Lowassa kutumia sh bilioni 70 kujenga gorofa 25 Dar City Centre!

Kwa mujibu wa gazeti la DIRA la leo toleo la Novemba 29 - Desemba 5, 2010, waziri mkuu wa zamani aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi ya Richmond, Edward Lowassa, amebomoa jengo la kihistoria la Nyumba ya Sanaa pale karibu na Movenpik Hotel Dar city centre na sasa atajenga gorofa 25 kwenye eneo hilo.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, mradi huo utagharimu dola za kimarekani $45.5 million, sawa na takriban shilingi bilioni 70!.

Mradi huo wa jengo unajengwa kupitia kampuni ya Lowassa inayoitwa Integrated Property Investment (Tanzania) Limited.

Kuna tuhuma kuwa huu ni mradi wa kifisadi. Wasanii walilalamika mpaka Ikulu kwa Kikwete kujaribu kuzuia Nyumba ya Sanaa isivunjwe na kampuni ya Lowassa wakashindwa.

Kampuni hiyo ya Lowassa ndiyo iliyohusika na kashfa ya kununua nyumba huko London kwa karibu shilingi bilioni 1. Kwa mujibu wa gazeti la RAIA MWEMA la wiki iliyopita, mtoto wa Lowassa, Frederick, anachunguzwa na polisi wa Uingereza kutokana na kashfa hiyo.

* Je, Lowassa ambaye maisha yake yote amekuwa civil servant ametoa wapi 70bn/- kujenga gorofa hilo?

* TAKUKURU inasemaje kuhusu utajiri wa kutisha wa PM huyu wa zamani haswa baada ya yeye kuhusishwa na ufisadi wa Richmond na baadae TAKUKURU kumkosha?

* Huyu ndiye mtu anayetaka kuwa Rais baada ya Kikwete 2015 "by any means necessary" kwa kushirikiana na Rostam Aziz, Andrew Chenge, Nazir Karamagi, Yusuf Manji, Yusuf Makamba, Kingunge Ngombale Mwiru, etc. Nchi hii ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itapona kweli?

Anayetoa taarifa dira Isije ikawa alipataka halafu kazidiwa...Ningewaelewa Dira kama wangetuambia na mchakato mzima wakupatikana hilo eneo..inawezekana kapata katika njia halali kabisa...na kuhusu suala katoa wapi Bil 70/= nadhani suala la financing kwenye mabenki au joint venture ni very possible..lets not discuss something on the face lete kitu detailed ili tu analyze sio cut and paste with your biased comments
 
Mkuu,

Nakubaliana na wewe kabisa hapo juu. Inaelekea watanzania tumeanza kuzidiwa na majungu vichwani mwetu na kuwa na wivu wa ajabu. Kila Mtanzania anayefanya jambo tunamwona ni mwizi wakati wageni wanakuja hapo hawana hata senti tano na baadaye wanakuwa mamilionea.

Watanzania tunamalizana wenyewe tunawaachia wageni wantamba kwenye uchumi...........that is being hypocrtic at the highest level.....chukulia mfano Pale kuna Invester anajenga uhuru peak ...ghorofa 30...wale jamaa walikuja hapa wakaaza kununua pamba ....kwa kukopeshwa na benki ...wakajenga maviwanda ..sasa wamepata mkopo nje na ndani na pesa zao wanajenga lile ghrofa refu kuliko yote tz.......so kwa kuwa ni wahindi ...no body cares....
wengine wamekuja wakimbizi toka somalia ...tumewapa mitaji haapa hapa ...wameinuka..,tatizo pesa akiishika mbantu ..kila mtu ana haha....tuacheni utumwa wa fikra!!!!.......naamini kabisa kwa mradi wa size ya nyumba ya sanaa na kwa dunia ya leo ..yenye intergrated actions against ufisadi lazima ni mkopo...tu!!!...na kama ni mkopo sioni ajabu!!!!

kwenye nchi za wenzetu you can own any asset you want kupitia mkopo ..ili mradi uwe na defined repayment strategies and plans!!
 
Nyie mliotumwa na membe acheni hizo.......unaweza kukopa agaist the project....nenda kwa banker wako akuambie....,kinachotakiwa tu uwe na biashara na uwe mtu unayeaminika .,,biashara yako iwe na uongozi imara....mahali unapojenga pawe na title etc......chukulia mfano uwe na site pale posta ..na uwe na business plan inayoeleweka unapata pesa ...msipotoshe watu!!!....that CBD is very lucrative site...na mikopo kama hiyo unaweza kukopa mabenki makubwa makubwa[merchant banks]...sio hizi baadhi ya benki zetu ila ni benki kubwa [investment banks]
....those are called syndicate loans ....kiasi kama $45 million unaweza kuchukua...benki kama tatu zikaungana kukukopesha..ie crdb,stanbic,stanchart,rasilimali,nmb etc......maana kwa level ya tanzania benki zetu kubwa ndio hizo na hata hizo kiasi cha $45 m ni kikubwa......au unaweza kukopa kupitia kwa benki za kimataifa zilizoko nchini kupitia kwa holding banks zao[ie Barclays banks plc etc...]...pia world banks na commonwealth finance[IFC] wana kiteNGo cha mikopo mkikubwa aina hii.....


SHARTI LAO KUU NI KUWA WAO NDIO WATAKUWA WANASIMAMIA MASUALA YA FEDHA HADI MRADI UISHE.....IKIWEMO KUFANYA VALUE FOR MONEY AUDIT MARA KWA MARA....NA JENGO LIKIISHA WANEWEZA KUWEKA PROPERTY MANAGER akakusanya ushuru kutokana na makubaliano ya makato na kiasi kingine unabaki nacho...hadi mkopo uishe ....au kama una uwezo wa kulipa kupitia biashara zako nyingine thats another point....

So naombeni ondokaneni na mawazo ya kuwaogopa watu wanaofanya miradi mikubwa ...mkadhani na nyie hamuiwezi.....na kubaki kulalama.......hakuna mfanyabiashara mwenye uwezo wa kujenga jengo la bilioni 70 kwa kuchukua pesa uvunguni mwa kitanda kama ambavyo tunajenga vibanda vyetu vya room 3 ,bila financing!!....ikitoke hivyo lazima hata INTERPOL na watu wa CIA / FBI anti money laundering watashtuka tu....

Nashukuru kwa elimu nzuri uliyotoa!vipi pale kwako kuna mikopo mikubwa kama hii?Nakuaminia mzee wa BAF!!!
 
Mkuu kama ni uzushi na uwe uzushi tu. Hapa Tanzania tuna sheria na taratibu za kuyashitaki magazeti zushi, kwa kuwa unasema huu ni uzushi itakuwa poa sana kama hao jamaa wazushi wakichukuliwa hatua. Lakini kama si kweli kuwa ni wazushi, yaani kama kweli Lowassa anataka kujenga nyumba yenye thamani ya Shilingi bilioni 70 hakuna ubaya kuuliza kwa kuwa yeye alikuw amtumishi wa umma mashara wae wote na marupurupu yake halali haayawezi kufika shilingi bilioni 1, sasa anataka kujengta nyumba ya shilingi bilioni 70, kama kweli kuna haja ya kuuliza kama alituibia hela, au alipew zawadi hizo hela. So simple.

Kuna watu walianza kusema Dr Slaa ni muongo, hakuna EPA, kuna mwingine alisema Richmind ni uongo, yalianzia huko huko kwenye vitabloid, lakini yote yakawa kweli.

Bongolander,

Ni sawa kuna sheria lakini sio rahisi kuwashitaki hao wakubwa wanaomiliki magazeti yanayoongoza kwa kuchafua watu. Labda kama unaongelea watu kama Lowassa tu. Lakini pia na yeye ni mwanasiasa na kwa wanasiasa hakuna kosa kubwa kama kwenda mahakamani hata kama haki iko kwako.

Imagine ni wewe umechafuliwa, ukiamua kulipeleka gazeti la Mengi mahakamani, jiandae kupoteza muda wako, pesa zako na mwishoni si ajabu kushindwa case on technicalities. Ndio maana watu wengi wanaamua kuachana na hayo magazeti na kuendelea na maisha yao.

Leo tunaweza kushangilia kwasababu yanamhusu mtu mwingine, lakini wakati wote ni bora kununua insurance wakati huihitaji. Haya magazeti hayana maadili kabisa. Mhariri anatumwa na wenye pesa kwenda kuchafua wengine na anafanya hivyo bila hata aibu. Hiyo fani imevamiwa na watu wa ajabu kweli kweli.
 
Waungwana, mbona tunapotosha mada? Hapa suala si kukopa benki, nenda wewe kajaribu kukopa kama utapewa hizo $45.5m. Lazima na wewe uwe na mabilioni benki ndiyo waweze kukukopesha. Suala la msingi ni kuwa kiongozi wa umma huyu Lowassa anatoa wapi pesa kuendeleza mradi wa shilingi bilioni 70 na kununua nyumba London kwa cash shilingi bilioni 1?

Hapa inabidi tuhoji huu utajiri kaupata wapi huyu kiongozi wa umma? Ni kukosa busara eti kumpongeza kwa kuwekeza Tanzania. Kwani Lowassa ni mwekezaji au kiongozi wa umma?

Akiwa kama kiongozi wa umma, serikali ina wajibu wa kuchunguza huu utajiri mkubwa kaupata wapi?

Tusitafute majibu ya haraka ya kusema kakopa benki na kumsifu kuwekeza Tanzania. Let's look at the bigger picture, hii "unexplained wealth" ya huyu Lowassa imetoka wapi?

Please kama kitu hujui kaa kimya..umengangania suala la kukopa nani kakuambia kakopa????? inawezekana thamani ya eneo ndio shares zake...please uliza kabla hujaandika upupu humu..mnachosha na umbea
 
Nyie mliotumwa na membe acheni hizo.......unaweza kukopa agaist the project....nenda kwa banker wako akuambie....,kinachotakiwa tu uwe na biashara na uwe mtu unayeaminika .,,biashara yako iwe na uongozi imara....mahali unapojenga pawe na title etc......chukulia mfano uwe na site pale posta ..na uwe na business plan inayoeleweka unapata pesa ...msipotoshe watu!!!....that CBD is very lucrative site...na mikopo kama hiyo unaweza kukopa mabenki makubwa makubwa[merchant banks]...sio hizi baadhi ya benki zetu ila ni benki kubwa [investment banks]
....those are called syndicate loans ....kiasi kama $45 million unaweza kuchukua...benki kama tatu zikaungana kukukopesha..ie crdb,stanbic,stanchart,rasilimali,nmb etc......maana kwa level ya tanzania benki zetu kubwa ndio hizo na hata hizo kiasi cha $45 m ni kikubwa......au unaweza kukopa kupitia kwa benki za kimataifa zilizoko nchini kupitia kwa holding banks zao[ie Barclays banks plc etc...]...pia world banks na commonwealth finance[IFC] wana kiteNGo cha mikopo mkikubwa aina hii.....


SHARTI LAO KUU NI KUWA WAO NDIO WATAKUWA WANASIMAMIA MASUALA YA FEDHA HADI MRADI UISHE.....IKIWEMO KUFANYA VALUE FOR MONEY AUDIT MARA KWA MARA....NA JENGO LIKIISHA WANEWEZA KUWEKA PROPERTY MANAGER akakusanya ushuru kutokana na makubaliano ya makato na kiasi kingine unabaki nacho...hadi mkopo uishe ....au kama una uwezo wa kulipa kupitia biashara zako nyingine thats another point....

So naombeni ondokaneni na mawazo ya kuwaogopa watu wanaofanya miradi mikubwa ...mkadhani na nyie hamuiwezi.....na kubaki kulalama.......hakuna mfanyabiashara mwenye uwezo wa kujenga jengo la bilioni 70 kwa kuchukua pesa uvunguni mwa kitanda kama ambavyo tunajenga vibanda vyetu vya room 3 ,bila financing!!....ikitoke hivyo lazima hata INTERPOL na watu wa CIA / FBI anti money laundering watashtuka tu....

Tatizo la "great thinkers" wengine humu ndani ni mafundi sana wa kujaribu kupotosha hoja za msingi. Sote tunajua Membe na Lowassa zamani walikuwa ni maswahiba wakubwa baadae wakakosana. Wenyewe wanajua sababu za kukosana kwao, ila zinapoibuka tuhuma zozote zile kuhusu Lowassa na kusema eti zimeanzishwa na Membe ni jambo la kitoto hilo. Tupime kila hoja/tuhuma kwa uzito wake.

Ni dhahiri kuwa ni kweli huenda Lowassa amekopa hizo shilingi bilioni 70 kujenga hilo gorofa ila ukweli unabaki palepale, benki hawawezi kukukopesha kwa kuangalia makaratasi tu. Lazima wacheki cash flow yako, bank statement na track record yako kuhakikisha kuwa wewe mwenyewe una mabilioni benki ndiyo wakupe hizo $45.5 million.

Swali la msingi liko palepale, Lowassa ambaye maisha yake yote amekuwa ni kiongozi wa umma, ametoa wapi utajiri wake huu wa kutisha? Je, yeye ni mwekezaji au ni kiongozi wa umma? Kwa nini serikali haichunguzi chanzo cha utajri wake ambao hata Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuuhoji?
 
Hili jukwaa mnalifanya kuwa la Majungu sasa! Utawezaje kunukuuu vijarida vya mtaani na kuvileta hapa!?

IPI ni kampuni kubwa ya Uingereza na wanawekeza pale Bahari Beach, waliingia mkataba na Nyumba ya Sanaa kupaendeleza pale. Unaweza kupata habari zaidi www.ipiltd.com , kwamba Lowasa ana share kwa IPI Ltd(Tz) kwangu naona ni fahari, tena kama wanawekeza hapa home ni fahari kubwa zaidi. Natofautiana na mwanaJF aliyemtaja Manji kwamba anawekeza nje ya nchi. Huyu ni tofauti kabisa na wengine wengi wanasiasa tunaowafahamu. Huyu ni crazy katika real estate investment, ukiacha yale magodown ya Ubungo, nenda Pugu/Nyerere Road, utaona utitiri wa majengo yake makubwa yenye nembo ya Quality Group. Ni Rostam huoni chochote cha maana licha ya utajiri wa kutukuka.

Tusimwandame Lowasa kwa hata yale mazuri anayotendea taifa
Njilembera, we have a problem somewhere, kuna watu wangependa kuwaona viongozi wastaafu wa seriakuli wakifuga ngombe wawili au watatu wa maziwa.

Amini usiamini, kama huyo developer angekuwa Patel, wala usinge sikia kelele yoyote, lakini kwa vile ni jina la kibantu tena alikuwa PM wetu, basi imekuwa issue kubwa!.

Watu wanapiga kelele sana, huku hakuna anayejua financier ni nani, developer kazi yake kudevelop, pesa amekopa benki kwa makubaliano maalum, hivyo sioni tatizo liko wapi.

Kauli yangu ni ile ile siku zote, mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!.
 
Kwa hiyo fisadi akiiba pesa za umma akaziwekeza Tanzania basi huyo ni mtu safi hajafanya kosa kwani anaendeleza nchi yake?! Hivyo hivyo kwa kiongozi wa umma kama Lowassa kuwa na utajiri mkubwa usioweza kuelezeka ni sawa tu kwa vile anawekeza pesa zake Tanzania? Na hiyo nyumba aliyonunua kwa cash London kwa 1 billion/- kawekeza Tanzania?

Wallahi, Baba wa Taifa angekuwa hai na kusikia Watanzania wanazungumza maneno haya ingemuuma sana.

Wapi maadili ya uongozi wa umma? Wapi maadili kwenye sisi wananchi kwenye jamii ambao baadhi yetu tunahusudu mafisadi na viongozi wa umma wasio waadilifu na wenye utajiri wa mashaka kama Lowassa eti kwa vile wamewekeza Tanzania?

Suala la msingi la kujiuliza na ambalo halikwepeki ni kuwa kiongozi wa umma kama Lowassa anatoa wapi utajiri kama huu? Sheria inataka vyombo vya dola kuwachunguza viongozi wa umma wenye "unexplained wealth." Je, kwa nini Lowassa hachunguzwi?
sa sijui ndo mjue JF imeingiliwa.
 
Tatizo la "great thinkers" wengine humu ndani ni mafundi sana wa kujaribu kupotosha hoja za msingi. Sote tunajua Membe na Lowassa zamani walikuwa ni maswahiba wakubwa baadae wakakosana. Wenyewe wanajua sababu za kukosana kwao, ila zinapoibuka tuhuma zozote zile kuhusu Lowassa na kusema eti zimeanzishwa na Membe ni jambo la kitoto hilo. Tupime kila hoja/tuhuma kwa uzito wake.

Ni dhahiri kuwa ni kweli huenda Lowassa amekopa hizo shilingi bilioni 70 kujenga hilo gorofa?

Nimekugusa eh?

.....miradi kama ile benki wanabaki na ownership hadi mkopo uishe na ni lazima uwe na insurance...ya ku cover hili jengo.....
wanatoa pesa ,wanazidhibiti ...jengo likiwa tayari wanafuata business plan yako....wanaweka property manager ...kila senti inapitia kwa wanalamba percent yao ...unapewa yako kulingana na mkataba.....mkopo ukiisha unarushiwa hati...[ownership]....

Mimi binafsi ninayo project kama hiyo ya milion..1$......na hutaamini zaidi ya kuwa na prime plot sina pesa ...na ndio condition niliyopewa ...nikope against mali...na karibu nitapata..ila as i said ma contractor wote wanalipwa na benki..hawakupi pesa ...wanaogopa uta divert project.
 
Lowassaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaanafurahisha sana huyu fisadi.
 
achaneni na lowassa do your shits....mimi mwenyewe simfagilii lakini naunga mkono wazo la kuwekeza alichonacho nyumbani....miaka ya nyerere tumepotreza mamilioni kupitia kwa watu kama cleopa msuya,etc ambao walijifanya wajamaa kumbe wana magorofa japan.....wengine wamedhulumiwa na wazungu na wahindi...sasa bora lipi kama mtu ana access ya kupata mkopo mkubwa au ana pesa si mwacheni ajenge!!!

mnajuwa tofauti ya ufisadi wa kenya na tanzania miaka ya mwanzo .....ni kuwa hakuna kiongozi wa kenya aliyepeleka pesa zake nje...wote wamewekeza kwenye mashamba ya chai ,kahawa na ufugaji....wakati watanzania wote walikuwa wakikimbiza pesa nje........kwa unafiki wetu!!
wakati moi anatoa hotuba ya kuaga pale bungeni mwaka 2002....alisema ..""..nastaafu na nitabaki kukaa kenya na mara nyingine nitatembea ndani ya afrika mashariki kama arusha au dar au kampala......chochote nilichokipata nikiwa madarakani nimewekeza kwenye nchi yangu..au ndani ya afrika mashariki...sina sababu ya kwenda ughaibuni kama wengine..."
ujamaa wetu tuliojitahidi kujenga tukashindwa umetujengea unafiki na wivu......tupambane na ufisadi...lakini vile vile tukatae pesa za kodi yetu kuwekezwa nje ya tanzania....na ni kazi ya takukuru vile vile kuangalia viongozi wanaoweka pesa nje...napendekeza hao wapewe adhabu kubwa zaidi..
mkuu unaloongea ni kweli nakuunga mkono ni bora fisadi anaye wekeza nchini kuliko anayewekeza kwenye visiwa na kuendeleza nchi zingine! Lowasa we tumia pesa zako za wizi hapahapa nchini!
 
Nashukuru kwa elimu nzuri uliyotoa!vipi pale kwako kuna mikopo mikubwa kama hii?Nakuaminia mzee wa BAF!!!

Excuse me ..what is BAF??

Mimi sitoi mikopo...ila nakopa..mzee...naishi kwa kukopa na kulipa,.....ila kwa kukusaidia ni vigumu kupata a single bank tanzania wakakupa..ndioo maana nikaongelea kuwa kwa mkopo mkubwa wa hivi kwa huzi local bank ..una discuss na bank kama tatu hivi wanakupa kitu kinaitwa syndicate loan...wenyewe wanakubaliana..ILA pia nimekueleza kuwa mikopo ya size hii hutolewa kirahisi na kwa terms nzuri na oversea investments banks....or finace institutions....kwani intrest rate ya local banks ni kubwa mno kuweza kumpa faida mwekezaji wa jengo la $45........
 
Wanaomtetea Lowasa ni walewale wasioionea huruma jamii ya kitanzania inayoteseka kutokana na maamuzi mabovu ya watedaji wa serikali.

Tukubali kwamba KIKWETE anahusika ktk hili ndo maana pamoja na taarifa alizofikishiwa na wasanii ameamua kuwapuuza.

Hivi huyu Lowasa analindwa na nani???
 
Yero subai jenga utupe ajira maana huku mtaani hapafai. Wajinga ndo waliwao
 
The fact that has decided to invest in Tanzania, I think he should be credited for that. There are many Tanzanians who are going to be employed up there. If there is a contract between Nyumba ya Sanaa and his company, what is the problem? After all, he has not changed the use of the area only improved!

Hey, Tanzanians, let us encourage our own people to invest in Tanzania. It is for the benefit of all Tanzanians.

Do you want him to invest elsewhere?

Jamani hata kama anajenga msikiti ama kanisa, suala hapa je, ni halali, maana viongozi wetu hawana huo utajiri halali wa kuwekeza, Mkapa alifanya jambo jema kununua Kiwira lakini mazingira yalikua na kila aina ya utata. Tusiwe vipofu na kuwa kama watoto wa kijiweni mtu akiuza madawa ya kulevya anasifiwa kuw ani mjanja na amefanya vyema, jambazi akiiba na kuwa tajiri anaitwa 'mjanja' na mfano wa kuigwa hali kadhalika fisadi. Jamani tufumbue macho. Hata huyo Manji ana vitega uchumi kibao nchini pamoja na kupeleka nje, Rostam naye ana vitega uchumi kibao nchini, tusiwasema sababu ni weupe na kumtetea Lowassa sababu ni mweusi. Wizi hauna rangi, dini wala kabila jamani.
 
Wanaomtetea Lowasa ni walewale wasioionea huruma jamii ya kitanzania inayoteseka kutokana na maamuzi mabovu ya watedaji wa serikali.

Tukubali kwamba KIKWETE anahusika ktk hili ndo maana pamoja na taarifa alizofikishiwa na wasanii ameamua kuwapuuza.

Hivi huyu Lowasa analindwa na nani???

Wasanii anao wajua yeye ni wale waliompigia kampeni sio hawa wa SINDIMBA
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom