Lowassa matatani zaidi

I found this massage very funny

Naye Lowassa akawaambia mawaziri wengine"
KESHENI mkiomba kwani hamjui siku wala saa atakayokuja Dr
Mwakyembe.Nami naenda mtaani kuwaandalia kijiwe ili
nitakapokuwa nanyi muwepo.Nanyi muonapo tume zaundwa
basi mtambue muda wa mavuno ya MAFISADI umekaribia". Kisha akakwea tena Ikulu kuomba Rais asimfilisi. Lakini RICHMOND akatokea na jeshi la Mwakyembe na kusema " Nitakayembusu huyo ndie....!".Mara Chenge akatoa Upanga alani na kumkata mfuasi wa Mwakyembe(Anna Kilango) sikio .Lowassa akamwambia Chenge "rudisha upanga wako alani,Kikombe nilichotupiwa na Kikwete Sina budi Kukinywa"


Moja kati wa mayahudi wale aitwaye Selelii hakuamini kama Lowasa Kajiuzuru,akatwaa mkuki akamchoma ubavuni na tazama...Ikatoka gas ya songosongo na nati ya mitambo ya umeme...Siku ya tatu wakaenda pale ofisini kwake..Lakini wakakuta wingu la Mvi limetanda na Suti ya mistarimistari pale kitini walipomweka..yule morani waliyemkuta getini akawaambia mnayemtafuta hayupo.....Ameshapaa kwenda Monduli na yupo kuume kwa Laiboni..Wakasema..."Hakika huyu alikuwa Fisadi.
Hehehe
 
1. Kama hujawahi kuunga mkono ujio wa Lowasa CHADEMA, sasa hebu tuoneshe ushahidi wowote wa wewe kupinga ujio wake Chadema.

2. Kama hujawahi kuunga mkono ujio wa Lowasa CHADEMA, ni kwanini sasa unashindwa kutetea/kushikilia msimamo wako kama mwanaume kwamba ''Lowasa ni tumaini la mafisadi, wezi, wahuni, majangili, magaidi, na wauza unga''?

View attachment 374460
Mmemnasa huyu kidampa aisee
 
Weka ushahidi wa mimi kubadili kile nilichoandika huko nyuma. Tatizo la kuonyesha kile nilichoandika miaka ya nyuma na sasa ni lipi!? Nashindwa kukuelewa wewe kuendelea kung'ang'ania kitu ambacho hakipo na wala hakitakuwepo. Narudia tena si kila aliyepinga ujio wa Lowassa CHADEMA aliamua kujiondoa CHADEMA. Ujio wa Trump GOP wengi ndani ya GOP hawakujiondoa pia pamoja na kuwa wanampinga Trump.

Kama kutukanwa mimi pia natukanwa sana humu hadharani na kwenye PM
Mbona ulimpigia kampein
 
Hahahahaha lol! Na wewe kuendelea kuunga mkono wahuni, mafisadi, wezi, dikteta uchwara, hutii kinyaa!? hata muasisi wa CCM alitamka hadharani kwamba CCM si mama yake kwa sababu alisikika kinyaa!? Wewe lini utaanza kusikia kinyaa na kuacha kuwaunga mkono wanaoiangamiza nchi yetu miaka nenda miaka rudi!?

Hebu niambie tofauti ya Mmarekani ambaye siku zote alikuwa akidai yeye ni Democrat kisha akageuka na kuingia Republican, na Mtanzania ambaye miaka yote alikuwa CCM agauka na kuingia CHADEMA!? Hakuna popote pale ambapo nimejiaibisha labda kwa mtu mwenye ufinyu wa akili kama wewe.

Acha upumbavu wewe! Unanitaka nilog out wewe ukiwa kama nani humu!? Acha kujibaraguza wewe.
Ccm itabaki tu madarakan cha muhim tunawaombeeni uzima ninyi kina BAK
 
Back
Top Bottom