Lowassa kutowahurumia watendaji wabadhirifu

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
802
Lowassa kutowahurumia watendaji wabadhirifu

Shadrack Sagati, Kyela

WAZIRI Mkuu Edward Lowassa amesema atakuwa mkali kwa watendaji wa halmashauri waliozoea kuiba fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ipinda wilayani hapa, aliwataka madiwani kutofumbia macho watendaji wa jinsi hiyo.

“Ni lazima sasa tuwe tunaangalia mradi wenyewe, siyo mtu anajenga daraja anakwambia limegharimu Sh milioni 20 wakati limegharimu Sh milioni 10, fedha nyingine anagawana na mkandarasi,” alisema Lowassa.

Waziri Mkuu alisema katika hilo, hatakuwa na huruma. Aliwataka wananchi kuwaondoa madarakani madiwani watakaoshindwa kusimamia fedha zao.

Akiwa katika wilaya hiyo, Lowassa aliahidi kuwa ndani ya miezi 18 umeme utawekwa katika vijiji vya Ipinda hadi Matema.

Mradi huo, awali ulikuwa utekelezwe, lakini baadhi ya watu wakatumia utapeli wa kukusudia kwenda mahakamani, hali iliyosababisha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kusimamisha upelekaji wa mradi wa umeme katika vijiji hivyo, alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile alimweleza Lowassa kuwa kuna mtu alijifanya wakili akaandika barua Tanesco kuwa mradi hauwezi kuendelea hadi ilipwe fidia, hali iliyoifanya shirika hilo kuacha kuendelea na mpango wa kupeleka umeme katika eneo hilo.

“Nawaahidi kuwa mimi kwa kushirikiana na Mbunge wenu Dk. Mwakyembe (Harrison) tutahakikisha umeme huo unawekwa ndani ya miezi 18,” alisema Waziri Mkuu na kumwamuru meneja wa shirika kuhakikisha mradi unatekelezwa mara moja.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Hussein Mashimba alisema umeme katika kata za Makwale na Matema ni muhimu, kwani utasaidia utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ya Matema inayohudumia wagonjwa zaidi ya 100 kila siku.

Source: HabariLeo
 
“Ni lazima sasa tuwe tunaangalia mradi wenyewe, siyo mtu anajenga daraja anakwambia limegharimu Sh milioni 20 wakati limegharimu Sh milioni 10, fedha nyingine anagawana na mkandarasi,” alisema Lowassa.

Huyu Mzee ni mtaalam wa shughuli yenyewe maana anajua wazi jinsi ambavyo mafisadi huwa wanatafuna hela ya walipa kodi. Uzoefu huo aliuonyesha kwenye Ricmond, ameishakatiwa chake halafu katulia tuli kama hayupo, akiona magazeti yanaanza kusema kulikuwa na mkono wa kigogo wa serikali anatishia kutumia sheria ya PCCB ya mwaka 2007! Halafu anategemea mafisadi waogope wakati wanajua na yeye mwenyewe ni fisadi?
 
Mbona ile waliyolipwa Richmonduli $172 million bila kufanya kazi yoyote haisemi!? Yeye angekuwa wa kwanza kujifukuza kazi! Usanii tumeuchoka!
 
Fisadi amshughulikie fisadi mwenzake, DANGANYA TOTO.

nilivyotoa Cv ya Lowassa kipindi kile nadhani sasa mmeanza kuamini,Alisomea usanii wa kucheza ngoma ila baada ya kumshinda ikabidi awe mbunifu katika fani ya kutuibia pesa.

wewe unaddhani mambo ya kudoble the amount mzee kaanza leo,ni mda na mvi zake hizo ..
 
Lowassa kutowahurumia watendaji wabadhirifu

Shadrack Sagati, Kyela

WAZIRI Mkuu Edward Lowassa amesema atakuwa mkali kwa watendaji wa halmashauri waliozoea kuiba fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ipinda wilayani hapa, aliwataka madiwani kutofumbia macho watendaji wa jinsi hiyo.

"Ni lazima sasa tuwe tunaangalia mradi wenyewe, siyo mtu anajenga daraja anakwambia limegharimu Sh milioni 20 wakati limegharimu Sh milioni 10, fedha nyingine anagawana na mkandarasi," alisema Lowassa.

Waziri Mkuu alisema katika hilo, hatakuwa na huruma. Aliwataka wananchi kuwaondoa madarakani madiwani watakaoshindwa kusimamia fedha zao.

Akiwa katika wilaya hiyo, Lowassa aliahidi kuwa ndani ya miezi 18 umeme utawekwa katika vijiji vya Ipinda hadi Matema.

Mradi huo, awali ulikuwa utekelezwe, lakini baadhi ya watu wakatumia utapeli wa kukusudia kwenda mahakamani, hali iliyosababisha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kusimamisha upelekaji wa mradi wa umeme katika vijiji hivyo, alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile alimweleza Lowassa kuwa kuna mtu alijifanya wakili akaandika barua Tanesco kuwa mradi hauwezi kuendelea hadi ilipwe fidia, hali iliyoifanya shirika hilo kuacha kuendelea na mpango wa kupeleka umeme katika eneo hilo.

"Nawaahidi kuwa mimi kwa kushirikiana na Mbunge wenu Dk. Mwakyembe (Harrison) tutahakikisha umeme huo unawekwa ndani ya miezi 18," alisema Waziri Mkuu na kumwamuru meneja wa shirika kuhakikisha mradi unatekelezwa mara moja.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Hussein Mashimba alisema umeme katika kata za Makwale na Matema ni muhimu, kwani utasaidia utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ya Matema inayohudumia wagonjwa zaidi ya 100 kila siku.

Source: HabariLeo

Huyu ndiye Lowassa...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom