Lowassa nenda Igunga kama wewe msafi

Mi naona siku zinavyo kwenda watanzania wanazidi kurudisha imani yao kwa mwizi wa rasilimali zetu na mmoja kati ya waliotuingiza kwenye mikataba mibovu inayo tutesa hadi leo. Lowa$sa ni mmoja kati ya walio asisi matatizo ya umeme na mfumuko wa bei, lakini nasikitika sana kuna watu wasio wazalendo walio huku jf wanamsafisha! Pengine wanalipwa lakini mlaaniwe wote mnao potosha ukweli watoto wetu watawalaani kwa kuwaachia nchi isiyo na kitu, mmeuza kila kitu kwa wageni kwa manufaa yenu binafsi, hakika mungu hatawaacha!
Hakuna anayerudisha imani kwa mwizi lakini so far kuna watu wanaotaka tuamini kwamba shutuma zote anazotupiwa Lowassa ni uzushi mtupu, basi ni kwa nini asiende Igunga ambako kundi kubwa la wale wanaomtuhumu wako huko? lengo letu hatutaki tuishi kwenye Polemical Politics za wale wengine wanasema huyu ni fisadi na wengine wanatuambia T.B Joshua katabiri huyu jamaa mtake msitake atakuwa rais wenu mwaka 2015.

Huwezi kumtumia mchezaji wako kwenye vyumba vya kubadilishia nguo (Vikao vya chama) bali uwanjani (Kwenye chaguzi) ambako ndiko mechi zinachezwa. Mechi ya sasa iko Igunga!!
 
Mwenyewe anapinga ciasa uchwara,hawezi kuambatana na wenye upeo mdogo wa kujidhalilisha wenyewe,ana maamuzi magumu yasiyo makini
 
Yeye mwenyewe yupo katka wakati mgumu, maana gamba mwenzake kaweza livua gamba yeye anasubiri avuliwe kwa hiyo hajui atoke vp?
 
Tarehe 3 mwezi October 2011 watanzania kuvaa nguo nyeus kulaani utendaji wa serikali kama kama unaguswa na mambo yafuatayo basi na wewe vaa na umwambie na mwenzako kama yana muhusu naye avae.
1.ukosefu wa ajira
2.kupanda kwa gharama za maisha
3.huduma mbaya za afya, elimu na maji.
4.ukosefu wa umeme
5. Ufisadi
6.mikataba mibovu
7. Ubaguzi kwenye mikopo ya elimu ya juu
8.malipo duni ya wafanyakazi wa serikali
9.ufujaji wa mali ya umma kwa watendaji wa serikali kwa safari zisizo na tija.
10. Kuwakumbatia wawekezaji katika kuiba ardhi na rasilimali ya wanyonge

Huu ni ujumbe unao zunguka kwenye Mitandao ya kijamii twitter, facebook na myspace pia sms kwa njia ya simu zimeanza kusambaaa nchi nzima. Kama Mod hatabania hii kitu na sisi wana JF tuchangia hapa.
 
kabla ya kwenda aende kwa mama rwakatare akaombewe,ya kutafuta mvuto wa kugombea urais si alikwenda nigeria
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom