Lowassa kutumia sh bilioni 70 kujenga gorofa 25 Dar City Centre!

Wagonjwa wa PHOBIA utawajua tu. Wao kila kitu wanaogopa. Hata akijenga ghorofa 70 kwa 800Bl, wewe yanakuhusu nini? After all magazeti yaTanzania ni uzushi mtupu. Nakumbuka gazeti moja liliwahi kuandika kuwa Sumaye anamiliki utajiri wa kutisha kwa njia ya rushwa. Baada ya kufikishwa MCT na mahakamani ili wa-prove walishindwa na ikaamuliwa wamlipe Sumaye mabilion ya fedha ingawa nao walishindwa. Kwa hekima mzee Sumaye aliwasamehe. MAGAZETI YETU NI WAZUSHI, MTU AKIJUA KUANDIKA BARUA YA MAPENZI ANAJIITA MUANDISHI WA HABARI. Hata mzee mwinyi wakati akiwa Rais, tulielezwa kuwa ana mpango wa kuishi uarabuni pindi atakapostaafu, yapo wapi leo? SHAME ON YOU WITH YOUR TABLOIDS
 
Mi sioni tatizo kama ana Invest,hivi hiyo milafi yooote ya CCM toka uhuru mbona hakuna hata mmoja aliyewahi kujenga hata Shule ya chekechea?
Pesa zote wanakimbiza kwenye mabenk nje wanamnufaisha nani sasa........hivi kama wangekuwa wanatuibia halafu wanazitumia humu humu si tungekuwa mbali sana....
 
Gazeti la DIRA silielewi vizuri lakini lime quote mkataba kati ya Nyumba ya Sanaa na Integrated Property Investment (Tanzania) Limited. Pia nyaraka za BRELA zinaonesha kuwa Lowassa ndiyo mmiliki wa Integrated Property Investment (Tanzania) Ltd. Tujifunze kuwa open-minded na si kutetea watu tu. Tunapaswa kufuatilia jambo hili. Pia si jambo la siri kuwa Lowassa ana utajiri mkubwa sana wa mashaka kupitia kampuni yake ya Alphatel na nyinginezo

Umenena, kaka ila HAMNA KIJIFUNGU CHOCHOTE CHA KATIBA tunachoweza kukifanyie AMMENDMENT alafu tukamuweka huyu jamaa ndani?? au mpaka tubadilishe utawala?? napo inachukuwa muda mrefu??
Inauma saaanaaaaaaa
Ila hamna hata kajipengele kengine ka KUTAIFISHA??
Yaani huyu jamaa ..... mi hapa nimetumia elfu 13 kwa ajili ya familia yangu chakula leo, bado naona kama natetereka.
poa tu ipo siku?
 
definatelly kwa mradi mkubwa kama huo ni benki.........

sasa jamani whats a big deal.....kama mkataba unaonesha perfoming theatres zitakuwa restored tena kubwa .....na wasanii wakaweza kuwa na stalls za kuonesha vitu vyao....tuacheni mawazo mgando!!!....nadhani pia board of trustee wa nyuma ya sanaa wamemshirikisha yule mama wa ki nordic aliyejenga lile jengo na kumkabidhi mwalimu...

tuacheni kuwabana watu wanapoamua kuwekeza pesa zao......nyie ndio mnafanya watu wanaenda kuwekeza ulaya......au south afrika.....waacheni wawekeze hapa..ili turudishe pesa yetu kwenye kodi na ajira...
 
mwacheni bana..Kila siku maneno tu ,umaskini kitu kibaya sana..Yaani badala ya kuwaza utapataje hela we unakazi ya kujadili Lowassa kafany anini..binafsi simpendi Lowassa ila sasa mmezidi kumsema bana

We hamna kitu kabisa, HAPA HAJADILIWI LOWASA, inajadiliwa MALI ALIYONAYO LOWASA KAIPATAJE WAKATI AMEKUWA MTUMISHI WA SERIKALI MIAKA YOOOOOOTE HIYO?
Mjadala huu wa leo NDIYO HUKUMU YAKE YA KESHO!!!
Tafakari, hapa hachukiwi mtu ila JIULIZE WAPO WATU WATANZAIA WANGAPI WALIOFANYA KAZI SERIKALINI KABLA na BAADA YA LOWASA (namaanisha watu waliokaa vitengo vizuri zaidi yake lakini walikuwa waadilifu) ambao wanayo hela ya kula tu??/
 
Membe ni bora akatumia muda wake kufanya kazi ,kumchafua lowassa haitasaidia ...kwani hata yeye membe[joka la mdimu] hatakuwa rais wa tanzania.....labda kama ccm wanataka kuipa urais CHADEMA ....membe ni mnafiki mkubwa ambaye yeye na lowassa walikuwa wakimchafua yeyote ambaye alionekana tishio kwa kikwete ..kuanzia kitine,idd simba,salim,malecela etc...

SASA WAMEKOSANA NA LOWASSA KWA AJILI YA URAIS .....ANAMCHIMBA....KWELI NDOA YA WANGA HAIDUMU!!!

MEMBE ANATAKIWA AJUWE KUWA RAIS WA NCHI ANATAKIWA AWE MTU KAMA...DR MAGUFULI...NA waziri mkuu aina ya mwakyembe ..what a dream team!!!
 
Hili jukwaa mnalifanya kuwa la Majungu sasa! Utawezaje kunukuuu vijarida vya mtaani na kuvileta hapa!?

IPI ni kampuni kubwa ya Uingereza na wanawekeza pale Bahari Beach, waliingia mkataba na Nyumba ya Sanaa kupaendeleza pale. Unaweza kupata habari zaidi www.ipiltd.com , kwamba Lowasa ana share kwa IPI Ltd(Tz) kwangu naona ni fahari, tena kama wanawekeza hapa home ni fahari kubwa zaidi. Natofautiana na mwanaJF aliyemtaja Manji kwamba anawekeza nje ya nchi. Huyu ni tofauti kabisa na wengine wengi wanasiasa tunaowafahamu. Huyu ni crazy katika real estate investment, ukiacha yale magodown ya Ubungo, nenda Pugu/Nyerere Road, utaona utitiri wa majengo yake makubwa yenye nembo ya Quality Group. Ni Rostam huoni chochote cha maana licha ya utajiri wa kutukuka.

Tusimwandame Lowasa kwa hata yale mazuri anayotendea taifa
 
definatelly kwa mradi mkubwa kama huo ni benki.........

sasa jamani whats a big deal.....kama mkataba unaonesha perfoming theatres zitakuwa restored tena kubwa .....na wasanii wakaweza kuwa na stalls za kuonesha vitu vyao....tuacheni mawazo mgando!!!....nadhani pia board of trustee wa nyuma ya sanaa wamemshirikisha yule mama wa ki nordic aliyejenga lile jengo na kumkabidhi mwalimu...

tuacheni kuwabana watu wanapoamua kuwekeza pesa zao......nyie ndio mnafanya watu wanaenda kuwekeza ulaya......au south afrika.....waacheni wawekeze hapa..ili turudishe pesa yetu kwenye kodi na ajira...

Hapa tunajadili alivyopata HATA HUO mkopo. MKOPO WOWOOOOTE shurti uwe na DHAMANA. Apart from dhamana BANK TRANSACTION lazime iwe angalau inaendana kwa kitu unachokopa (hapa nazungumzia transactions siyo BALANCE) so $45ml lazima huyu jamaa transactions zake nahisi ziwe -$10ml or +10ml ya kiasi anachokopa.

Swali ni Je.... katoa wapi huo mfumo mpaka kumuwwezesha kukopa kiasi hicho??? Pili Uuzaji wa eneo husika je ulienda kihalali?? Kama ndio MBONA WADAU WENYEWE NDIYO WANAOLALAMIKA??(najua hujasoma ile barua iliyowekwa hapa ya malalamiko kwa Rais) Na je KILE KIWANJA KAMA SERIKALI INGETAFUTA MUWEKEZAJI kwa kufuata taratibu, aidha kwa kutangazwa katika vyombo vya habari, na kilivyo karibu na hoteli ile, NINA UHAKIKA ASILIMIA 1,000,000,000,000,000 Lowasa asinge kipata!! Hata mwenye Movempik (sina uhakika labda NI LOWASA MWENYEWE) na wageni wa pale wangekinunua na kuwekeza zaidi ya tunachokijadili cha $45ml .

Nimewasilisha.
 
definatelly kwa mradi mkubwa kama huo ni benki.........

sasa jamani whats a big deal.....kama mkataba unaonesha perfoming theatres zitakuwa restored tena kubwa .....na wasanii wakaweza kuwa na stalls za kuonesha vitu vyao....tuacheni mawazo mgando!!!....nadhani pia board of trustee wa nyuma ya sanaa wamemshirikisha yule mama wa ki nordic aliyejenga lile jengo na kumkabidhi mwalimu...

tuacheni kuwabana watu wanapoamua kuwekeza pesa zao......nyie ndio mnafanya watu wanaenda kuwekeza ulaya......au south afrika.....waacheni wawekeze hapa..ili turudishe pesa yetu kwenye kodi na ajira...

Waungwana, mbona tunapotosha mada? Hapa suala si kukopa benki, nenda wewe kajaribu kukopa kama utapewa hizo $45.5m. Lazima na wewe uwe na mabilioni benki ndiyo waweze kukukopesha. Suala la msingi ni kuwa kiongozi wa umma huyu Lowassa anatoa wapi pesa kuendeleza mradi wa shilingi bilioni 70 na kununua nyumba London kwa cash shilingi bilioni 1?

Hapa inabidi tuhoji huu utajiri kaupata wapi huyu kiongozi wa umma? Ni kukosa busara eti kumpongeza kwa kuwekeza Tanzania. Kwani Lowassa ni mwekezaji au kiongozi wa umma?

Akiwa kama kiongozi wa umma, serikali ina wajibu wa kuchunguza huu utajiri mkubwa kaupata wapi?

Tusitafute majibu ya haraka ya kusema kakopa benki na kumsifu kuwekeza Tanzania. Let's look at the bigger picture, hii "unexplained wealth" ya huyu Lowassa imetoka wapi?
 
Kama amewekeza Tanzania ni bora mno. Kuna wanasiasa wengi tu wa Tanzania kuanzia CCM mpaka upinzani ambao wanatoa pesa zao nje na ku invest huko na kutengenezea ajira kwa watu wa huko wakati Watanzania wenzetu kibao wako hoi bila kazi.

Inaelekea nguvu kubwa sana inatumika kumwandama Lowassa na kuwaacha majambazi wengine wakitamba bila kuguswa.

Kuna watu wanatumia nguvu kubwa sana kujaribu kuwadanganya Watanzania. Ni sawa Lowassa akikosea lazima aandikwe lakini kusiwe na agenda ya siri ya kuchafua watu tu hata pale ambapo hakuna ubaya wowote.

Nasema hili nikiwa nakumbuka jinsi magazeti hayo hayo yalivyojaribu kutuchafua hata wengine na kutuunganisha na Lowassa kwasababu tu ya kuamua kugombea ubunge. Unaunganishwa na mtu ambaye hujawahi hata kuonana naye maishani, hajawahi hata kukuazima senti tano, hujawahi hata kuongea naye maishani. Mpaka unajiuliza kwanini watu wanaamua kuzua uwongo wote huo? Kwa faida ya nani?

Kama mtu ana ugomvi na Lowassa basi apambane na Lowassa lakini sio kufanya juhudi ya kuwaingiza Watanzania wote kwenye ugomvi huo.
 
We hamna kitu kabisa, HAPA HAJADILIWI LOWASA, inajadiliwa MALI ALIYONAYO LOWASA KAIPATAJE WAKATI AMEKUWA MTUMISHI WA SERIKALI MIAKA YOOOOOOTE HIYO?
Mjadala huu wa leo NDIYO HUKUMU YAKE YA KESHO!!!
Tafakari, hapa hachukiwi mtu ila JIULIZE WAPO WATU WATANZAIA WANGAPI WALIOFANYA KAZI SERIKALINI KABLA na BAADA YA LOWASA (namaanisha watu waliokaa vitengo vizuri zaidi yake lakini walikuwa waadilifu) ambao wanayo hela ya kula tu??/

achaneni na lowassa do your shits....mimi mwenyewe simfagilii lakini naunga mkono wazo la kuwekeza alichonacho nyumbani....miaka ya nyerere tumepotreza mamilioni kupitia kwa watu kama Cleopa Msuya,etc ambao walijifanya wajamaa kumbe wana magorofa JAPAN.....wengine wamedhulumiwa na wazungu na wahindi...sasa bora lipi kama mtu ana access ya kupata mkopo mkubwa au ana pesa si mwacheni ajenge!!!

MnAJuWa tofauti ya ufisadi wa kenya na tanzania miaka ya mwanzo .....ni kuwa hakuna kiongozi wa kenya aliyepeleka pesa zake nje...wote wamewekeza kwenye mashamba ya chai ,kahawa na ufugaji....wakati watanzania wote walikuwa wakikimbiza pesa nje........kwa unafiki wetu!!
Wakati Moi anatoa hotuba ya kuaga pale bungeni mwaka 2002....alisema ..""..nastaafu na nitabaki kukaa Kenya na mara nyingine nitatembea ndani ya afrika mashariki kama arusha au dar au kampala......chochote nilichokipata nikiwa madarakani nimewekeza kwenye nchi yangu..au ndani ya afrika mashariki...sina sababu ya kwenda ughaibuni kama wengine..."
Ujamaa wetu tuliojitahidi kujenga tukashindwa umetujengea unafiki na wivu......tupambane na ufisadi...lakini vile vile tukatae pesa za kodi yetu kuwekezwa nje ya Tanzania....na ni kazi ya TAKUKURU vile vile kuangalia viongozi wanaoweka pesa nje...napendekeza hao wapewe adhabu kubwa zaidi..
 
Mkuu,

Nakubaliana na wewe kabisa hapo juu. Inaelekea watanzania tumeanza kuzidiwa na majungu vichwani mwetu na kuwa na wivu wa ajabu. Kila Mtanzania anayefanya jambo tunamwona ni mwizi wakati wageni wanakuja hapo hawana hata senti tano na baadaye wanakuwa mamilionea.
 
Tusubiri tuone kama hii ni kweli. Nyerere (RIP) alishamjua huyu ni mkwapuaji toka akiwa AICC ndiyo maana alimkataa hata wakati ule. Kwa hiyo hiyo ni fact tusubiri tuone.Hakuna siri sasa ya mafisadi hata wajifiche wapi tutawaona tu
 
achaneni na lowassa do your shits....mimi mwenyewe simfagilii lakini naunga mkono wazo la kuwekeza alichonacho nyumbani....miaka ya nyerere tumepotreza mamilioni kupitia kwa watu kama Cleopa Msuya,etc ambao walijifanya wajamaa kumbe wana magorofa JAPAN.....wengine wamedhulumiwa na wazungu na wahindi...sasa bora lipi kama mtu ana access ya kupata mkopo mkubwa au ana pesa si mwacheni ajenge!!!

MnAJuWa tofauti ya ufisadi wa kenya na tanzania miaka ya mwanzo .....ni kuwa hakuna kiongozi wa kenya aliyepeleka pesa zake nje...wote wamewekeza kwenye mashamba ya chai ,kahawa na ufugaji....wakati watanzania wote walikuwa wakikimbiza pesa nje........kwa unafiki wetu!!
Wakati Moi anatoa hotuba ya kuaga pale bungeni mwaka 2002....alisema ..""..nastaafu na nitabaki kukaa Kenya na mara nyingine nitatembea ndani ya afrika mashariki kama arusha au dar au kampala......chochote nilichokipata nikiwa madarakani nimewekeza kwenye nchi yangu..au ndani ya afrika mashariki...sina sababu ya kwenda ughaibuni kama wengine..."
Ujamaa wetu tuliojitahidi kujenga tukashindwa umetujengea unafiki na wivu......tupambane na ufisadi...lakini vile vile tukatae pesa za kodi yetu kuwekezwa nje ya Tanzania....na ni kazi ya TAKUKURU vile vile kuangalia viongozi wanaoweka pesa nje...napendekeza hao wapewe adhabu kubwa zaidi..

Kwa hiyo fisadi akiiba pesa za umma akaziwekeza Tanzania basi huyo ni mtu safi hajafanya kosa kwani anaendeleza nchi yake?! Hivyo hivyo kwa kiongozi wa umma kama Lowassa kuwa na utajiri mkubwa usioweza kuelezeka ni sawa tu kwa vile anawekeza pesa zake Tanzania? Na hiyo nyumba aliyonunua kwa cash London kwa 1 billion/- kawekeza Tanzania?

Wallahi, Baba wa Taifa angekuwa hai na kusikia Watanzania wanazungumza maneno haya ingemuuma sana.

Wapi maadili ya uongozi wa umma? Wapi maadili kwenye sisi wananchi kwenye jamii ambao baadhi yetu tunahusudu mafisadi na viongozi wa umma wasio waadilifu na wenye utajiri wa mashaka kama Lowassa eti kwa vile wamewekeza Tanzania?

Suala la msingi la kujiuliza na ambalo halikwepeki ni kuwa kiongozi wa umma kama Lowassa anatoa wapi utajiri kama huu? Sheria inataka vyombo vya dola kuwachunguza viongozi wa umma wenye "unexplained wealth." Je, kwa nini Lowassa hachunguzwi?
 
Mh!huyu jamaa ni money monger wa kufa mtu!anaweza kunywa hata uji wa mgonjwa!!
 
EL+RA=UFISADI Nyie mliotumwa na membe acheni hizo.......unaweza kukopa agaist the project....nenda kwa banker wako akuambie....,kinachotakiwa tu uwe na biashara na uwe mtu unayeaminika .,,biashara yako iwe na uongozi imara....mahali unapojenga pawe na title etc......chukulia mfano uwe na site pale posta ..na uwe na business plan inayoeleweka unapata pesa ...msipotoshe watu!!!....that CBD is very lucrative site...na mikopo kama hiyo unaweza kukopa mabenki makubwa makubwa[merchant banks]...sio hizi baadhi ya benki zetu ila ni benki kubwa [investment banks]
....those are called syndicate loans ....kiasi kama $45 million unaweza kuchukua...benki kama tatu zikaungana kukukopesha..ie crdb,stanbic,stanchart,rasilimali,nmb etc......maana kwa level ya tanzania benki zetu kubwa ndio hizo na hata hizo kiasi cha $45 m ni kikubwa......au unaweza kukopa kupitia kwa benki za kimataifa zilizoko nchini kupitia kwa holding banks zao[ie Barclays banks plc etc...]...pia world banks na commonwealth finance[IFC] wana kiteNGo cha mikopo mkikubwa aina hii.....

SHARTI LAO KUU NI KUWA WAO NDIO WATAKUWA WANASIMAMIA MASUALA YA FEDHA HADI MRADI UISHE.....IKIWEMO KUFANYA VALUE FOR MONEY AUDIT MARA KWA MARA....NA JENGO LIKIISHA WANEWEZA KUWEKA PROPERTY MANAGER akakusanya ushuru kutokana na makubaliano ya makato na kiasi kingine unabaki nacho...hadi mkopo uishe ....au kama una uwezo wa kulipa kupitia biashara zako nyingine thats another point....

So naombeni ondokaneni na mawazo ya kuwaogopa watu wanaofanya miradi mikubwa ...mkadhani na nyie hamuiwezi.....na kubaki kulalama.......hakuna mfanyabiashara mwenye uwezo wa kujenga jengo la bilioni 70 kwa kuchukua pesa uvunguni mwa kitanda kama ambavyo tunajenga vibanda vyetu vya room 3 ,bila financing!!....ikitoke hivyo lazima hata INTERPOL na watu wa CIA / FBI anti money laundering watashtuka tu....
 
Last edited by a moderator:
Wagonjwa wa PHOBIA utawajua tu. Wao kila kitu wanaogopa. Hata akijenga ghorofa 70 kwa 800Bl, wewe yanakuhusu nini? After all magazeti yaTanzania ni uzushi mtupu. Nakumbuka gazeti moja liliwahi kuandika kuwa Sumaye anamiliki utajiri wa kutisha kwa njia ya rushwa. Baada ya kufikishwa MCT na mahakamani ili wa-prove walishindwa na ikaamuliwa wamlipe Sumaye mabilion ya fedha ingawa nao walishindwa. Kwa hekima mzee Sumaye aliwasamehe. MAGAZETI YETU NI WAZUSHI, MTU AKIJUA KUANDIKA BARUA YA MAPENZI ANAJIITA MUANDISHI WA HABARI. Hata mzee mwinyi wakati akiwa Rais, tulielezwa kuwa ana mpango wa kuishi uarabuni pindi atakapostaafu, yapo wapi leo? SHAME ON YOU WITH YOUR TABLOIDS

Mkuu kama ni uzushi na uwe uzushi tu. Hapa Tanzania tuna sheria na taratibu za kuyashitaki magazeti zushi, kwa kuwa unasema huu ni uzushi itakuwa poa sana kama hao jamaa wazushi wakichukuliwa hatua. Lakini kama si kweli kuwa ni wazushi, yaani kama kweli Lowassa anataka kujenga nyumba yenye thamani ya Shilingi bilioni 70 hakuna ubaya kuuliza kwa kuwa yeye alikuw amtumishi wa umma mashara wae wote na marupurupu yake halali haayawezi kufika shilingi bilioni 1, sasa anataka kujengta nyumba ya shilingi bilioni 70, kama kweli kuna haja ya kuuliza kama alituibia hela, au alipew zawadi hizo hela. So simple.

Kuna watu walianza kusema Dr Slaa ni muongo, hakuna EPA, kuna mwingine alisema Richmind ni uongo, yalianzia huko huko kwenye vitabloid, lakini yote yakawa kweli.
 
Back
Top Bottom