Lowassa/Mbowe watunishiana misuli

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,283
3,274
"Chama kinapita kwenye process nyingi, kwanza unaanza na siasa za uwanaharakati na CHADEMA tulisha graduate kwenye hili sasa hatuhitaji siasa za maandamano tena",Hii ni kauli alioitoa Lowassa alipokua akizungumza na vijana wa CHADEMA.

Watanzania wanajua na dunia inajua kwamba ulisikika uvumi kila kona ya nchi kwamba ukiachilia mbali sababu zilizotolewa na chama juu ya kile kilichoitwa ukiukwaji wa katiba ambao mwisho wa siku ulipelekea ZZK na kina Kitila kung'atuka CHADEMA pia kulizungumzwa habari ya mwenyekiti kua alfa na omega kwenye chama na sasa zipo ishara ya siku moja Lowassa yakamkuta.

Leo tunaona chama kimeyatupilia mbali mawazo ya Lowassa yakuachana na siasa za maandamano badala yake CHADEMA wamekuja na operation UKUTA kinyume kabisa na mawazo ya Lowassa.

Hapa lipo swali la msingi lakujiuliza je ushauri wa Lowassa umeonekana hauna maana? Na kama umepuuzwa pia lipo swali la msingi lakujiuliza ni kipi kimejificha nyuma ya pazia hata mh Lowassa akaanza kupuuzwa mapema?

Kama hiki kilichotokea hakikutokea kwa bahati mbaya basi tunaendelea kuwasisitiza CHADEMA wakae na LWS wamshauri asiwe anakurupuka kutoa matamko ambayo mwisho wa siku yanaleta ukinzani.

Tujikumbushe haya:

"Wanaofikiri mimi nitaondoka CCM wataondoka wao mimi siondoki CCM".Baada ya muda,"CCM sio baba yangu wala mama yangu".Hii ni ishara yakukurupuka kwenye kutoa matamko.
 
Siasa za uanaharakati na kudai democrasia na kupinga udicteta uchwara ni vitu viwili tofaut
Uanaharakati sio kuandamana bali ni kupinga maovu katika nchi
Ukweli haukuwahi kukubali kupindishwa
 
Nakuhakikishia
Hizo porojo za hawa watu hazifiki mbali

Eti UKUTA !!!

Hehehe kweli ukisha kosa
huishi kutapatapa.

Lakini sio mbaya maana kula,kukojoa
Wanapata kutoka kwenye siasa,
Sio Mbaya kujihami,

Shida ni kwa hawa Vibendera
Wasio taka kupima nakutumia vichwa vyao
 
Chadema wanatakiwa kubadilika ili kwenda na hali ya siasa ya wakati huu na hasa kasi ya serikali ya Magufuli, kinyume na hapo 2020 hali itakuwa ngumu hawataamini. Tayari walisha jitabiria mwaka jana kuwa wangeshindwa kuing'oa CCM basi tena, hawakuing'oa na sasa wanakuja na mikakati ya kitoto ambayo hata mtoto mdogo anaelewa itashindwa asubuhi tu.
 
Chadema wanatakiwa kubadilika ili kwenda na hali ya siasa ya wakati huu na hasa kasi ya serikali ya Magufuli, kinyume na hapo 2020 hali itakuwa ngumu hawataamini. Tayari walisha jitabiria mwaka jana kuwa wangeshindwa kuing'oa CCM basi tena, hawakuing'oa na sasa wanakuja na mikakati ya kitoto ambayo hata mtoto mdogo anaelewa itashindwa asubuhi tu.

we siunaipenda C C M ushauri wako uhifadhi CDM HAWAHITAJI USHAURI WAKO ahsante
 
Wakati Lowassa akitangaza CHADEMA kugraduate kuachana na harakati,kamati kuu imetangaza operesheni UKUTA.
Ni mbinu gani ya kigraduesheni operesheni hii itaendeshwa bila kugusa harakati?
 
Back
Top Bottom