Lowassa: Mkapa alikuza uchumi, JK punguza matumizi

Amezungumzia pia kwamba yapo magazeti yanatumiwa na baadhi ya watu wenye malengo yao kuwazushia wengine
 
Hebu tizameni ITV sasa Lowasa anahojiwa.

Kasema afya yake iko safi kabisa ila watu wanatunga habari, anachoumwa yeye ni jicho.

Pia kaongelea kuhusu kauli ya kutangaza vita, kakana kasema wamamnukuu si sawa.

Sasa anaongelea mgogoro na Malawi kwa ujumla.

sasa akiwa rais ataweza kuisoma miswada?:wacko:
 
Zile pesa alizopata kupitia epa ameshazirudisha? Tunataka azirudishe awe safi tumtayarishe kwa 2015

hapo mtakuwa mnambebesha mzigo usiokuwa wa kwake maana hakuna jambo la richmond alilolifanya ambalo rais alikua halifahamu. :car:
 
Lutulgia ni kitu gani? anataja sana hilo neno.

Huyu hata akipambanishwa na Nzi, mie nachagua Nzi. Awe Rais kwa kuchaguliwa na wengine lakini sio mimi
 
Kuhusu balozi zetu nje ni kwamba kuna tatizo la fedha kwenye balozi zote............kwa mfano mishahara inachelewa kwa miezi sita au mitatu, na wakati mwingine pesa za pango kwa wafanyakazi

Athari zake ni morali ya wafanyakazi inapungua........na kwamba wizara ya mambo ya nje inachelewesha kutoa pesa

Majengo ya ubalozi Marekani na Canada yapo kwenye hali mbaya
 
Tuna viwanja london na waliomba kibali cha wizara ya mambo ya nje wajenge lakini kimya.........na kwamba vibaka wanaishi hapo na kuwatoa inahitaji mahakama kuwaondoa.............."hapa ni kama anasemea uzembe wa wizara ya mabo ya nje'
 
Anasema inahitaji maamuzi kwa kutumia motgage finance ........na kuwa itumike hiyo ili kujenga balozi zetu. Tuunde chombo cha kusimamia hayo majengo
 
Huyu Mtangazaji anakomaa na Ubalozi wakati kuna mambo muhimu ya kumuuliza
 
jamaa kapewa zali na itv na yeye baada ya maadui wake wakubwa kukanyaga sana katika jamvi la itv
 
Hebu tizameni ITV sasa Lowasa anahojiwa.

Kasema afya yake iko safi kabisa ila watu wanatunga habari, anachoumwa yeye ni jicho.

Pia kaongelea kuhusu kauli ya kutangaza vita, kakana kasema wamamnukuu si sawa.

Sasa anaongelea mgogoro na Malawi kwa ujumla.

Kongosho ina maana mzee matatizo ni vision au? Dira muhimu bana.
 
Mbona anaongea kama yeye ni mkuu sana hapa nchini??

Anaongelea nyumba za serikali kwenye balozi mbali mbali.

Huko washngton wanataka USD 1mil ili wakarabati waweze kupangisha.

Wanataka NSSF iwe inakopesha serikali kujenga nyumba nje ya nchi.

Duh!
 
Anamlima Membe kiaina....anasema pamoja na shida ya fedha bado wizara hasikilizi vilio vya watu wetu kwenuye balozi
 
Hili la Maamuzi Lowasa anarudiarudia kwanini asiulizwe nani sasa wa kutoa maamuzi?
 
Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama Mh. Edward Lowassa atazungumzia mgogoro wa Malawi kuhusu ziwa nyasa na pia ugawaji vitalu migodini Katika Kipindi cha SAA 3.00: DAKIKA 45 Kupitia Runinga ya ITV.

Najiuliza maswali alistaili kuongelea haya? Mbona Bungeni huwa mkimya sana? Je Jimbo lake halina matatizo? Ungependa aulizwe maswali gani?

Semuyu kabadilisha location?au amemfuata home?if yes Why?
 
Mbona anaongea kama yeye ni mkuu sana hapa nchini??

Anaongelea nyumba za serikali kwenye balozi mbali mbali.

Huko washngton wanataka USD 1mil ili wakarabati waweze kupangisha.

Wanataka NSSF iwe inakopesha serikali kujenga nyumba nje ya nchi.

Duh!
Ndio anasafisha njia wewe unafikiri Rais JK ameenda kwenye Mgogoro wa Malawi hajaongelea hilo yeye anaongelea ....hapa ndio ujue Tanzania haina mwenyewe kila mtu anaongea yake.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom