Lowassa ni kiona mbali

Lowasa ndio jembe la CCM, Richmond mwizi alikuwa Kikwete, Lowasa alibebeshwa aibu kulinda heshima ya nchni.

Ndugu yangu chonde chonde chonde! Usidhani tumezaliwa leo. Kama wewe ulikuwa mtoto wakati kashfa hii inatokea, au kama wewe hukuwa na akili timamu au ulikuwa jela kipindi hicho, tuache tuliokuwepo tena tukiwa na akili timamu tutafakari njia nzuri ya kumwadhibu mwizi wetu huyu, maana hadi sasa amekaa mkao wa kusubiri adhabu laini wanaotakiwa kumuadhibu wameshiba dini na sasa wanaona kama vile ni dhambi kumtia adabu. Kitendo hiki cha kumuacha huru ndicho kinachotumiwa na hawa akina Yuda waliotapakaa pote nchini wakidai kuwa hakuhusika. Mungu bahati ametuonyesha katika makashfa mengine anavyoendelea kutoboa hazina ya nchi hiyo hiyo ambayo leo anajifanya kuipenda na kuihurumia.

Hivi kazi ni urais tu? Atuache tupumue na kutafakari mustakabali wa taifa hili! Kila tukijipanga kufanya la maana aliowakodi kumtakasa wanaibuka na hoja tasa ambazo ni kichefuchefu. Huyu bwana maekuwa mbunge toka 1990 na jimbo lake ni miongoni mwa majimbo yanayoshika mkia kielimu. Kwa nini asiwapeleke private schools badala ya kutoa suluhisho la kinafiki na lenye nia ya kuendelea kuifilisi hazina yetu. Maskini populist huyu! Na wapambe wake wanacheka tu na huku wanampotosha!
 
Lowasa ndio jembe la CCM, Richmond mwizi alikuwa Kikwete, Lowasa alibebeshwa aibu kulinda heshima ya nchni.

Maskini huyu baba, kila analolishika linamponyoka. Hii inanikumbusha ule wimbo wa taarab kwamba nyama ikifika bucha hairudi kuwa ng'ombe. Alipokuwa anahujumu alijiona mjanja kwa kudhani watu hawatamuona au watasahau kirahisi kumbe wapi!

Sasa hivi yamemgeuka na gharama anazozitumia kujisafisha ni kubwa sana, na kwa bahati mbaya zinapotelea baharini kwani hakuna anayejisumbua kumsikiliza. Wananchi walishatoa hukumu na sasa wanasubri tu kutoa adhabu, na hii itatokea 2015 kule kizota. Tembea kwa magoti uombe msamaha kabla halijakuchwea maana sisi hatujakusamehe wala kukusahau baba kwa mateso uliyoyaleta. Hivi ile mvua ya Thailand ulikuwa utuuzie kiasi gani vile?
 
Ni kiongozi makini sana. Ana upeo mkubwa sana wa kufikiri na kutenda. Anathubutu na anawapenda watu wake. Majuzi akiwa katika kijiji cha Lolkisale Monduli Lowassa alisema yeye akiwa mbunge anakusudia kuliomba Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA) ililiwaruhusu wanafunzi waliofeli kidato cha nne warudie mitihani. Kweli, Monduli wamepata kiongozi. Taifa linahitaji akina Lowassa wengi.Kama Lowassa, ninaamini kuwa ELIMU KABLA.....

Nimepita ghafla wakuu. Ila bado natia msisitizo ya kwamba:
Japo kugombea au kutogombea ni haki ya msingi ya kila mtu,, lakini uongozi unahitaji sifa nyingi. Na nyingi kati ya hizi Mh. Lowassa anazo kama uchapakazi na uthubutu au alivyosema muungwana hapo juu. Lakini pia kuna sifa nyingine ya kuona mbali kama alivyokuwa Mwalimu Nyerere. Sasa hii ndiyo sifa anayopungukiwa Mh. Lowassa. Alama za nyakati hajazijua kuzisoma huyu. Kwa mtu anayeipenda Tanzania na mzalendo wa kweli na angeona mbali basi Mh. Lowassa asingethubutu hata kufikiria kugombea Urais. Ndiyo!!! Kwa sababu kufanya hivyo ni kutoitakia mema Tanzania ambapo machafuko makubwa yanaweza kutokea kwa vile watu wana hasira sana na haya wanayoyasikia kila kukicha,, basi tu hawajapata kianzio. Mimi siyo CDM ila nasema ukweli tu kwamba huu si wakati wa kuchezeachezea amani ya nchi kwa kujaribisha jambo hili. Ni sawa na kuwasha kiberiti palipo gesi,, ndivyo itakavyokuwa. Wakongo wanasema kwamba kama unatembea na umebanwa sana na mkojo na hakuna pa kujisaidia karibu,, basi mvua ikinyesha NDIYO WAKATI MZURI WA KUJIKOJOLEA. Maana yake hapa ni kwamba wananchi wengi wana hasira, ni kama wamebanwa mkojo,, sasa kitendo cha Mh. Lowassa kuwa Rais ndipo mvua itakaponyesha.
Naenda lunch nitarudi.
 
OGOPA M2 ALIYEONA LOOP ZA KUIBA NA AKAZITUMIA KUPORA MALI YA UMMA WAKATI WA NYERERE. Lowasa aliziona na kuzi2mia wakati wa uongoz makini sasa iv anaona kila sehem ni wazi chin ya selikali zembe kama hii!
 
Kama nikiulizwa nani bora kati ya Lowasa na Kikwete nitasema Lowasa kwa sauti kubwa kabisa na nitatoa ushahidi thabiti, pia nitamwita Dr. Mwakyembe atoe maelezo ya nyongeza juu ya kashfa ya Richmond kwa yale aliyosema ameficha ilikuepusha kudhalilisha serikali.

Kwahiyo kwa mtizamo wangu yeye ndio Jembe la CCM, maana amekubali kudhalilika juu ya wizi uliofanywa na CCM chini ya Kikwete bila kulalamika, unadhani kuna mtu angelikubali hilo, ni watu wachache sana wanaweza kukubali kubeba lawama lukuki ambazo siyo zao peke yako na wakaakimi. Lowasa angelitaka kuangamiza CCM angeliweza ndani ya 24hours, maana anajua siri zote jinsi Kikwete alivyoshiriki katika wizi tangia EPA Kagoda hadi Richmond ila kamezea "Funika kikombe mwanaharamu apite".

Kama Lowasa hasingekubali kubeba lawama peke yake Serikali ya Kikwete ingeng'oka yote maana Lowasa angetoboa siri zote na kukataa kujiuzuru mpaka Bunge litoe adhabu kwa wezi wote!! ambao ni wazi wezi wetu wote ni CCM ikiongozwa na Kikwete. hapo ndipo mjue umuhimu wa Lowasa kwa CCM hasa Kikwete, hamuoni anapewa cheo chotechote anachotaka! yeye ndio kamuweka yule Bi Kizee kuwa Spika na kachagua akamate Kamati muhimu ya Usalama sasa hamuoni hayo yote kuwa yeye ndio Jembe la CCM na hasa CCM ya Kikwete?

Bravo Masai bin Mchagga AkA Lowasa au EL kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa na kuokoa serikali ya Kikwete na kuisaidia imalize muda wake.
 
Ni kiongozi makini sana. Ana upeo mkubwa sana wa kufikiri na kutenda. Anathubutu na anawapenda watu wake. Majuzi akiwa katika kijiji cha Lolkisale Monduli Lowassa alisema yeye akiwa mbunge anakusudia kuliomba Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA) ililiwaruhusu wanafunzi waliofeli kidato cha nne warudie mitihani. Kweli, Monduli wamepata kiongozi. Taifa linahitaji akina Lowassa wengi.Kama Lowassa, ninaamini kuwa ELIMU KABLA.....
Umetumwa wewe, huna hoja ya msingi. Kwani wakati yeye akiwa waziri mkuu wanafunzi walikuwa hawafeli? Kwa nini hakuliagiza Baraza la Mitihani liwe linawaruhusu wanaofeli kurudia mitihani? Lowassa alishachafuka hata ukimpeleka kumsafisha mto Yordan walikokuwa wanatakasika wakoma enzi zile EL hawezi kutakasika. Ujumbe kwako ndio huo.
 
Ni kiongozi makini sana. Ana upeo mkubwa sana wa kufikiri na kutenda. Anathubutu na anawapenda watu wake. Majuzi akiwa katika kijiji cha Lolkisale Monduli Lowassa alisema yeye akiwa mbunge anakusudia kuliomba Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA) ililiwaruhusu wanafunzi waliofeli kidato cha nne warudie mitihani. Kweli, Monduli wamepata kiongozi. Taifa linahitaji akina Lowassa wengi.Kama Lowassa, ninaamini kuwa ELIMU KABLA.....[/QUOTE

Tigo wewe!!!
 
Ni kiongozi makini sana. Ana upeo mkubwa sana wa kufikiri na kutenda. Anathubutu na anawapenda watu wake. Majuzi akiwa katika kijiji cha Lolkisale Monduli Lowassa alisema yeye akiwa mbunge anakusudia kuliomba Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA) ililiwaruhusu wanafunzi waliofeli kidato cha nne warudie mitihani. Kweli, Monduli wamepata kiongozi. Taifa linahitaji akina Lowassa wengi.Kama Lowassa, ninaamini kuwa ELIMU KABLA.....
Lowasa aliyejiuzuru upm au?? Huyu huyu Lowasa rafiki wa Rostam! Akili yako ipo sawa lakini!!??!
 
Ni kiona mbali kwa kutafuta BIG DEALS za ma-cent kwa ajili yake na marafiki zake ambao hawakutani barabarani
lakini si kwa UONGOZI WA TAIFA.tunahitaji kiongozi
makini anayejua UCHUNGU wa maisha yanayowakabili raia
wake kwa undani na si wa kusomewa risala.
Shule za kata ndio ilikuwa mashiko yake kwenye (come-pain)kampeni zilzopita.sasa zimethibisha sera za kukurup
uka tayari ameona mbali maswali magumu 2015!!
"~UNAWEZA KUNUNUA CHEO, LAKINI HUWEZI KUNUNUA HESHIMA~
"
 
Kwenye hili la shule za kata, kwanza walikamata kuku na kuezua mabati ya nyumba za wananchi maskini kujenga shule wakati mabilioni waliyoiba RICHMOND na dili nyingine za kifisadi yangeweza kujenga shule hizi bila michango ya kiporaji toka kwa wananchi maskini. Pili imethibitika shule hizi zimekaa kisiasa zaidi. Matokeo ya Form 4 yamedhibisha ni majengo na idadi wanafunzi bila elimu.
 
Mko wengi sana mliotumwa kuja kupiga kampeni JF....wengine wamesambazwa wapi?Hapa mmeingia chaka....

We ni mgumu kuelewa inawezekana ulizaliwa kuwa kizazi cha utumwa! mtoto wa mtumwa akili yake mara nyingi uganda kama barafu Pamoja na kusoma hiyo hoja umeambulia zero nadhani hata darasani ndivyo ulivyokuwa.
 
Mafisadi papa na dagaa nawashauri mtumie gazeti la RAI kumsafisha EL
Tutajitokeza kwa wingi kulinunua
Hapa mtakuwa mnapoteza mda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom