Lowassa na Mulugo, si lazima muongee kiingereza!

Sio kwamba hawajui Kiingereza hawana matumizi nacho kwa asilimia zaidi ya tisini kwa muda wote wa maisha yao, lugha inakuwa, na inakufa, kama huitumii lazima huwezi kuwa na misamiati ya kutosha, lafudhi sio hoja sana kwani hata waingereza wana lafudhi tofauti kati ya sehemu na sehemu au na wamarekani nk.

Ama tuanze kujifunza kiingereza kuanzia darasa la kwanza na kiwe ni kwa masomo yote ili tuwe na misamiati ya kutosha la sivyo tutaonekana vituko siku zote tukizidi kkuking'ang'ania . Wapo wengine kichwa ni patupu hata wakiongea kimatumbi na wako ambao wana make sense ila lugha ndio inawachanganya.
Mkwawa,JK acha alipokuwa waziri wizara za fedha na kule Nishati,lakini kawa Foreign kwa miaka 10 na kila siku anakutana na watu wazungumzao lugha hiyo.Acha hii miaka 7 ya upresida ambayo siku nyingi amekuwa nje na kutumia lugha hiyo. Tatizo ni nini kama lugha unaitumia sana halafu kigugumizi? Tatizo ni kuwa kama lugha inakutatiza waweza kutofikisha ujumbe uliokusudia hivyo kutotimiza azma yako
 
Kiingereza ni cha waingereza wala haaimananishi kwamba kukijua ndiyo una uelewa mkubwa...mbina kuna wanajua kiingereza sana lakini hawajui kusoma wala kuandika??? Ninadhani tuwashangae sana wasioweza kujieleza sawasawa kwa kiswahili......mnajichosha bure.....mnafikiri kwa kutumia kiswahili halafu mnataka mtoe mawazo yenu kwa kiingereza......ni utumwa nao pia
 
nilijua nikiwagusa viongozi wa chadema tu hoja itaanza kulainishwa,haya kaka hatutawaweka hapa zitto anatosha..
 
Ukweli husemwa:

Watanzania wengi walio na shahada ya juu wana uwezo wa hali ya juu katika kuandika kwa lugha hii ya kiingereza lakini pia wana uwezo mdogo wa kuiongea kwa ufasaha. Wazungu wanasema 'practice makes perfect'. Kuna wengine inaweza ikapita wiki nzima bila kuongea hata sentensi moja ya kiingereza pamoja na kufanya kazi ofisini huku wakiandika barua na report kwa lugha ya kiingereza. Ni vigumu kuongea lugha yoyote ile kwa ufasaha kama hufanyi mazoezi ya kuiongea.

Watanzania wengi kwa sasa ni magwiji wa kuongea katika kiswaenglish. Wengi kwa sasa hata kiswahili hawawezi kuongea kwa ufasaha, kiingereza ndiyo basi kabisa. Na pale wanapotakiwa kuongea kiingereza tu, kutokana na mazoea ya kiswaenglish, wanaanza kubadilisha kwa kufikilia kwanza sentensi ya kiswahili kuwa ya kiingereza, na hapo ndipo tatizo linajitokeza.

Sipendi lugha ya kiingereza kuwa kama ndiyo kigezo cha kuwapima wanasiasa wetu lakini vilevile ni muhimu kama maisha yao ya kisiasa kwa sababu muda mwingi wako katika majukwaa. Kutokana na mapungufu ya mtililiko wa lugha wakati mwingine hata ujumbe haufiki inavyodhamiliwa.

Kwa vile umeanzisha thread basi waweke wote ili tuwasikilize. Itakuwa siyo kuwatendea haki wanasiasa uliowaweka kama wengine hautawaweka ili jamii janvini pia iwasikilize.

Kama umeweza kuwaweka hawa bila kuiuliza jamii janvini, kwa nini unaiuliza ili kuwaweka Dr Slaa na Mbowe. I'm sorry, Unaonekana kama kuna bias fulani katika ujumbe wako.
 
Mkwawa,JK acha alipokuwa waziri wizara za fedha na kule Nishati,lakini kawa Foreign kwa miaka 10 na kila siku anakutana na watu wazungumzao lugha hiyo.Acha hii miaka 7 ya upresida ambayo siku nyingi amekuwa nje na kutumia lugha hiyo. Tatizo ni nini kama lugha unaitumia sana halafu kigugumizi? Tatizo ni kuwa kama lugha inakutatiza waweza kutofikisha ujumbe uliokusudia hivyo kutotimiza azma yako

zitto nae amekua waziri wa mambo ya nje kwa miaka ingapi labda?kwanini hatupendi kukubali tu kwamba wengi wetu tuna udhaifu na kufanya jitihada za kuuondoa kama tunapenda kukitumia,kujifanya hakina mpango huku kimtindo tunapenda kukitumia ni kujidanganya
 
Wekeni na bi mkubwa wa mjengoni bi........... na tyson wassira tumsikie, msisahau na lema
 
Mkwawa,JK acha alipokuwa waziri wizara za fedha na kule Nishati,lakini kawa Foreign kwa miaka 10 na kila siku anakutana na watu wazungumzao lugha hiyo.Acha hii miaka 7 ya upresida ambayo siku nyingi amekuwa nje na kutumia lugha hiyo. Tatizo ni nini kama lugha unaitumia sana halafu kigugumizi? Tatizo ni kuwa kama lugha inakutatiza waweza kutofikisha ujumbe uliokusudia hivyo kutotimiza azma yako

Kutembea nchi za nje sio kutumia lugha zao, Jk kaenda sana nje ila hajaishi nchi zinazoongea Kiingereza, Lugha lazima ujifunze na uitumie kwa muda mrefu ili uweze kumudu maneno na kucheza nayo. Sikiliza wote mliowaweka kwenye video kila mmoja anahangaika na lugha hii ya kiingereza. kumjua mtu anahangaika kutafuta maneno angalia wanavyokwamwa au kutumia neno moja mara zaidi kumi.

Tatizo letu tunakataa ukweli, mtanzania ambaye ameishia form akaenda nje kama uingereza akaishi huku kwa miaka kumi akiongea kiingereza utamwona anatofauti kubwa na wengi hata waliosoma zaidi yake. Kenya wanaomisamiati mingi kwa sababu wanasoma kiingereza tangia darasa la kwanza na masomo yao karibu yote yanatolewa kwa kiingereza. Sisi tunatumia kiswahili kwa asilimia zaidi ya 90 kwenye maisha yetu. JK akisafiri anasafiri na wasidizi wake zaidi ya kumi hata akiwa nje anatumia kiswahili isipokuwa muda kidogo sana akiwa na wageni wasiojua kiswahili.

Raisi wa Iran, Venezuila, Rusia nk wanajua Kiingereza ila hawakubali kuvitumia kwenye maswala ya kimataifa kwani watakosa misamiati ya kuwakilisha wayatakayo kama wanavyotapenda hivyo hutumia wakalimani kutafsiri wanachoongea.

Lazima tuamue tuanze kufundisha watoto wetu kiingereza kuanzia darasa la kwanza kama lugha ya biashra na kazini na kiswahili kibakie lugha ya taifa.

Ukijaribu kuangalia wote waliozungumza wanazungumza kwa tabu sana na wanatafuta maneno hawako free kama kiswahili. Wengine ni tabu hata kukisoma. Mkapa yeye anajitahidi sana ila tofauti yake kubwa na wengine anaonekana hajawahi kukurupuka huwa anajiandaa kwa presentation zake nyingi.

Chief Mkwawa wa Kalenga
tatizo letu ni mfumo wa elimu na kuchagua faida za taifa.
 
Mbona Ji Ntao wa china haongei kiingereza..mbona Ahmadinejad haongei kiingereza.?acha umbumbumbu
 
Wachina wametukuza lugha yao sana,ukienda nchi za kiarabu hawapokei mkataba wowote kama haujaandikwa kwa lugha ya kiarab,wala barua yyte kwenda wizara yeyote lazima iandikwe kwa lugha yao,maana yake wanataka waelewe vizuri nini kimeandikwa,lakini sisi wanasaini hata vipengele kibao hawajaelewa kwa sbb lugha sio yetu,bora tungetumia kiswahili tu
 
To do you do you
to say you say me

If you hear your name and you think you are hear, please come forward this time!! Huyo alikuwa Mwl. wa Zamu wa Kihaya akiwapiga mkwala wanafunzi ambao walikuwa wamechelewa kufika shuleni. Maneno hayo alikuwa akiongea akiwa na fimbo ndefu na nene mkononi.
 
...... kwenda wizara yeyote......

Hata Kiswahili nacho ni patashika. Hakuna kitu kinachoitwa "wizara yeyote". Neno YEYOTE lina-describe kitu chenye uhai na utashi fulani. Kwa mfano, ni sahihi kusema "mtu au mnyama yeyote". Huwezi ukasema "mti yeyote" badala yake utasema "mti wowote". Kwa hiyo, ulitakiwa useme "wizara yoyote" badala ya "wizara yeyote". Kama ungesema "waziri yeyote" ungekuwa sahihi kwani tayari subject umeiobgezea uhai na utashi. Hopefully, it is now clear.

Thanks!
 
Mimi nadhani sio sahihi kabisa kuwabeza watanzania kwa kigezo cha lugha yoyote ya kigeni.
Ufahamu na Uwezo binafsi wa mtu kuhusiana na mambo mbalimbali havina uhusiano na uwezo wako wa kutumia lugha za kigeni.
 
Hongera wanajamvi kwa udadavuzi. Itapendeza kama tutajijenga kwa lugha yetu kama walivyo wachina.
 
Mbona Ji Ntao wa china haongei kiingereza..mbona Ahmadinejad haongei kiingereza.?acha umbumbumbu
Nadhani ni kwa kuwa hakijui na wala hakipapatikii sasa kama ni hivyo mbona hawa wanasiasa wetu kama hawa kina lowassa na mulugo wanaking'ang'ania bila sababu za msingi
 
lakini kwanini wanaking'ang'ania,mh lowassa mfano jinsi ambavyo hayuko comfortable na hiyo lugha,ni wazi aliandika mahali kwanza then akajikaririsha kutwa nzima

Lowasa nishamsikia akivunja yai mara 1 tu, ile siku anasulubiwa bungeni:
"There is a wish which i am going to grant, ni Uwaziri Mkuu"
 
Mimi nadhani sio sahihi kabisa kuwabeza watanzania kwa kigezo cha lugha yoyote ya kigeni.
Ufahamu na Uwezo binafsi wa mtu kuhusiana na mambo mbalimbali havina uhusiano na uwezo wako wa kutumia lugha za kigeni.
Hakuna anayewabeza bali tunawashangaa kwa nini wanaking'ang'ania wakati hawakiwezi
 
Back
Top Bottom