ndio malipo, na TAKUKURU waanzie hapa
   
 20. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2011
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 550
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Halafu hawa jamaa si ndio wamechukua na Nyumba ya Sanaa? nadhani na RA yumo katika hili
   
 21. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #21
  Feb 16, 2011
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 550
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Taarifa ya Lowassa kuchunguzwa balaa

  Mwandishi Wetu
  Disemba 1, 2010

  [​IMG]Raia Mwema lapata msukosuko
  [​IMG]
  Nakala 10,000 zaharibiwa zisisomwe


  HABARI iliyoihusisha familia ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, imeibua utata mkubwa baada ya kuibuka kwa vitisho vilivyosababisha kuzuiwa kuchapwa kwa gazeti la Raia Mwema toleo lililopita Namba 161 katika mazingira ya kutatanisha; huku habari hiyo ikikanushwa kwenye gazeti jingine hata kabla haijatoka.

  Utata huo ulisababisha uongozi wa Imprint iliyopo chini ya kampuni ya Jamana Printers kusitisha ghafla kuendelea kuchapwa kwa gazeti la Raia Mwema ikiwa tayari limeshachapwa nakala 10,000 katika mazingira yaliyoonyesha kuwapo shinikizo zito kutoka kwa kigogo mmoja aliye karibu na mwanasiasa huyo la kutaka habari inayomhusu Lowassa iondolewe ndipo gazeti lichapwe.

  Raia Mwema ambalo lina makubaliano maalumu na wachapaji hao lilishtushwa na uamuzi huo wa ghafla wa wachapaji hao hasa baada ya uamuzi huo kuambatana na hali ya woga mkubwa uliotawala wafanyakazi wa kiwanda hicho usiku wa Jumanne ya wiki iliyopita.

  Taarifa ya Meneja Usambazaji wa Raia Mwema, Omari Mwendapole, ambaye alikuwapo usiku huo, inaeleza kwamba hali ya uchapaji iliendelea katika hali ya kawaida kuanzia saa 11 jioni kabla ya kubadilika ghafla saa 1:30 usiku, ilipotolewa amri ya kusitisha uchapaji wakati zikiwa zimekwishachapwa nakala 10,000.

  “Tulifika kiwandani mapema saa 11:00 na hakukua tatizo lolote baada ya wahusika kukagua gazeti letu na kuridhika nalo na wakaanza taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuchoma plate saa 11:15 na saa 12:00 kazi ya uchapaji ilianza taratibu hadi saa 12:30 mashine zilipoanza kuchanganya na kutoa gazeti zuri.

  “Lakini baada ya muda kidogo, msimamizi wa uchapaji wa Imprint akaitwa na mlinzi kwenda kusikiliza simu na aliporejea akawaagiza mafundi wazime mashine kabla ya kuamua kuzima mwenyewe baada ya kuona wanachelewa kufanya hivyo.

  “Baadaye niliitwa kwa bosi wao na kuambiwa natakiwa kwenda kwa Meneja Mkuu, aitwaye Shaber, ambako nilijulishwa kwamba ni lazima habari kuu (inayomhusu Lowassa) iondolewe vinginevyo gazeti halitochapwa kabisa,” anasema Mwendapole.

  Kutokana na amri hiyo ya wachapaji, wafanyakazi wote wa Raia Mwema na watu wengine wote waliokuwamo kiwandani wakati huo waliamriwa kutoka eneo la uchapaji na kupekuliwa kuhakikisha hawabebi hata nakala moja ya gazeti hilo.

  Habari zinasema kuwa nakala 10,000 ambazo tayari zilishachapwa ziliharibiwa chini ya uangalizi mkali wa maofisa wa kiwanda hicho ili kuhakikisha kuwa haziingii kwenye soko, na hivyo habari hiyo kusomwa na wananchi.

  Hata hivyo, wakati uongozi wa Raia Mwema ukihangaika kutafuta mahali pengine pa kuchapa, ilibainika kwamba kigogo huyo pamoja na mbunge mmoja walikuwa tayari na nakala ya gazeti hilo na ilidhihirika siku iliyofuata baada ya gazeti la Mtanzania lenye uhusiano wa karibu na kigogo huyo kuchapisha habari iliyokanusha habari hizo kabla hata ya habari husika kuchapishwa.

  Katika habari hiyo, gazeti hilo lilielezea kwamba kuna taarifa “zilizochapwa katika magazeti” huku zikimnukuu Frederick Lowassa, ambaye ndiye aliyekuwa mhusika mkuu katika habari ya Raia Mwema, akijitetea kwa kudai kwamba hakuwahi kusafirisha fedha nyingine Uingereza kama ilivyoandikwa na ‘magazeti hayo.’

  Katika tukio hilo la aina yake katika tasnia ya habari, Frederick Lowassa, alisema;
  “Jamani mimi nashangaa sana. Watu hawa wanasahau kuwa mimi ni mfanyabiashara kwa zaidi ya miaka kumi sasa. Na katika kufanya biashara ni lazima nisafirishe fedha nje ya nchi kwa nia ya kununua material (bidhaa). Nasafirisha fedha sehemu mbalimbali duniani, na sijui wameliokota wapi hilo.

  “Hakuna wakati nimewahi kusafirisha paundi 495,000 nje ya nchi kwa mara moja, ila nasafirisha fedha nje ya nchi kununua bidhaa mara nyingi tu. Hili wanalozungumza la Uingereza ni kweli kati ya Machi na Aprili nilisafirisha kama Paundi chini ya 200,000 hivi, kwa ajili ya biashara kama kawaida. Benki kama kawaida walijiridhisha fedha hizo zilikotoka, tukawasiliana likaisha.

  “Sasa nashangaa watu hawa hili wamelitoa wapi? Na ifahamike kuwa mimi nafanya biashara nyingi tu, na moja ya biashara zangu ni kampuni ya Alphatel. Sisi ni mawakala wa Vodacom. Tunover (mzunguko wa fedha) yetu kwa mwezi ni zaidi ya Sh bilioni 8.0. Hizi ni fedha zinazotumiwa kama sehemu ya mtaji na faida kwa kununua bidhaa na kuuza. Sasa walitarajia mfanyabiashara kama mimi nishindwe kutumia kiasi hicho nje ya nchi? Nanunua vitu kutoka Uingereza, China, Falme za Kiarabu (Dubai), Afrika Kusini, Italia na sehemu nyingine. Watu wa ajabu kweli hawa.

  “Nasikitika jinsi wanavyoendelea kumchafua mzee wangu. Na ndio maana nimeelewa barua hiyo ya mwaka jana imeletwa leo wiki hii. Tayari nimewasiliana na mwanasheria wangu katika hili na nitatoa vielelezo vyote, hakuna cha kuficha…. Jamani siasa zao wazibakize huko, kazi waliyofanya kumchafua mzee wangu (Lowassa) hawajaridhika kweli? Katika hili nasema hapana.”

  Habari hiyo ilifuatiwa na habari nyingine ambayo iliyomnukuu Lowassa mwenyewe akionyesha kwamba Lowassa anaandamwa na katika toleo hilo aligusia tena kuhusu mwanae Fredrick kuchukua hatua za kisheria kuhuhusiana na habari inayohusiana na usafirishaji fedha Uingereza. Habari hiyo imenukuliwa tena katika gazeti lingine jana.

  Uongozi wa Raia Mwema tayari umeiandikia barua kampuni hiyo ya uchapaji ukilalamikia tukio hilo la kuzuia gazeti lisichapwe na kuharibu nakala ambazo tayari zilishachapwa, na pia kutoa usiku huo huo baadhi ya nakala za toleo hilo kwa watu wa nje bila idhini ya wamiliki wa gazeti. Pia unataka ulipwe fidia kwa hasara iliyopatikana kwani ililazimu gazeti kuchapwa kwingineko alfajiri, na hivyo kuchelewa kuingia sokoni.

  Katika habari yake ya wiki iliyopita iliyoibua mambo yote hayo, Raia Mwema liliripoti kwamba Frederick Lowassa anacunguzwa na Kitengo Maalumu cha Polisi wa Kimataifa wa Uingereza wanaofuatilia utata wa uhamishaji fedha kutoka Tanzania.

  Fedha hizo zinahusishwa na ununuzi wa nyumba yenye thamani ya pauni za Uingereza 475,000 (takriban Shilingi bilioni moja) katikati ya Jiji la London.

  Hata hivyo, watu walio karibu na Frederick wameelezea kwamba kijana huyo hakuwahi kununua nyumba; bali aliwahi kutaka kupanga kwa ajili ya kuishi akiwa masomoni nchini Uingereza na fedha nyingine alizituma kwa ndugu yake aishie nchini humo.
  Nyumba ambayo inatajwa katika maelezo ya awali iko mtaa wa Leinster Gardens, jijini London.

  Hata hivyo, hakuna ofisa yeyote wa Serikali ya Tanzania aliyekuwa tayari kuzungumzia suala hilo, pamoja na kuwapo taarifa kwamba tayari vyombo vya dola vya Tanzania vimekwisha kuhusishwa katika uchunguzi huo.

  Maofisa wa Polisi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (CID) wanaohusika na uchunguzi wa fedha haramu, wamekwepa kuzungumzia suala hilo na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba, hakuweza kupatikana, na alielezwa kuwa nje ya nchi kikazi.

  Ofisa wa CID aliyeelezwa kuongoza kitengo kinachochunguza makosa ya uhalifu wa fedha na nyaraka, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Samson Kasala, alikanusha kufahamu chochote kuhusiana na suala hilo, kabla ya kukata simu alipohojiwa na Raia Mwema kuhusu taarifa hizo.

  Taarifa zinaeleza kwamba Kitengo cha Ufuatiliaji wa Fedha Haramu (Financial Intelligence Unit-FIU) kilichopo chini ya Wizara ya Fedha nchini, kilipokea taarifa kutoka Polisi wa Kimataifa wa London, Uingereza, wakitaka taarifa muhimu kuhusiana na Frederick, kabla ya kitengo hicho kuomba msaada wa polisi.

  Hata hivyo, Kamishna wa FIU, Herman Kessy, hakutoa ushirikiano na Raia Mwema, kuhusiana na sakata hilo.

  FIU imeanzishwa chini ya Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu ya mwaka 2006 (Anti-Money Laundering Act-2006) kwa kuundiwa kanuni mwaka 2007, lakini hadi sasa kitengo hicho kimekuwa kikiendeshwa na maofisa watano tu, Kamishna Kessy, mchambuzi mmoja, mtaalamu wa mawasiliano na wasaidizi wawili wasio wataalamu, kitengo kilichopaswa kuendeshwa na watu wengi zaidi kutokana na unyeti wake.

  Habari zinaeleza kwamba hata ofisa wa Polisi aliyewahi kuhamishiwa FIU kwa kazi maalumu alijikuta akitengwa na kutopangiwa kazi na maofisa hao ambao wengi wanatoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), baada ya kuwa ‘wameaminiwa’ sana na uongozi wa juu wa serikali.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo bado zinafanyiwa kazi, Frederick ambaye baba yake alijiuzulu Waziri Mkuu kwa kuhusishwa na kashfa ya ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme iliyokabidhiwa kwa kampuni tata ya Richmond Development LLC, anadaiwa kufanya mawasiliano kupitia kampuni ya uwakala iliyotajwa kwa jina la ‘Mishcon’.

  Nyaraka alizowasilisha, zilidai kuwapo ubia kati ya mtuhumiwa huyo na kampuni tatu ikiwamo Integrated Property Investment(T) Ltd na Barare Ltd Company.

  Mkataba huo unaonyesha kuwa Frederick Lowassa ana hisa kwenye kampuni hizo, na kwamba fedha za ununuzi wa nyumba hizo zinatokana na fedha za malipo ya hisa anazopata kutokana na kampuni hizo.

  Hata hivyo, mkataba huo unaonyesha kusainiwa Machi 25 mwaka 2009 siku moja baada ya Frederick Lowassa kusaini mkataba kati yake na kampuni ya Mishcon kama wakala wake katika ununuzi wa jengo hilo.

  Pia aliwasilisha nyaraka zinazoihusisha kampuni ya Alphatel kama moja ya kampuni ambayo pia yeye ni mkurugenzi wake ambayo pia ni chanzo chake kingine cha fedha anazotumia kununua jengo hilo.

  Taarifa zimedokeza kuwa ununuzi huo ulikwama baada ya kushindwa kutoa malipo hayo kwa mujibu wa mkataba kati yake na wakala wa ununuzi wa nyumba hiyo (kampuni ya Mishcon) ambao ulimtaka awe amekamilisha kulipa fedha hizo kabla ya Aprili 14, mwaka 2009.

  Hata hivyo, siku chache baadaye ndani ya mwezi huo wa Aprili, Frederick aliipelekea Mishcon kiasi cha pauni za Uingereza 199,940 zikitokea kwenye kampuni ya ununuzi fedha ya Wall Street Exchange.

  Aidha kiasi cha pauni 100,000 kiliingizwa kwenye akaunti ya kampuni hiyo hiyo ya Mishcon kwa fedha taslimu katika mikupuo 12 tofauti zikitokea kwenye matawi tofauti ya benki ya NatWest Bank plc iliyoko Kaskazini mwa Jiji la London.

  Raia Mwema limeelezwa kuwa mazingira ya kuingizwa fedha hizo kwenye akaunti ya wakala huyo ( Mishcon) ndiyo yameifanya Taasisi ya SCD 6 Economics and Specialist Proceeds of Corruption Unit ya Uingereza inayosimamia uchunguzi wa sakata hilo kuwa na mashaka makubwa kuhusu uhalali wa fedha hizo.

  Kutokana na mazingira hayo, SCD 6 Economic and Specialist Crime Proceeds of Corruption Unit yenye ofisi zake Victoria Block, New Scotland Yard, London, ililazimika kuwasiliana na FIU ikitaka maelezo ya awali kuwezesha kufanyika kwa uchunguzi kuhusu fedha hizo.

  Raia Mwema iliwasiliana na Fred ambaye alikana kununua nyumba Uingereza lakini alikiri kuwahi kutuma fedha huko. Aliliambia Raia Mwema pia kwamba hajawahi kuhojiwa na yeyote kuhusu suala hilo, na pia kwamba hana taarifa kuwa polisi wa Uingereza wanampeleleza.

  Hata hivyo kwa upande mwingine, gazeti hili limebaini kuwa, maelezo ya awali ambayo yalitakiwa kutoka Tanzania na makachero hao wa Uingereza, ni pamoja na kutaka kufahamu kama kweli Frederick Edward Lowassa amezaliwa Agosti 26, 1977, Mwanza Tanzania na anamiliki hati ya kusafiria yenye namba AB 109402 iliyotolewa Tanzania na kwamba anwani yake nchini Uingereza ni 71 Hendrix Drive, Milton Keynes, MK8 0DY.

  Pia makachero hao waliitaka Serikali ya Tanzania kutoa ufafanuzi wakitaka kujua kama Frederick Lowassa ni mbia katika kampuni za Alphatel Partnership (Tanzania) Barare Ltd na Intergrated Tanzania Limited, kampuni ambazo zimefahamika kumilikiwa na familia ya Lowassa.

  Asasi hiyo ya Uingereza pia imeomba kujua kama FIU wana taarifa zozote za uhalifu dhidi ya Frederick Lowassa na kama baba yake Edward Lowassa anachunguzwa kwa tuhuma yoyote ya rushwa na mamlaka za uchunguzi wa rushwa nchini Tanzania kuhusu fedha haramu.

  Uchunguzi wa awali uliofanywa na vyombo vya dola, ulielezwa na taarifa hizo kwamba Frederick Lowassa si mbia katika kampuni hizo na kwamba Barare Ltd wenye hisa ni Edward Ngoyai Lowassa mwenye hisa 500 na Regina Mumba Lowassa mwenye hisa 500 huku wakurugenzi wakiwa ni hao hao.

  Ofisa wa Uingereza anayesimamia uchunguzi huo, George Simpson, ameliambia Raia Mwema kupitia barua pepe kwamba kanuni za uchunguzi kuhusiana na kesi zenye mguso wa kisiasa huwazuia kukanusha au kuthibitisha kuhusu uchunguzi unaoendelea hadi pale wanapofikia hatua ya kukamata mtuhumiwa ama anapofikishwa mahakamani.

  Taarifa ambazo gazeti hili limezipata mwanzoni mwa wiki hii kutoka vyanzo vyake zinasema kwamba uchunguzi wa suala hilo bado unaendelea, na kwamba watendaji wamepewa maelekezo ya kuendelea nao.
   
 22. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #22
  Feb 16, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Barare wanapewa 7500 shares wakati kampuni Integrated proper... ime register share 1000!!!
   
 23. Simbajr

  Simbajr JF-Expert Member

  #23
  Feb 16, 2011
  Joined: Apr 1, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  DUh!! Nice Job Fredrich Edward Ngoyai Lowassa!!
  Like Father like Son
   
 24. genekai

  genekai JF-Expert Member

  #24
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 10,585
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 48
  What? Nipe muda nizipitie nitarudi!
   
 25. K

  Kambarage Member

  #25
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eti Lowassa ni msafi??! Mwizi mkubwa huyu. Subirini akirithishwa Urais na Kikwete 2015 mtaona atakavyojilimbikizia mali (in billions of US dollars) kama Hosni Mubarak wa Egypt. Ana tamaa kubwa sana ya utajiri huyu.

  LOWASSA has an insatiable appetite for political and economic power.
   
 26. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #26
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  Mwaka huu tutaona mengi.................................. Halafu anamsema Mubarak kwa kujilimbikizia mali, lakini ametuzindua Watanzania kwamba kuna viongozi akiwamo yeye ambao wametumia madaraka yao kujitajirisha
   
 27. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #27
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,539
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ina maana kuna mtu alikuwa na mashaka kwamba jamaa ni fisadi au laa? Mimi nadhani ambacho kilikuwa hakijulikani ni kiwango chake cha ufisadi kama kinafanana na Mubarak wa Misri au la! Kwa kweli huyu bwana hatufai na kama alidhani watanzania ni mbumbumbu sasa aelewe kwamba ukimya wao siyo ukondoo na sasa nadhani ajiandae kuvuliwa nguo kwa dhambi alizodhani ni siri yake yeye na washirika wake tu.

  Eti mtu huyu ndiyo anjifanya kutoa angalizo! Hana aibu.

  Yote anayoyafanya na kujilimbikizia kote huko, kwao monduli wananchi wake ndo wanaongoza kwa kufa njaa na kutembea umbali mrefu kusaka maji na malisho. Baba urais wako ni huko huko monduli huku marufuku!
   
 28. m

  mapambano JF-Expert Member

  #28
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alianza safari yake ya kujisafisha ..mara leo mgeni rasmi kwenye gospel music, mara ndio mwenyekiti wa mambo ya nje...mara anasema Hosni ni mchafu sana kwa kujilimbikizia mali ...
  Huyu hafai hata kuwa katibu kata...mwizi tapeli mkubwa!!
   
 29. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #29
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,539
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Invisible endelea hivyo hivyo na Mungu atakujaalia. Hivi ni vita vikubwa na kwa hakika vinahitaji makamanda kama wewe ili wale wanaokuja humu jambvini na kuanza kuwapamba hao mafisadi na kudai wanasingiziwa waone aibu maana kila kitu kinakwenda kwa takwimu tu! Basi utaona baada ya muda wanaibuka watu wa ku-divert attention ili watusahaulishe. Huyu jamaa ni jizi!
   
 30. P

  Proud Patriot JF-Expert Member

  #30
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 208
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i guess ndo hao hao wana appartments za kukodisha kule bahari beach and plenty more space imebaki to be turn into gigantic luxurious appartments!
   

Share This Page