Lowassa: Mkapa alikuza uchumi, JK punguza matumizi

Zipuwawa

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
3,051
653
Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama Mh. Edward Lowassa atazungumzia mgogoro wa Malawi kuhusu ziwa nyasa na pia ugawaji vitalu migodini Katika Kipindi cha SAA 3.00: DAKIKA 45 Kupitia Runinga ya ITV.

Najiuliza maswali alistaili kuongelea haya? Mbona Bungeni huwa mkimya sana? Je Jimbo lake halina matatizo? Ungependa aulizwe maswali gani?
21 August 2012 | Gazeti la Mwananchi

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa ameitaka Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kupunguza matumizi na kufanya uamuzi wa kukuza uchumi kama ilivyokuwa wakati wa mtangulizi wake, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.

Lowassa alisema, Mkapa alifanya uamuzi mgumu kiuchumi uliowezesha nchi kupiga hatua zaidi kimaendeleo ikilinganishwa na sasa ambapo taifa limekumbwa na mfumuko mkubwa wa bei.

"Serikali ipunguze matumizi ili kupunguza Inflation (mfumuko wa bei) kwani ni tatizo kubwa," alisema Lowassa katika kipindi cha dakika 45 kilichorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV juzi usiku na kuongeza:

"Rais Mkapa wakati wake alifanya maamuzi mengi ya uchumi, lakini pamoja na wakati wake watu kuuita ukapa, bado alifanya maamuzi mazuri na uchumi ukaenda juu."

Lowassa alimsifu Mkapa akisema, alifanya uamuzi mgumu wenye lengo la kukuza uchumi na kuyasimamia jambo ambalo linapaswa kuwa mfano kwa Serikali zingine.

"Tusikubali hivyo, tufanye maamuzi ya msingi na tuyaeleze hivyo… Rais Mkapa wakati wake alifanya maamuzi ya kiuchumi akayasimamia, sasa tufanye maamuzi ya namna hiyo na kuyasimamia," alisema Lowassa na kuendelea:

"Mfumuko (wa bei) umefikia asilimia 17.9. Imekuwa hivyo kwa muda mrefu. Wakati wa Rais Mkapa ulishuka zaidi."

Alisema Serikali ya Rais Kikwete imefanya mambo makubwa, lakini inatakiwa kubana matumizi ili ukuaji wa uchumi umnufaishe mwananchi wa kawaida.

Lowassa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, alisema ili ukuaji wa uchumi umnufaishe mwananchi wa kawaida, lazima mambo matano yafanyike. Alitaja mambo hayo kuwa ni pamoja na usalama wa chakula, upatikanaji wa mafuta na kilimo cha mashamba makubwa.

"Lakini la muhimu zaidi ni Serikali kupunguza matumizi. Lazima Serikali ipunguze matumizi ili kupunguza ‘inflation' (mfumuko wa bei) lazima kupunguza matumizi, lazima sana," alisisitiza Lowassa.

Kuhusu usalama wa chakula, Lowassa alitaka wakulima waruhusiwe kuuza mazao yao nje ya nchi bila bughudha.

"Kuna maeneo ambayo nadhani hatujayafanyia kazi, moja ni ‘Food Security' (usalama wa chakula). Tuangalie uwezekano wa kuongeza hizo barabara zitumike kuwasaidia wakulima," alisema na kuongeza:

"Kwa mfano wanalima mazao yao Rukwa, tusiwalazimishe kuyauza Arusha kwa sababu gharama za kuyatoa mahindi kutoka Rukwa hadi Arusha ni kubwa mno…Anayetaka kuuza Kenya auze, anayetaka kwenda Burundi ayapeleke. Wakulima wapate nafasi ya kuuza mazao yao kwa uhuru kwa haraka na kwa bei nzuri, hilo ni muhimu sana," alisema Lowassa.

Kuhusu suala la mafuta alisema ,aliishauri Serikali kununua mafuta kwa wingi wakati wa bei ni nzuri.

Aliitaka Serikali kuchukua uamuzi mgumu katika kuimarisha kilimo cha mashamba makubwa na matumizi ya zana za kilimo za kisasa hasa matrekta.

"Trekta ni muhimu sana… Serikali inajitahidi, imeleta matreka mengi ya kutosha… tuongeze mengine, tuondoke kwenye jembe la mkono,..haliwezi kututoa kwenye umaskini,"alisema Lowassa na kuongeza:

"Hata wakati wa Nabii Bwana Yesu, watu walishahama kwenye jembe la mkono… unakumbuka ile habari ya mtu aliyealikwa kwenye sherehe akasema ‘mimi nimenunua jozi ya ngombe nakwenda kulijaribu' walikuwa wameshahama, sisi mpaka leo tuko na jembe la mkono, haiwezekani."

Kauli hiyo ya Lowassa imekuja wakati kukiwa na malalamiko kutoka kwa wananchi na wadau wa siasa kuitaka Serikali ipunguze matumizi hasa katika ununuzi wa magari ya kifahari na safari za ndani na nje za viongozi wa Serikali
 
Leo tarehe 20/08/2012 saa 3.00 Usiku Edward Lowassa atakuwa ndani ya dakika 45 za ITV. Je kuna jipya? Natarajia atajibu hoja za JK kwamba wanaozungumzia vita kati ya Malawi na Tanzania ni wapinzani.

Source: Radio One
 
Bora LOWASA AONGELEE HILI, maana naona mkuu kashindwa kazi kaogopa!!!!! Lowassa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama...ongea bwana hao Malawi wasitutanie. Siwa letu afu wanatuchezea kisa....nanukuu 'udhaifu wa rais wetu'
 
Nikisikia lowasa tu huwa natapika na kuharisha. Samahani sn wana jf kwa hili.
 
hivi hiki kipindi kinakuwaga live au kinakua kimesherodiwa.!
 
Nikisikia lowasa tu huwa natapika na kuharisha. Samahani sn wana jf kwa hili.

Unaomba samahani kwa jambo lipi au kwa kuharisha na kutapika!? Kama inawezekana kapime maana hizo ni dalili nzuri sana za kale kananii.
 
Zile pesa alizopata kupitia epa ameshazirudisha? Tunataka azirudishe awe safi tumtayarishe kwa 2015
 
Nasubiri kumuona,, akiongea pumba nampotezea naendelea kujiangalizia man untd live van prsie
 
Spidi ya Lowasa kwa siku za karibuni imekuwa kubwa sana kutaka kuwaaminisha waTZ anastahili kuiongoza Tanzania kuanzia 2015 hadi 2025. Anajidai kuibua kero za waTZ lakini namwona amebaki peke yake ktk hizi kampeni kama nyati aliyejeruhiwa anavyojitenga na kundi na kuishi peke yake porini huku akivizia adui ammalize.
 
Back
Top Bottom